SoC03 Tanzania inaweza kutokomeza tatizo la kukata kwa umeme

Stories of Change - 2023 Competition
Jan 12, 2021
9
9
Utangulizi: Ndani ya makala hii viongozi na watanzania wote wataweza kutambua sababu za kwa nini Tanzania inaweza kutokomeza tatizo la kukata kwa umeme ovyo ovyo.

Tanzania ni nchi ambayo ni miongoni mwa ñchi zinazoendelea. Pia ni nchi ambayo bado haijaimarisha miundo mbinu ya nishati ya umeme. Hivyo Kuna haja ya Kila mtanzania kuchunguza kwa makini makala hii makini.

Mabadiliko ya kweli yataletwa na yule aliyeadhimia kuelewa kile kilichomo ndani ya makala hii.

FAHAMU SABABU MUHIMU ZA NCHI YA TANZANIA ZINAZOWEZA KUIFANYA ISIWE NA TATIZO LA KUKATA KWA UMEME OVYO OVYO

1. UPATIKANAJI WA UPEPO WA KUTOSHA NCHINI

Nchi yetu ya Tanzania imebahatika kuwa na upepo wa kutosha, hivyo haiwezekani kuwa na umeme wa kusuasua.

Wakati mimi bado nasoma shule ya msingi nilifundishwa na mwalimu wangu wa somo la sayansi kuwa upepo nao huzalisha umeme unaoweza kutumika kwa shughuli mbalimbali. Jambo linalostaajabisha ni kwamba nchi yetu bado ina tatizo la kukata kwa umeme na pengine kutokuwepe kwa nishati ya umeme katika baadhi ya maeneo.

Kati ya fursa ya kuzalisha umeme tuliyopewa hapa Tanzania ni upepo. Hivyo waziri wa nishati na madini akisaidiwa na kamati yake wakae na kufikiri juu ya kuweka vinu upepo Kila mahali ili angalau kupunguza ukatikaji wa umeme na kusababisha shughuli nyeti kushindwa kuendelea.

Upepo huu usivume bure bali ulete matokeo chana katika maisha ya Kila mtanzania.

2. UPATIKANAJI WA JUA LA KUTOSHA

Jua ni chanzo kikuu Cha nishati mbalimbali Kama tunavyoelezwa na wataalamu tofautitofauti. Na kwa sababu hiyo hatuna sababu ya msingi ya kuwa na umeme unaokata mara kwa mara.

Tunapaswa kufikiri Sana juu ya kuwa na Sola paneli za kutosha zenye uwezo mkubwa wa kuvuna mionzi ya jua ya kutosha ili kuzalisha umeme na kusambaza Kila Kona ya nchi. Beteri zenye uwezo wa hali ya juu ziwepo Kila mahali ili kuondoa tatizo la umeme Tanzania.

Kwa nini nchi yetu ihangaike wakati Mungu kaibariki kiasi hiki?. Huu ni wakati wakutumia nishati ya jua kuzalisha umeme katika nchi yetu.

3. UPATIKANAJI WA MAPOROMOKO YA MAJI KATIKA NCHI

Maporomoko ya maji yanayopatikana nchini ni mengi, na hivyo ni kwa ajili ya Kila mtanzania ili anufaike. Katika maporomoko ya maji tunaweza kuwa na nishati ya umeme isiyokatika kwa urahisi. Hivyo jenereta zikiwekwa Kila sehemu zenye maporomoko ya maji.

Hakuna haja ya kuwa na umeme wa mgao katika nchi ya Tanzania kwa sababu ya upatikanaji ya maporomoko hayo.

4. UPATIKANAJI WA VINYESI VYA WANYAMA NA MABAKI YA VIUMBE HAI
Vinyesi vya wanyama na mabaki ya viumbe hai huchakatwa na kubadilishwa kuwa "bayogesi" na bayogesi hutumika Kama chanzo Cha nishati ya umeme.

Hebu jiulize wewe mwenyewe elimu tuliyoipata darasani inatusaidia nini ikiwa hata hili nalo hatuwezi?. Huu ndio wakati wa kugeuza mitazamo yetu juu ya uzalishaji wa umeme Tanzania.

HITIMISHO
Nchi yetu ya Tanzania ni nchi yenye baraka za kutosha zenye mchango mkubwa juu ya uvunaji na uzalishaji wa umeme Kila mahali. Hivyo kuwa na maeneo ambayo hayana nishati ya umeme ni aibu kubwa mno.

Hakika yake ni kwamba wale waliosoma makala hii nia zao, mitazamo yao na fikra zao zitakuwa na uelewa wa hali ya juu. Na Tanzania yetu wataibadilisha na kuwa Kama paradiso ndogo wa si Kama ulaya maana ulaya bado ni hadhi ya duniani tu.

Maarifa uliyopata humu usikae nayo yatumie katika kuleta maendeleo ya miundombinu ya nishati ya umeme.

Karibu katika makala zingine .
 
Back
Top Bottom