Tanzania haitambui ushindi wa Mugabe - Membe


JMushi unaona unavyotukorogea habari kwa nini usibaki kwenye hoja ya mjadala?


Haya ya kwako yapeleke yanakohusika, nafikiri umesoma heading ya post hapa ni nini au unataka watu turudie tena??????
 

Wewe Unayesema Au Vs Wanachama Leta Matokeo Ya Kura Huko Au Kama Yapo Ili Tujuwe Ni Kina Nani Walisema Mugabe Hatambuliwi Na Afrika!
 
Membe kaongea muda mfupi uliopita kuwa suala la Zimbabwe AU walipeleka SADC na hajasema kuwa AU hawaitambui srikali ya Mugabe

Tanzania Broadcasting Corp. kwenye taarifa ya habari ya saa mbili leo (saa saba mchana ya Mashariki ya Marekani) wametangaza kwamba Membe kasema African Union haimtambui Mugabe.

Sasa jamani kama hawajui tofauti ya Tanzania na African Union hii inazidi kudhihirisha ninachokisema kila siku: Tanzania hakuna press!
 
Yale yale ya kupewa mashinikizo kutoka Washington DC na Downing street.

Hivi ni lini sisi waafrika tutafanya maamuzi yetu bila ya kupewa mashinikizo kutoka UK au Marekani au EU???

Kama kweli wanasimamia haki na usawa mbona hawakuzipinga au kutozitambua chaguzi hizi??

Yaani wanataka kutuambia nini kuhusu chaguzi hizi?
-Uchaguzi uliofanyika uganda?
-Uchaguzi uliofanyika pemba?
-Uchaguzi uliofanyika Kenya?
_Uchaguzi uliofanyika Egypt?
-Uchanguzi uliofanyika Rwanda?

Kwao zote hizi ni fair and democratic!! ni Zimbabwe tu ndiyo ulikuwa na violence.Mambo ya Kiza Besigye kuwekwa ndani hawakuyasikia hata kidogo!

Hebu waafrika acheni mambo hayo ya kufuata mkumbo, jengeni tabia ya kupigania haki bila ya kupewa mashinikizo au kufuata propaganda za magharibi.

-Wembemkali
 

Okay, hivi ni wapi mimi Nyani Ngabu niliposema kuwa ni "JF mtandao"? Si umesevu kwenye word....bandika basi hizo nukuu mjomba, mbona kila siku unanipiga chenga ya mwili?
 
JMushi unaona unavyotukorogea habari kwa nini usibaki kwenye hoja ya mjadala?



Haya ya kwako yapeleke yanakohusika, nafikiri umesoma heading ya post hapa ni nini au unataka watu turudie tena??????

Nani anataka kukoroga nini?
Vita ya Zimbabwe...Nani alikuwa anataka tumpe sapoti TSIVANGIRAI?
Nani alimpigia kifua kikwete awe msuluhishi wa pale KENYA?
Kofi Annan hakutosha?
Nani aliyemtuma Kikwete apige drums za vita dhidi ya MUGABE kama si BUSH NA MWINGEREZA?
 
Mkuu samahanini nimepata news vibaya.......ni sawa kabisa
 
Mushi, hakuna anaejua hicho kitu hapa, inaonekana.

Kuna mataifa yaliyokuwa na misimamo yao!
Namibia ni sapota wa Mugabe,so as SA.
Zambia chini ya Mwanawasa(Mungu amlaze pema) Ni sapota wa TSIVANGIRAI..The list goes on and on..So kama mataifa hayo yakichagua mabwana kama MKJJ anavyotaka yafanye...Then hakuna vita?
 

Sio TANZANIA HAKUNA PRESS...TANZANIA HAKUNA VIONGOZI!
NINASHANGAZWA SANA NA MKJJ ETI SASA MEMBE ANA AKILI TIMAMU?
TUSUBIRI MAANA UTASEMA THE SAME KWA MKULLO!
KWAMBA SASA KAMA TUMKIMSIKILIZA BERNARD MEMBE..KWANINI TUSIFANYE HIVYO KWA MUSTAFA MKULLO?
 
Angalia makala yangu ya leo kwenye Tanzania Daima. Bernard Membe amesema kuwa Umoja wa Afrika hautambui Mugabe kama Rais wa Zimbabwe. Zaidi ya yote kwa niaba ya Mawaziri wa SADC amesema kuwa Au haiutambui uchaguzi uliofanyika huko Zimbabwe.

So at last they have delivered the messege from the Saints.It is undrestandable they had no choice, either with Mugabe or with them.While we see them as leaders, the fact is that they are just decoys!!.If there is anybody who dont know what a decoy is;a decoy is usually a person, device or event meant as a distraction to conceal what an individual or a group might be looking for.
Coming back to the subject as far as I undrestand the AU resolution passed did not mention anything about recognition nor rejection of the Zimbabwe election.
 
BBC wanatangaza katika internet bbcswahili.com Membe anasema OAU imekabidhi madaraka ya kushughulikia jambo la Zimbabwe officially kwa SADCC, Pia Membe anasisitiza kuwa ndio msimamo wa AU chini ya mwenyekiti JK. Iko kwenye dira ya dunia ya leo na bado unaweza isikiliza mda wowote leo, kesho watatoa waweke ya kesho.

Membe anasisitiza kuwa Marais walitaka aje waseme naye na kumwambia ukweli, kisha anajichanganya kuwa hata wasingemualika angeweza kuja tu, ila walifikiri kuwa ulikuwa ni mda muafaka wa kuongea naye ghafla. Pia Membe anasisitiza kuwa AU wasingeweza kumuzuia kuja kwa saabu mualiko unapotolewa unasema marais bila kuchagua nani aje na nani asije. kila anayejiona mjumbe basi anakuja.
 

On the highlight....HOWEVER...THE AU CHAIRMAN...ON BEHALF OF THE AFRIKAN PEOPLE...CONGRATULATED THE PEOPLE OF ZIMBABWE FOR THEIR DECISSION TO VOTE THE WAY THEY VOTED!
 

Mkuu kwenye highlight...NANI ANALIKOROGA?
Hata hivyo kila mwenye nia nzuri na pia msimamo wa AU ulikuwa ni Mbeki aachiwe kazi ya usuluhishi!
Sasa viongozi wetu mnafuata habari za mabwana zenu tu!
Hivi Mfaransa naye role yake ipi?
 
Sio TANZANIA HAKUNA PRESS...TANZANIA HAKUNA VIONGOZI! ?

Utanambiaje Tanzania kuna press wakati hawajatangaza mpaka leo kwamba Harare wamemuita balozi wao nyumbani na wamemsikia Mbunge anatamka hicho kitu Bungeni?

Utanambiaje Tanzania kuna press wakati hawajui tofauti ya Tanzania kutokumtambua Mugabe na African Union kutokumtambua Mugabe?

Utanambiaje Tanzania kuna press wakati maswali yote ya Msimamo wa Africa na Tanzania kuhusu Zimbabwe anaulizwa Membe akiwa nje ya nchi, au anaulizwa Zitto (Mh.) hapa JF?

Umewahi kusikia mwandishi wa Kibongo anambana Kikwete atoe msimamo wake kuhusu Zimbabwe? Thubutu, waoga ile mbaya.

Umeona ile video clip Mwanakijiji aliyoweka ya mwandishi huko Egypt anambana Mugabe mbavu mpaka ma bodi gadi wa Mugabe wanamlegeza mwandishi, mpaka Mugabe anamtukana Mwandishi?

That's what you call the press! Tanzania tutoe wapi press Mushi wewe?
 
I'm totally comfused, if this is the way we are tackling serious issue such as Zimbabwe.
 

Mkuu PRESS INAZITOA HABARI KUTOKA SERIKALINI..NA WAO WANARIPOTI!
KUNA WALIOHONGWA TAYARI NA WAO WANAFANYA KAZI KISIASA!
Na kuhusu hiyo ya Mugabe..Haihusiani na PRESS TU...Ni maslahi!
Huyo mwandishi alitumwa na waingereza!
Na ndio maana MUGABE AKAWA ANA TAUNT..KUWA WE ARE NOT A BRITISH COLON!
Huku wa Egypt wakichombeza kwa pembeni kwa kumpa HONGERA.
Kikwete naye aliupongeza uamuzi wa wananchi kumchagua MUGABE!
Kuna PRESS KIBAO..WE KUTUMIA AKILI YAKO NA KUCHUJA HABARI!
HAPO NDIO UTAWEZA KUUJUA UKWELI...Lakini ukibugia mihabari tuu!
Tab tupu!
 
Mkuu PRESS INAZITOA HABARI KUTOKA SERIKALINI..NA WAO WANARIPOTI!
KUNA WALIOHONGWA TAYARI NA WAO WANAFANYA KAZI KISIASA!

Sasa ishu za Mugabe na Zimbabwe, nani amuhonge yupi kwa manufaa ya nani na siasa zipi?

Ni incompetence tu. Hawajui fani yao wale watu.

Harare imemwita balozi nyumbani hawaandiki? Hao watu wameenda shule ya Uandishi kweli? Au wanashindwa kuumuliza Mbunge hizo habari umezisikia wapi, mpaka anakuja kuulizwa hapa JF? Kuna press hapo kweli? Please Mushi, be objective for a second.
 

Kuhani fuatilia haya mambo vizuri!
Habari hata za kifo cha Mwanawasa zilitolewa tofauti na MWINGEREZA,MCHINA NA HATA MFARANSA MWENYEWE AMBAYE NDIYE ANASHIKILIA UENYEKITI WA EU!
Huyo mwandishi aliyemfuata Mugabe alitaka ile issue ya yeye kukwidwa na walinzi wake imchafue ili kuonyesha kuwa ni mtu asiyependa hata uhuru wa press!
Uhuru wa press umekuwa UHURU WA MAFISADI!
 
Kuhani... you have no idea.. ndio maana tunaomba support ya watu kama nyinyi kwani mnatuwezesha sisi wengine kufanya yale ambayo hayawezi kufanyika nyumbani. Binafsi hakuna siku nzuri kama ya kupata habari kwa uhakika kama leo. But then.. one man can't do it all! Kuhani, kwa vile inaonekana una uwezo sana kwenye mambo haya naomba tushirikiane, utakuwa mmojawapo wa correspondent wetu na nitakupa contacts kwa niaba ya KLHN na jinsi ya kurekodi n.k halafu uwasiliane nao ili ufanye kile ambacho wengi tunashindwa kufanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…