waziri2020
Senior Member
- May 31, 2019
- 197
- 468
Wanacha wa tlp wachachama mikoani wamkalia mwenezi kooni
Pia soma > Msajili wa Vyama vya Siasa alalamikiwa kusimamia uchaguzi feki wa TLP
TAARIFA KWA UMMA YAH: KUTOLEA UFAFANUZI WA UHALALI WA UCHAGUZI ULIOFANYIKA JUZI TAREHE 02/02/2025 KATIKA UKUMBI WA MRINA HOTEL TIP TOP MANZESE
Ndugu wanahabari, wanachama wa TLP na watanzania kwa ujumla, napenda kuwafahamisha ya kwamba baada ya kufanyika kwa uchaguzi tajwa hapo juu tumepokea malalamiko kwa wanachama na wajumbe wa mkutano mkuu na halmashauri kuu na wanachapa wa TLP (Tanzania Labour Party) wakilalamikia kukiukwa kwa utaratibu wa kuitishwa kwa mkutano mkuu ulioitishwa na kaimu mwenyekiti na katibu wake.
Ndugu wanahabari, wajumbe wa mkutano mkuu na halmashauri kuu pamoja na wanachama kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani wameshangazwa na wajumbe feki waliohudhuria mkutano huo huku wajumbe halali wakiwa wameachwa mikoani bila hata taarifa.
Kwa taarifa tulizonazo watu waliohudhuria mkutano huo sio wanachama wa chama cha TLP bali ni mamluki waliookotwa mtaani na kuvalishwa Tshirt za chama kwa sababu ya ukiukwaji huo tumeamua kuchukua hatua zifuatazo.
1. Tumemuandikia msajili wa vyama vya siasa barua ya kupinga uhalali wa mkutano huo.
2. Wajumbe wote kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani wamepinga kwa maandishi na kuziwasilisha kwa msajili wa vyama vya siasa.
3. Tunakusudia kuwaburuza mahakamani kaimu mwenyekiti na katibu wake walioitisha mkutano huo waende kueleza mahakama namna walivyokiuka katiba ya chama na kufanya uchaguzi usio halali na kesi hiyo itasimamiwa na jopo la mawakili wasiopungua sita (6)
4. Pia wanachama wamependekeza mahakama kutowatambua uongozi huo na kuweka zuio kujihusisha na shughuli zozote za chama mpaka kesi ya msingi itakaposikilizwa
5. Kwasasa chama kinaomba wanachama wake wawe na utulivu nakuendelea na taratibu za kujenga chama katika ngazi ya tawi, shina, kata jimbo, wilaya na mkoa.
6. Tunaomba wanachama na watanzania wote wanaoitakia mema chama cha TLP wawe watulivu wakati huu ambapo tunasubiria majibu ya rufaa kutoka kwa msajili wa vyama vya siasa na utaratibu wa mahakama kukamilika, tutaendelea kuwapa taarifa za mara kwa mara kuwajulisha kinachoendelea
Hali ilivyokuwa awali wakati wa Uchaguzi Februari 2, 2025
Chama Cha Tanzania Labour - TLP kimefanya Uchaguzi Mkuu wa Kuziba Pengo la Aliyekuwa M/kiti wa Chama hicho marehemu Augustine Lyatonga Mrema aliyefariki Dunia ambapo wajumbe Kutoka Mikoa yote ya Tanzania bara na Visiwani walimchagua Kwa Kura zote aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho Richard Lyimo kuwa M/kiti wa Chama hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuchaguliwa Bw. Lymo amesema kazi yake ya kwanza ni kwenda kuwaunganisha wanachama wote wa TLP katika mikoa yote nchini lakini pia kujipanga kuelekea Uchaguzi Mkuu wa October mwaka huu.
=================
CHAMA cha Tanzania Labour Party (TLP), kimemchagua Richard Lyimo, kuwa mwenyekiti mpya wa chama hicho atakayeongoza kwa miaka mitano ijayo huku wanachama 21 wakifukuzwa uanachama.
Ikumbukwe kuwa tangu alipofariki aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Agustino Mrema, mwaka 2022, nafasi hiyo ilikuwa inakaimiwa na Hamad Mkadamu.
Lyimo alichaguliwa katika mkutano mkuu wa Chama cha hicho, uliofanyika jana Dar es Salaam ukijumuisha wajumbe 84.
Katika uchaguzi huo, Lyimo alikuwa mgombea pekee katika nafasi hiyo ya Mwenyekiti na kabla ya kuchaguliwa katika nafasi hiyo mpya, alikuwa Katibu Mkuu wa TLP.
Kwa upande wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara, aliyechaguliwa ni Johari Hamis, ambaye naye katika kinyang`anyiro hicho alikuwa mgombea pekee.
Kadhalika, mkutano huo kwa kauli moja, uliridhia kuwafuta uwanachama, wanachama 21 wa chama hicho, wakiwamo viongozi wanaodaiwa waliofanya majaribio ya kuandaa mikutano miwili ya kuchaguana kinyume cha chama chao hicho kwa ajili ya kuziba nafasi iliyokuwa imeachwa wazi na Mwenyekiti wa chama hicho Agustino Mrema, aliyefariki mwaka 2022.
Miongoni mwa wanachama na viongozi waliofukuzwa uanachama ni Dominata Rwechangura ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti Bara wa chama hicho, Ivan Maganza, aliyekuwa Mwenyekiti wa vijana taifa wa chama hicho na Mariam Kassin.
Wengine waliofukuzwa ni Riziki Nganga, Stanley Ndumagoba, Mary Mwaipopo, Mohamed Mwinyi, Laurian Kazimiri, Nataria Shirima, Kinanzaro Mwanga, Godfrey Stivin na Rashid Amiri.
Pia, wapo Twaha Hassan, Tunu Kizigo, Damari Richard, Hamad Alawi, Mohamed Hemed, Mariam Hamis, Mussa Fundi, Mwajuma Mussa na Osward Nyoni.
Baadhi ya wanachama waliofukuzwa walipoulizwa, walikana kuutambua mkutano huo wakidai haukufanyika kisheria huku wakisisitiza kuwa wao bado ni viongozi.
Naibu Msajili wa vyama vya siasa, Sisty Nyahoza, alithibitisha kwamba mkutano huo uliomchagua Lyimo na wenzake pamoja na kuwafukuza baadhi ya wanachama hao ulifanyika kihalali.
Pia, aliwata wenye malalamiko kuhusiana na chochote kilichofanyika katika mkutano huo, wampelekee malalamiko yao.
“Mkutano ulifanyika kihalali na aliyeuitisha anatambuliwa kikatiba na taratibu za chama chao na walishatoa taarifa, kwa hiyo yote yaliyofanyika ni halali na yana baraka kutoka kwa wajumbe wa mkutano, wenye malalamiko waniletee kwa kufuata utaratibu, nitayashughulikia,”alisema Nyahoza.
Pia soma > Msajili wa Vyama vya Siasa alalamikiwa kusimamia uchaguzi feki wa TLP
TAARIFA KWA UMMA
Ndugu wanahabari, wanachama wa TLP na watanzania kwa ujumla, napenda kuwafahamisha ya kwamba baada ya kufanyika kwa uchaguzi tajwa hapo juu tumepokea malalamiko kwa wanachama na wajumbe wa mkutano mkuu na halmashauri kuu na wanachapa wa TLP (Tanzania Labour Party) wakilalamikia kukiukwa kwa utaratibu wa kuitishwa kwa mkutano mkuu ulioitishwa na kaimu mwenyekiti na katibu wake.
Ndugu wanahabari, wajumbe wa mkutano mkuu na halmashauri kuu pamoja na wanachama kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani wameshangazwa na wajumbe feki waliohudhuria mkutano huo huku wajumbe halali wakiwa wameachwa mikoani bila hata taarifa.
Kwa taarifa tulizonazo watu waliohudhuria mkutano huo sio wanachama wa chama cha TLP bali ni mamluki waliookotwa mtaani na kuvalishwa Tshirt za chama kwa sababu ya ukiukwaji huo tumeamua kuchukua hatua zifuatazo.
1. Tumemuandikia msajili wa vyama vya siasa barua ya kupinga uhalali wa mkutano huo.
2. Wajumbe wote kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani wamepinga kwa maandishi na kuziwasilisha kwa msajili wa vyama vya siasa.
3. Tunakusudia kuwaburuza mahakamani kaimu mwenyekiti na katibu wake walioitisha mkutano huo waende kueleza mahakama namna walivyokiuka katiba ya chama na kufanya uchaguzi usio halali na kesi hiyo itasimamiwa na jopo la mawakili wasiopungua sita (6)
4. Pia wanachama wamependekeza mahakama kutowatambua uongozi huo na kuweka zuio kujihusisha na shughuli zozote za chama mpaka kesi ya msingi itakaposikilizwa
5. Kwasasa chama kinaomba wanachama wake wawe na utulivu nakuendelea na taratibu za kujenga chama katika ngazi ya tawi, shina, kata jimbo, wilaya na mkoa.
6. Tunaomba wanachama na watanzania wote wanaoitakia mema chama cha TLP wawe watulivu wakati huu ambapo tunasubiria majibu ya rufaa kutoka kwa msajili wa vyama vya siasa na utaratibu wa mahakama kukamilika, tutaendelea kuwapa taarifa za mara kwa mara kuwajulisha kinachoendelea
KATIBU MUENEZI TLP TAIFA
GEOFREY STEPHEN PAULO
====================================