Tanesco muwe na line zenu za simu kwa ajili ya LUKU. Mitandao inatutesa

instagram

JF-Expert Member
May 27, 2014
2,108
4,814
Hali ni mbaya sana sasa hivi kwa mitandao ya simu kuhusu swala la kununua umeme kupitia simi za viganjani.
Imagine unanunua umeme kupitia twigoopesa unakaa masaa matatu hakuna token na giza linaingia ukipiga simuzao zinakatwa hakuna majibu.

Kwanini nyie Tanesco msiwe na line zenu za simcard mkatusajilia sisi wateja alafu mkasambaza kwa ma agent wote wa lukupesa nchi nzima ili mteja akiwa na line yake ya lukupesa ana mpa agent elfu10 kwa namba yake ya line Kisha agent ana muwekea hela mteja kwenye line yake kisha mteja anaweka line yake ya LUKUpesa kwenye simu yake then anaingia menu ya LUKUpesa ananunua umeme wake au anamnunulia mzazi wake umeme kupititia line yake ya lukupesa kwa kuweka mita namba then umeme unaenda direct kwenye luku bila kuingiza token.

Kwanini mnatupa wateja wenu mlolongo mrefu wa kununua umeme kupitia server za mitandao mingine ya simu wakata nyie pia mnaweza kuwa na mtandao wenu huu huu wa luku kuliko kuvukavuka maboda kupitia ma server ya mitandao mingine ambayo saa zingine server zao zinakuwa na shida. Na pia kuna makato.

Hebu fanyeni makakati mtuletee line za simcard zenye options mbili tu za kuweka hela na kununua umeme kwenda mita namba na kucheki salio na kuwasiliana na huduma kwa wateja tu basi mtatusaidia sana
 
Aisee umewaza kiboya sana. Hilo haliwezi kutokea kwa sababu TANESCO biashara yao ni kuzalisha na kisambaza umeme full stop. Hizi tigo pesha ni channel tu za malipo na kuna channel nyingi hujalazimishwa kutumia Tigo. Pia wakati mwingine umeme kuchelewa huwa ni matatizo ya TANESCO yenyewe na si Matatizo ya Tigo au channel husika.

Unachotakiwa kufanya.
1. Usisubiri hadi umeme uishe kabisa. Kadiria kwa mfano umeme wa 5000 unatumia siku 7 ikifika siku ya 6 nunua umeme na uweke mapema kabla haujaisha.
2. Kama channel uliyotumie ni Tigo pesa imezingua nenda kwa kwa kibanda ununue umeme hata wa buku jero kupitia channel nyingine kama selcom wakati unasubiri. Au kama una line nyingine ya voda tumia nunua umeme kidogo wakati unasubiri.
 
Wewe unajua maisha ya mtanzania kweli? Unazani hali ya uchumi ni nzuri kiasi hicho mtu kupanga umeme utaisha mda gani atakuwa na hela kiasi gani yani mtu anunue umeme kupitia kila channel asitegemee channel moja sijui unaishi ndoto za wapi.

Eti leseni ya kusambaza umeme, kwaiyo hawaruhusiwi wao kuuza umeme? Zamani alikuwa anauza nani umeme kabla ya hao twigoo? Kwani wao wakiwa na simcard zao za kufanyia malipo ya umeme watakuwa wamekiuka masharti gani? Halafu tenesco ni shirika la serikali ujue hakuna leseni wanakosa
 
Wewe unajua maisha ya mtanzania kweli? Unazani hali ya uchumi ni nzuri kiasi hicho mtu kupanga umeme utaisha mda gani atakuwa na hela kiasi gani yani mtu anunue umeme kupitia kila channel asitegemee channel moja sijui unaishi ndoto za wapi
Kama huwezi si ukae kimya usubirie huo umeme uje? Kuliko kushauri vitu ambavyo haviko duniani?

Yaani Tanesco wajenge minara ya simu nchi nzima ili kuwezesha ununuzi wa luku tu? Hizo gharama unajua bei yake?
 
Kama huwezi si ukae kimya usubirie huo umeme uje? Kuliko kushauri vitu ambavyo haviko duniani?
Haviko duniani kwani kila kitu ulizaliwa nacho tumboni kwa mamaako si watu wenye akili wanavitengeneza unavitumia kaa kimya kama mawazo yako ni mafupi
 
Haviko duniani kwani kila kitu ulizaliwa nacho tumboni kwa mamaako si watu wenye akili wanavitengeneza unavitumia kaa kimya kama mawazo yako ni mafupi
Watu wana buni vitu ambavyo vinapunguza gharama na kurahisisha maisha. Siyo wazo kama lako la kuongeza gharama na ku complicate maisha. Hivi kwanza nani anataka kila akitaka kununua umeme abadilishe line kwenye simu.
 
Kama kweli wewe ni wa kuweza kununuanunua umeme kwenye kila channel unashindwa kumiliki kisimu cha kitochi maalumu chenye logo ya Tanesco maalumu kwa kulipia umeme tu ambacho hakigharimu zaidi ya elfu 25 ambacho pia ni mbadala wa kimashine cha luku hata kimashine chako cha luku kikikiwa hakina betri usiku umeme umeisha una kitochi chako kinakaa na chaji miezi miwili kweli bado akili yako haioni umuhimu wa kuwa na line maalumu ya lukupesa kweli?
 
Back
Top Bottom