Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,037
- 4,752
Zamani tulifundishwa tusiwaseme vibaya viongozi wa dini; tukaishi na huo utamaduni na kutufanya kushindwa kulijenga kanisa la kweli na uislamu wa kweli.
Kutokana na kufundishwa kuwa waongo mbele ya viongozi wa dini ilituwia ngumu kuwakemea pale wanapokosea. Tukawa tunakwenda kanisani na misikitini kumwomba Mungu lakini hatuna mamlaka yakukemea maovu yanayopelekwa au kufanywa na viongozi wa dini katika nyumba hizi takatifu.
Viongozi wa dini walipozidi kuzeeka wakatamani zaidi maisha nje ya kanisa na msikiti na wakaambatana na siasa kwa kisingizio cha haki ya kuchagua na kuchaguliwa.
Dhambi ilipokomaa ikapelekea sasa viongozi wa dini waanze kutoa rushwa na kujipendekeza waweze kukubalika kisiasa. Tumeona Kenya kuelekea uchaguzi wanasiasa wote waligeuka miungu kwenye nyumba za ibada. Mahubiri yanapewa muda wa nusu saa na hotuba z wanasiasa zinapewa lisaa. Baada ya uchaguzi wanasiasa wote wa Kenya wameondoka kanisani wapo wanakula maisha.
Tanzania napo tumeona viongozi wa dini wakifanya kufuru; viongozi wa dini wa Tanzania wamekosa subira ofisini kwao na sasa wanaomba mwaliko kwenda kuwaona viongozi wa kisiasa.
Viongozi wa dini wa Tanzania wanatembea na waandishi wa habari kwenda kwenye ofisi za wanasiasa. Viongozi wa dini wanafurahia kupiga picha na wanasiasa kuliko kupiga picha na waumini.
Kibaya zaidi hakuna kiongozi wa Dini Tanzania aliyeachwa salama. Viongozi wote wametekwa na mamlaka za Duniani na wameacha Mungu awe mpweke.
Nimeandika haya kama malaika anayekuja kulionya kanisa na nyumba nyingine za ibada. Tuiache nyumba za ibada zibaki na hadhi yake. Wanasiasa msipowakwepa viongozi wa dini natabiri Tanzania inakwenda kuwa na watu wakatili waliokosa roho wa Mungu ndani yao.
Leo kuna waumini wameacha kwenda nyumba za ibada kwa sababu wanaona kabisa kwamba wanapoteza Muda bora waswali wakiwa nyumbani kwao. Haya yote yamesababishwa na mambo matatu
1. Tamaa
2. Umaskini
3. Kufanya dini iwe ajira