Nsennah
JF-Expert Member
- Jan 9, 2021
- 1,921
- 1,542
Utangulizi
Somo la hisabati (mathematics) ni moja kati ya masomo yaliyoko kwenye mtaala wa masomo Tanzania kwa kidato cha kwanza hadi cha nne. Kutokana na umhimu wake kwa mtu binafsi, jamii na taifa kwa ujumla, somo hili ni msingi kwa kila mwanafunzi katika ngazi hiyo kulisoma na kufanyiwa upimaji katika mitihani. Licha ya umhimu wake, somo hili limekuwa changamoto katika ufaulu wake kwa wanafunzi wengi hivyo kudidimiza juhudi za kuwa na jamii yenye wajuvi na wataalamu wa somo hili.
Hali ya ufaulu kwa sasa
Kwa takwimu za hivi karibuni, zinaonesha ufaulu wa somo hili umekuwa wa chini sana ukilinganisha na ufaulu wa masomo mengine ya msingi. Mwaka 2022, Masomo yote ya msingi yalikuwa na ufaulu wa juu ya wastani isipokuwa somo la hisabati, mwaka 2023 bado somo la hisabati liliendelea kuwa chini kiufaulu licha ya kupanda ukilinganisha na mwaka 2022. Hata miaka ya nyuma 2016-2020 bado hali ya ufaulu wa somo hili ulikuwa chini ya wastani wa 25% ya ufaulu kwa watahiniwa. Hesabu zaendelea kuwatoa jasho wanafunzi kidato cha nne Tanzania - Nukta Habari
Changamoto chochezi
Wadau wa elimu na asasi mbalimbali walishaorodhesha changamoti kadha wa kadha kama vile:
-- upungufu wa walimu wa somo ukilinganisha na idadi ya wanafunzi
-- mtazamo hasi wa wanafunzi juu ya somo hili (jamii inavyolizungumzia somo kuwa gumu).
-- kukosa kufanya mazoezi mengi kwani somo linahitaji kufanya mazoezi ama maswali mengi
-- upungufu wa ubunifu wa njia nyepesi katika kufanya maswali ya hisabati
-- wingi wa mada katika somo la hisabati ambazo zote zinauwezekano wa kupimwa katika mtihani wa mwisho.
Suluhisho
Ni wazi kuwa somo la hisabati linahitaji mazoezi na kufanya maswali mengi hivyo basi kuelekea Tanzania tuitakayo yenye mtaala mpya, ni bora tukafanya mageuzi kadha wa kadha ili kukabiliana na tatizo hili la ufaulu hafifu katika somo la hisabati. Moja ya mageuzi hayo ni:
-- Kuendelea na juhudi za kutatua changamoto ya uwiano uliopo kati ya mwalimu na wanafunzi anaowahudumia. Ni wazi kuwa ni rahisi elfu kumi kushibisha mtu mmoja kuliko watu watano kwa chakula cha aina ile ile. Hivyo serikali haina budi kubeba jukumu la kuongeza idadi ya walimu kulingana na wanafunzi wanaohitaji huduma.
-- Matumizi ya tehama wezeshi kwa wanafunzi. Kwenye somo la hisabati, wahanga wakubwa ni wanafunzi hivyo ni vyema serikali ikaweka vifaa vya tehama ambavyo ndani yake kutawekwa video zinazoelezea mada mbalimbali za somo la hisabati zilizoko kwenye mtaala wetu. Hii itachangia zaidi wanafunzi kujihusisha (interact) na somo kuliko wanavyofundishwa darasani tu. Mwanafunzi kwa muda wake wa ziada ataweza kwenda kwenye kompyuta na kujikumbusha mada za nyuma mfano wa kidato cha 4 kujikumbusha logarithm ya kidato cha 2. TWAWEZA wanaweza kutusaidia kutafuta takwimu ilivyo mbaya kwa mwanafunzi wa kidato cha 4 alivyosahau ya kidato cha 2.
--Kuandaa bajeti ya kununua zana za kujifunzia katika somo hili katika shule za serikali. Ni wazi kuwa ni rahisi kukuta vifaa vya kujifunzia kwa masomo yote ya sayansi ila usikute kifaa hata kimoja cha kujifunzia hisabati. Maumbo ya kujifunzia mada kama 3D figures, geometry n.k yanamlazimu mwalimu ndo atengeneze hivyo kukuta alichokitengeneza si imara na wala hakivuti umakini wa anayejifunza. Ni vyema kukawepo bajeti ya kununua vifaa hivi mashuleni.
-- Kuwepo na mtihani wa taifa kwa vitendo wa somo la hisabati (practical examination). Katika masomo yote, ni wazi kuwa hisabati ni somo linalotakiwa kufundishwa ama kujifunza zaidi kwa vitendo ndiyo maana kunasisitizwa uwepo wa zana toshelezi za kujifunzia na kufundishia. Kila mada ndani ya somo la hisabati kuna shughuli (activity) ambazo mwanafunzi anatakiwa kuzifanya, kwa dhana hii ni ngumu mtoto anafika kwenye mtihani vifaa anavyoruhusiwa kuvitumia ni rula, bikari, kalamu na four figure. Kufanyika mtihani wa vitendo utawafanya wanafunzi kujihusisha na mahesabu zaidi kuliko kukariri formula zote. Nitaeleza zaidi kuhusu hili kwa kutoa mifano ya mada (mahiri) zinazoweza kufanyika kwa vitendo.
1. Geometrical transformations: kama kwenye fizikia tunaweza kufanya majaribio ya kisayansi kwenye mada kama kuakisi kwa mwanga (reflection of light) inashindikana vipi kufanya majaribio ya Reflection na rotation kwenye hisabati kuliko kuwafanya wanafunzi kukariri njia (formula) za kutumia sine na cosine? Tulitafakari hili.
2. Three dimensional figures. Mada hii inahusisha maumbo ambayo mwanafunzi anahitaji kuona na kuyagusa zaidi kuliko fikra na taswira ya kichwani, nishukuru kupitia mafunzo ya SEQUIP kuna mwalimu alikiri kuwa mada hiyo kaielewa vizuri kwenye mafunzo hayo kwa sababu ilifanyika kwa vitendo na vifaa vikawa vinaonekana kuliko ya kuchorewa ambapo karatasi haiwezi kuonesha uhalisia wa 3D. Kama mwalimu alikuwa hivyo, piga picha kwa mwanafunzi anayefundishwa naye.
3. Congruence and similarity: kwa kutumia vifaa na kwa vitendo, mwanafunzi ataweza kujua maumbo yapi ni ya kufanana na yapi ni ya kulingana kila kitu kuliko kukariri theorems zote kwa maumbo dhahania tu unayoundiwa maneno uchore au wachore uanze kunyambua mwenyewe.
4. Areas and volumes. Kwa kuwa lengo ni mwanafunzi ajue uhalisia wa eneo na ujazo wa maumbo, ni vyema mwanafanzi akafanya kwa vitendo huku akiliona umbo husika kuliko kumwambia kutafuta ujazo wa tufe ( sphere ) ambalo halionekani. Mpe mwanafunzi apime kipenyo mwenyewe ndipo atafute ujazo. Hapo nimechukulia kama mfano tu.
5. Probability. Mada kama hii tunaweza kutumia vifaa kadha wa kadha kwa vitendo. Mfano wa vifaa kama hivyo ni sarafu (coin), die, karata (cards), mifano ya mipira midogo midogo yenye rangi tofauti n.k kupima uelewa wa mwanafunzi juu ya uelewa wake kuhusu mada hii kuliko kuleta maswali ya mwanafunzi kukariri tu die tulifundishwa iko namna fulani.
Moja ya faida za mtihani wa vitendo ni kupunguza idadi ya mada zinazoweza kuulizwa (33 examination contents) kwenye mtihani mmoja ambao unampa mzigo mzito mwanafunzi kufanya maandalizi vizuri
Source. CSEE FORMAT 2019.
Hitimisho
Tanzania siyo kisiwa hivyo ni vyema tukajitafakari kuwa kama tunafanya majaribio ya kutambua na kuchora sehemu za ua, kujaribu kama mchanganyo fulani una kundi fulani la chakula, sampuli hii ina hiki na kile ni kwa nini tusipime uwezo wa mwanafunzi kama anajua vipimo vya maumbo ili asiambiwe mara kwa mara "Injinia soma hiyo". Kupitia uwepo wa kufanya hisabati kwa vitendo itawafanya wanafunzi kulipenda somo maana wanahusisha milango mingi ya fahamu, itawapunguzia hali ya kukariri sana, na vitendo vitawafanya kuhusianisha somo na mazingira pamoja na maisha yao ya kila siku na mwishowe kulipenda somo hili.