Mwanagenzi
JF-Expert Member
- Sep 11, 2006
- 728
- 253
Hii ni habari nzito iliyokuwa inasubiriwa...
Kwa kuwa tumekuwa na matatizo sana kwenye mikataba, sijui na mradi huu utasalimika!
Ni kampuni ile ile walioshinda tenda zamani wakanyimwa ikawa kesi? Au ni zabuni mpya?
Vitambulisho vya taifa Tanzania kugharimu Sh192bilioni
Na Simon Berege, Dodoma, MWANANCHI
SERIKALI imetangaza rasmi kuanza kutekelezwa kwa mradi wa taifa wa kutengeneza vitambulisho vya raia wa Tanzania walimo ndani na nje ya nchi pamoja na wakazi wasio raia waishio nchini utakaogharimu jumla ya Dola za kimarekani 152 milioni sawa na Sh192bilioni.
Waziri wa Mambo ya ndani, Joseph Mungai alisema mjini hapa jana kwamba mradi huo unaoanza mara moja ulipitishwa na kikao cha Bazara za Mawaziri kilichoketi Februari 2 mwaka huu mjini hapa chini ya Rais Jakaya Kikwete. Mchakato wa maandalizi yake ulianza mwaka 1995 na unatarajiwa kukamilika mwaka 2009.
Akizungumza na Wanahabari kwenye ofisi za Bunge, Mungai alieleza kwamba vitambulisho hivyo vipya vitatumia teknolojia ya Smart Card ambayo ina uwezo wa kuingiza taarifa nyingi za muhusika zinazoweza kutumika kurahisisha huduma mbalimbali kwa mwenye kitambulisho.
Teknolojia ya Samart Card ni ya kisasa zaidi kwani inaweza kubeba picha ya mwenye kitambulisho, alama za dole gumba, alama za kiganja, taarifa za DNA (chembechembe za urithi) , vipimo vya ndani ya macho, taarifa za elimu na nyingine, alieleza Waziri Mungai na kuongeza kwamba teknolojia hiyo imeonekana kufanikiwa sana katika nchi ya Malaysia ambako walikwenda kujifunza.
Akifafanua zaidi Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Lawrence Masha, alisema kwamba uzuri wa teknolojia hiyo mtu anaweza kuamua ni taarifa zipi zisomwe na nani kama zile zinazohusu DNA, Afya, Uhalifu, Elimu, Benki na nyinginezo.
Kwa mfano alisema si lazima mtu wa benki ajue kwamba una-typhoid, au ukienda polisi si lazima wajue mambo yako mengine alieleza Masha na kuongeza kwamba teknolojia hiyo pamoja na kuwa nzuri kuliko ile ya Barcode ambayo ilitumika katika kutengeneza vitambulisho vya kupigia kura ni ya gharama nafuu.
Kama tungekuwa tumetumia smart card kuandikisha kadi za kura ingekuwa rahisi sana kutekeleza mpango huu kwa sasa...kwa kutumia Smart card unaweza kuongeza taarifa wakati wowote tofauti na barcode alifafanua Waziri Mungai na kubainisha kwamba Benki ya dunia imeshakubali kusaidia Dola 20 milioni kufanikisha mpango huo.
Mungai alieleza kwamba katika mradi huo raia waishio nchini na wale wanaoishi nje ya nchi watapewa vitambulisho na wasio raiai ambao wanafanya shughuli mbalimbali hapa nchini watapewa vitambulisho vitakavyowatambulisha wao na utaifa wao.
Alisema mradi huo utakuwa wa kitaifa kama ulivyo wa uchaguzi mkuu na wa sensa ambao utapewa vyenzo za kuukamilisha kwa kuzingatia ratiba maalum ya utekelezaji inayoanza mwezi huu na kukamilika mwaka 2009.
Katika kuhakikisha kwamba utekelezaji wake unakwenda vyema Waziri huyo alisema kwamba utaundwa Wakala wa Usimamizi wa Vitambulisho (National ID Management Agency) unaojitegemea kwa ajili ya kuendesha mradi huo chini ya Wizara ya Mambo ya ndani kwa kushirikiana na wadau wengine.
Alisema Mradi huo utaongozwa na Kamati ya Usimamizi ya Makatibu Wakuu na Wakuu wa Idara na vitengo vinavyohusiana na mambo muhimu kwa vitambulisho vya taifa ambayo pamoja na mambo mengine itatoa mwongozo na mwelekeo wa programu za mradi.
Kazi nyingine ya kamati hiyo itahusu ufuatiliaji wa mchakato wa mabadiliko ya menejimenti, kuidhinisha bajeti ya mipango ya utekelezaji, kuhakikisha kwamba fedha zilizotengwa kwa ajili ya programu husika na kufanya mapitio ya utekelezaji wa mipango kamambe wa shughuli mradi.
Waziri Mungai alieleza kwamba kutokana na makisio yaliyomo kwenye bajeti ya mwaka 2006/07 jengo maalum limetengwa kwa ajili ya mradi huo na watendaji wakuu wa Wakala wa usimamizi wa vitambulisho watateuliwa bila kuchelewa.
Wizara ya mambo ya ndani inachukua fursa hii kutoa wito kwa wananchi waliopo ndani na nje ya nchi na wageni waliopo nchini kutoa ushirikiano ili kufanikisha utekelezaji wa mradi huu muhimu kwa taifa alitoa rai Mungai na kubainisha kwamba vitambulisho hivyo vitatolewa bure.
Mradi huo utatekelezwa katika hatua mbili ambazo ni ya maandalizi na nyingine ni ya utekelezaji. Ratiba ya awamu ya kwanza inaonesha kwamba shughuli ya uanzishaji Wakala wa Usimamizi wa Vitambulisho na uteuzi wa watendaji wakuu na uimarishaji wa kiutendaji wa kuazimwa watumishi wengine kutoka idara za serikali vinapaswa kukamilika katika kipindi cha Februari na Aprili mwaka huu.
Kwa upande wa ukamilishaji wa makusanyo ya fedha zinazohitajika kutoka bajeti ya Serikali, wahisani na vyanzo binafsi utatekelezwa kati ya Marchi na Mei mwaka huu wakati Kampeni ya kufahamisha umma kupitia vyombo vya habari, mikutano ya hadhara, semina na mikutano ya ndani itafanyika kuanzia Aprili mwaka huu hadi Juni 2008.
Ratiba hiyo inaonesha kwamba mapitio (review) ya sheria husika na kufanya marekebisho inapobidi yatafanyika katika kipindi cha Februari hadi Mei 2007 wakati jukumu la kujenga uwezo katika ngazi mbalimbali litafanywa na ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma kati ya Julai na Desemba 2007.
Hatu ya pili ambayo ni ya utekelezaji wa mradi itahusisha utambuzi na uandikishwaji itafanyika kati ya Julai na Desemba mwaka huu ikihusisha ukusanyaji wa taarifa mbalimbali, uundaji wa kamati za utambuzi, Uchapishaji wa kadi za vitambulisho, usambazaji na utoaji wa kadi za vitambulisho na uanzishaji wa rejista za utambuzi.