Tanzania kwanini ni wazito kufuata taratibu?

Ni wagumu kufuata utaratibu kwa sababu sheria Tanzania ni kisu cha mkate, si msumeno. Leo unafanya kosa hufanywi chochote, kesho unafanya unanyooshewa tu kidole, keshokutwa unafanya unatoa rushwa, mtondogoo unaiba unaambiwa rudisha, kwa hiyo hakuna hofu juu ya madhara ya kufanya makosa. Na tabia hii pia inaanzia kwenye taasisi za malezi hasa nyumbani na shuleni. Mtoto hafundishwi kuwa kila kosa lina matokeo. Mwanafunzi anapewa mtihani, anaambiwa ajibu maswali mawili, yeye anajibu matatu na hafanywi chochote. Tena mivyuo mingine inamwambia mwalimu asahihishe yote matatu halafu achague mawili yenye alama za juu! Hii nchi ni kama jehanam kwa watu waliostaarabika wanaofata sheria. Ukiwa dereva ukafata sheria za barabarani uwezekano wa kugongwa au kufika nyumbani kesho ni mkubwa, achilia mbali matusi na kejeli. Unasimama nyuma ya zebra cross watu wavuke, nyuma huko anakuja dereva mwenzio "mstaarabu" amekanyaga mafuta ya kutosha halafu anawapigia honi wavukaji wampishe haraka iwezekanavyo. Anashika breki za ghafla, anashusha kioo anamwaga matusi!! Waenda kwa miguu nao ni hadithi nyingine ndefu. Boda boda mmeshasema. Huko kwenye taasisi nako ukifata taratibu nako inakula kwako. Ni kujifunza tu uvumilivu na kutokulalamika maana unaweza kupata maradhi yatokanayo na stress.
Kwa hiyo tuiite nchi ya wahuni kama mchangiaji mmoja alivyotuita
 
Unaichezea CCM Kwa kuwaharibu watanzania Akili? Miaka 50 ya Uhuru shida kibao watanzania wanafurahi
 
Nadharia inaanza kuharibikia kwenye salamu.

MAMBO→POA.

Maana yake kila kitu poa tu, hata kama unamawazo ni poa.

Mambo sio poa kama unavyochukulia na unavyojibu.
 
kwanzia viongozi hadi wananchi wa kawaida wote awafati taratibu na sheria.Hili ni janga la kitaifa
 
Back
Top Bottom