Tanzania kupewa Tsh. Bilioni 779.9 kutoka Benki ya Dunia kwaajili ya utekelezaji wa Mradi wa TASAF

Mtoa Taarifa

JF-Expert Member
Sep 21, 2024
210
659
Benki ya Dunia imeahidi kutoa kiasi cha takribani Dola za Marekani milioni 300 kwa ajili ya kusaidia Awamu ya Tatu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini nchini chini ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania ( @tasaf.tanzania ) ambayo inatajiwa kutekelezwa baada ya kukamilika kwa Awamu ya Pili ya Mpango huo mwaka

Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini, Bw. Nathan Belete katika Mjadiliano ya Ngazi ya Juu kati ya Serikali na wadau wa maendeleo kuhusu mustakabali wa Awamu ya Tatu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini chini ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF).

Bw. Belete alisema wameamua kutoa fedha hizo kwakuwa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unatekelezwa na TASAF ni mfano wa kuigwa duniani kwasababu umechangia kukabiliana na umaskini na kuonesha matokeo chanya .

Aliipongeza Serikali kwa mafanikio mbalimbali iliyoyapata kupitia Awamu ya Kwanza na ya Pili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini chini ya TASAF na kuahidi kuwa benki hiyo kwa kushirikiana na washirika wengine wa maendeleo wataendelea kushirikiana na Serikali kuhakikisha inafikia malengo yake hususan ya kuwawezesha wananchi kukabiliana na umaskini.

Naye Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba (Mb), ambaye aliongoza majadiliano hayo, alisema Awamu ya Tatu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini itakuwa na mpango jumuishi utakao endana na Dira ya Maendeleo ya Taifa inayoandaliwa ya 2025 -205

Alisema utakuwa mpango jumuishi kwa kuwa hatuo acha mtu yoyote nyuma kwa kuhakikisha kuwa unawezesha wananchi wa hali ya chini kujumuishwa katika mpango mkuu kwa kushiriki katika miradi mbalimbali inayoendelea nchini.

“Uandaaji wa Mpango wa Tatu wa TASAF utahusisha shughuli za uzalishaji ambazo hazita bagua sehemu ya jamii yetu, makundi yote yatahusishwa katika shughuli za maendeleo na mgawanyo wa bajeti kwa ajili ya maendeleo hayo ”, alisema Dkt. Nchemba.

Alisema Awamu ya Tatu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini inaandaliwa baada ya mafanikio makubwa yaliyopatikana katika Mpango wa Kwanza na Wapili ambapo kumekuwa na shuhuda mbalimbali kutoka kwa wanufaika ambao vipato vyao vimeongezeka kutoka hatua moja kwenda nyengine kwa kuoonesha shughuli walizo fanikiwa kuzifanya.

WIZARA YA FEDHA
 
Back
Top Bottom