Hakuna ugunduzi wa chopa unaoweza kufanywa ndani ya miezi miwili kama ilivyoandikwa. Tusijidanganye na theory tulizokariri madarasani, ukiacha ugunduzi wa wazungu, wengine wote kama Japan, China, Afrika Kusini nk wamekuwa wakijifunza na kumodify teknolojia ya wazungu.Mkuu ni kweli wamegundua Chopa????????? Nauliza tu
Nauliza, Chuo kinayo chopa ya mafunzo ili kujua/kujifunza walao katika hali halisi kwamba chopa ina vitu gani ndani na inafanyaje kazi? Adisai Msongole ni Mhasibu, ugunduzi ni kitu kinachotaka ubobezi, sasa huyu mhasibu alibobea lini kwenye teknolojia ya kutengeneza chopa na kugundua aina mpya ya chopa, au ugunduzi huu ni wa aina gani?
Tuchukulie kwamba ni kweli, chuo kitafanya mass production ya chopa hiyo au tunafanya just for funny?. Ikiwa inafanywa for the sake of humor, ni nini uhalali wa rasilimali zote zitakazokuwa zimetumika?
Wasomi, wanasayansi na wanateknolojia huwa wanahangaika na ugunduzi wa vitu vitakavyotatua matatizo yanayoikabili jamii inayowazunguka. Hivi, tatizo linaloikabili jamii ya watanzania katika kuendesha maisha yao ya kila siku ni kukosekana kwa usafiri wa chopa? .....