Tanzania ina demokrasia kuliko Uingereza na Norway

Tanzania viongozi hupatikana kidemokrasia kwa sanduku la kura lakini wafalme na malkia wa Uingereza na Norway huwa hawapigiwi kura pamoja na kuwa hutumia hela za walipa kodi katika shughuli zao.

Malkia na wafalme wa Uingereza na Norway ni ving`ang`anizi wa madaraka ni wao tu kutawala na familia zao.Yaani wanatawala nchi kiukoo.Hamna demokrasia kabisa.Waafrika huwa tunaambiwa kuwepo ukomo wa muda wa uongozi lakini kwao malkia wao na wafalme wao ruksa kuendelea hadi wafe na wakifa wakabidhi watoto wao LOOOO!!!

Kwa kipengele hiki Tanzania kidemokrasia imewazidi mbali Uingereza na Norway.Iko haja uingereza na norway kuja kujifunza demokrasia tanzania.

Nafuu iwe hivyo lakini Ufisadi wa kisenge kama huu tunaoukumbatia na serekali hii ya kijani, poor governance, corruption, serious violation of human rights, poor education, social services, economy and standard of living. Halafu anayeng'ang'ania madaraka ni nani kati ya Norway na ccm? Unanunua magari 700 kwa ajili tu ya kutishia watu ..au hayo huyaoni? Kama viongozi hawakumbatii hayo niliyoyataja apo juu....watawale tu hata maisha.
 
Kwani Queen Elizabeth wa Uingereza ni kada wa chama gani?Labor Party au Conservative Party?na akagombee dhidi ya Queen/King wa chama gani?Mmh...hizi hoja zenu nyingine utafikiri za watoto wa primary school,si hoja ya kutolewa na msomi wa ngazi ya chuo.

Uingereza kuna wagombea binafsi wasio na vyama au unafikiri na Uingereza ni kama Tanzania mtu lazima uwe na chama kugombea?

Umalkia na ufalme waweza kugombaniwa na wagombea binafsi wasio na vyama.Cha msingi mtu asiitwe tu mfalme au malkia kwa kuzaliwa tu apimwe kwa uwezo na kwenye sanduku la kura.Hapo ndipo itakuwa demokrasia .
 
Halafu anayeng'ang'ania madaraka ni nani kati ya Norway na ccm?

Mfalme wa Norway ndiye anang`ang`ania madaraka maana hajawahi pigiwa kura iwe halali au feki hata siku moja.CCM wameingia kwenye kura mara ngapi?Futa usemi wako na iombe CCM msamaha.
 
Fangasi za ubongo mbaya sana . we mtoa Mada ebu omba mods watoe hizi taka mwili zako
 
Nitajie kabila moja tu la hapa Tanzania ambalo chief wake anachaguliwa kwa njia ya kura.Na hawa machief walikuwepo kabla hata ya ujio wa Wakoloni,sawa tu na Ma_king na Ma_Queen ambao walikuwepo ulaya tangu enzi hizo.
Uingereza kuna wagombea binafsi wasio na vyama au unafikiri na Uingereza ni kama Tanzania mtu lazima uwe na chama kugombea?

Umalkia na ufalme waweza kugombaniwa na wagombea binafsi wasio na vyama.Cha msingi mtu asiitwe tu mfalme au malkia kwa kuzaliwa tu apimwe kwa uwezo na kwenye sanduku la kura.Hapo ndipo itakuwa demokrasia .
 
Nitajie kabila moja tu la hapa Tanzania ambalo chief wake anachaguliwa kwa njia ya kura.

Chifu wa kitanzania sio kiongozi wa serikali usilinganishe na malkia wa uingereza na mfalme wa NOrway.Wale ni viongozi wa serikali.Malkia ni head of state NA mfalme wa Norway katika kazi zake pia ni amiri jeshi wa majeshi yote ya ulinzi.Mtu anayefanya kazi za serikali za juu kama hizo kidemokrasia lazima achaguliwe.Machifu wetu ni viongozi wa mila za matambiko na mambo mengine ya kiswahili swahili tu na kishirikina ampigie kura nani kwenye ofisi hiyo ya kishirikina?

Mimi naongelea viongozi ambao ni wakuu wa nchi zao wanaofanya kazi za kiserikali kama malkia wa uingereza na mfalme wa Norway
 
Tanzania viongozi hupatikana kidemokrasia kwa sanduku la kura lakini wafalme na malkia wa Uingereza na Norway huwa hawapigiwi kura pamoja na kuwa hutumia hela za walipa kodi katika shughuli zao.

Malkia na wafalme wa Uingereza na Norway ni ving`ang`anizi wa madaraka ni wao tu kutawala na familia zao.Yaani wanatawala nchi kiukoo.Hamna demokrasia kabisa.Waafrika huwa tunaambiwa kuwepo ukomo wa muda wa uongozi lakini kwao malkia wao na wafalme wao ruksa kuendelea hadi wafe na wakifa wakabidhi watoto wao LOOOO!!!

Kwa kipengele hiki Tanzania kidemokrasia imewazidi mbali Uingereza na Norway.Iko haja uingereza na norway kuja kujifunza demokrasia tanzania.
Sawa Muungwana Hongera zetu nyingi, napia umesahau sifa zetu nyingine kuwazidi wao, sisi pia viongozi wetu hawa tuchagulii jamaa zao kuwa viongozi wa kuwarithi kama Wafalme kwa vikaratasi mifukoni,kwenye chaguzi zetu kura haziibiwi na wala hakuna rushwa,tume zetu za uchaguzi tuna chagua wenyewe wananchi, matokeo ya chaguzi zetu mshindi ni mshindwa na mshindwa ni mshindi ili mradi katiba yetu ndivyo inavyo taka hadi raha,nani aseme nini kwa Domokrasi yetu tukuka.
 
Pia mbali na demokrasia Tanzania ina rasilimali nyingi za asili kuzizidi nchi hizi kwa mbali sana.
Tusichojiuliza na kukitafakari ni kwa nini nchi hizi zinatuzidi kimaendeleo. Tukijiuliza hili basi zile kelele za wale wabunge wanaoshinda bungeni kuhakikisha rais haojiwi na yeyote badala ya wao kuhoji changamoto za waliowachagua majimboni mwao zitapungua kama sio kuisha!
 
Zetu zipi? kwa sasa hatuna zetu, zetu tuliziacha miaka zaidi ya 100 iliyopita.
Huo mfumo wao wanauita Demokrasia na wanataka usiguswe, kwanini wajivute katika kufuatilia ya kwetu? Kama wao wanataka Mugabe au Museveni watoke, wangeanza kwa kuwaondoa Wafalme na Malikia wanaowatawala kwa vizazi na vizazi. Upo?
 
Yaani acha tu mfano malikia wa uingereza huu ni mwaka wa 64 toka awe malkia akiwa head of state wa Uingereza.Mugabe ana miaka 36 tu toka aanze kutawala Zimbabwe wanampigia kelele ni uonevu.Wote ni wakuu wa nchi zao wa kwao hawamsemi wanamsema Mugabe wetu.Uonezi tu.
 
Ni vitu vigumu kuelewa na vyenye kuamsha udadisi.
 
Back
Top Bottom