Tamko la UVCCM mkoa wa Arusha kuhusu Lowassa

Lowassa tuliza domo lako hilo. Huna jipya. CCM ni imara uzee wako umekuwa wenye laana. Umezeeka vibaya sana.
 
TAMKO KUTOKA UVCCM MKOA WA ARUSHA.

Umoja wa vijana wa chama cha Mapinduzi mkoa wa Arusha umeshtushwa nakufadhaishwa na kauli ya aliyekua mgombea wa urais kwa tiketi ya Ukawa Ndg Edward Lowasa kwamba Chama Cha Mapinduzi ni cha msimu na kwamba kimejaribu kununua madiwani wa upinzani kwa Tsh million 20.
Kama Umoja wa Vijana tulidhani Ndg Lowasa aliposhindwa kwenye uchaguzi mkuu angetekeleza ahadi yake kwa vitendo ya kwenda kuchunga mifugo yake na kuacha kuendeleza maigizo aliyoyaanzisha ya kuendelea kuwalaghai na kuwachonganisha chama cha Mapinduzi na wananchi wake ambao nao
wameshazielewa hila zake.
Ndg Lowasa anasema CCM ni ya wezi n wanyanganyi na kwamba watanzania wote wanajua yeye ndiye mshindi wa uchaguzi mkuu. Tunamshukuru sana kutukumbusha alivyoasisi genge la kidhalimu ndani ya CCM, tunakiri kwamba chama hiki ni kweli kilikua kiwe cha msimu na kisingeaminika kabisa, hii ni kutokana na uwepo wake na kikundi hicho kilichodhamiri kugeuza taifa hili kuwa pango la walanguzi.

Ambacho Ndg Lowasa amesahau kuwaambia wananchi wa monduli ni kwamba alishapiga dili na walanguzi wenzake kuondoka ndani ya Chama hiki tukufu July mwaka jana, na kwamba wachache waliobaki tutaendelea kuwasafisha na kuwatupa kwenye dampo letu linaloitwa Ukawa ili kurejesha utakatifu wa Cham hiki.

Ndg Lowasa Umoja wa Vijana wa Arusha unakutaka urudi kijiji cha Ngarash mara moja ukachunge mifugo yako umuache mteule wa Mungu aliyepewa dhamana na watanzania wote kutufikisha katika nchi ya neema Mhe.John Pombe Magufuli aendelee kufanya vitu vyake.

Ni heshima mbele za Mungu kumpa mtu anachostahili, na kwa Ndg Lowasa alifanikiwa kupasua CCM lakini Mungu akawa upande wetu, aligawa vijana Mungu pia akasimama na alijaribu kuaminisha watanzania kuwa pesa ndio kila kitu jambo ambalo ameshuhudia aliposhindwa na kama kuna jambo anastahili nalo pongezi ni hiyo hulka ya kuwagawa watanzania.

UVCCM mkoa wa Arusha inawaaminisha na tunasema kam Ndg Lowasa ataendelea na harakati zake za kuikejeli serikali hii hatutamvumilia kamwe.
Imetolewa na Umoja Wa Vijana CCM mkoa wa Arusha....... Imetolewa na COMRED MUNISI MWKT UVCCM MKOA
UVCCM ARUSHA WAMEISHIWA PUMZI
 
halafu kesho yakiwa geuka kama wale waliotoa tamko kumsapoti kitwanga cha ulevi,sijui sura zenu mtaziweka wapi?
ni rahis tu, watageuza maneno!! kama CHADEMA walimweka lowasa kwenye list of shame na sasa ivi wanamsafisha itakuwa hilo tamko tuu!
 
Teh,teh uvccm arusha,mbona ccm ilishafutwa arusha?huyu munisi si ndo yule mchumia tumbo anayeshirikiana na jambazi maarufu anayefahamika kwa jina la mjusi anayejificha chini ya kivuli cha uvccm amemaliza roho za wahindi arusha
Mkuu kumbe unamfahamu j4 mjusi.kunawatu wanaishi nyumba za vioo halafu wanaanza vita vya mawe.
 
Teh,teh uvccm arusha,mbona ccm ilishafutwa arusha?huyu munisi si ndo yule mchumia tumbo anayeshirikiana na jambazi maarufu anayefahamika kwa jina la mjusi anayejificha chini ya kivuli cha uvccm amemaliza roho za wahindi arusha
Jambazi maarufu anajulikana sana na hata wewe unamjua, bali unona aibu kumtaja.
 
Nasikia huko Arusha hakuna upinzani wowote kwenye chaguzi za ndani. Watu hupeana tu vyeo kwa sababu ya uchache wa wanachama. Nasikia wanachama wa CCM hapo Arusha Mjini hamzidi 20, sasa haya matamko ya kazi gani?
Familia yangu peke yake ni zaidi ya watu hamsini na sote ni wanachama wa CCM. Ni kweli chadema inaongoza Arusha kwa Sasa, Lakini CCM bado ipo, na inarudisha hadhi yake Arusha.
 
Kuelekea uchaguzi 2015 Mbowe alitumia mamilioni kutoa mafunzo kwa makundi ya vijana ,na baadae kuutangazia uma kuwa ,CHADEMAhaitaibiwa kura tena. .Cha ajabu baada ya uchaguzi Mbowe na BAVICHA wote wakaimba wimbo uleule Wa kuibiwa kura!!!

Sasa kwa nini Mbowe alitumia hela za chama kutoa mafunzo kwa vijana???
 
Familia yangu peke yake ni zaidi ya watu hamsini na sote ni wanachama wa CCM. Ni kweli chadema inaongoza Arusha kwa Sasa, Lakini CCM bado ipo, na inarudisha hadhi yake Arusha.

utakuwa umebaki ww na mkeo,na yule mzee wa longido aliyeshindwa ubunge longido miguu inamenyeka kama nyoka,miaka yake yote ya ubunge wake ameshindwa kununuwa viatu anashindia sendoz kuanzia masika hadi kiangazi
 
Huyu Munisi kuna siku tutchoma moto ni kibaka maarufu hapa Arusha...pamoja na Jumanne mjusi ...namfikishia taarifa ache kuwa kibaka ...kila siku ana kwapua pochi za kina mama na anajificha kwenye CCM.....
 
nampata sana,huyu ni jambazi sugu nakumbuka kesi ya mwisho alikutwa huko arusha ndani kwa mhindi sijui ile kesi iliishia wap
Huyu Munisi ni mpiga roba maarufu ...maeneo ya Ungalimited kunasiku tulimkimbiza ,tukamkamata akapelekwa polis ,sijui alitokaje ......naona ndiye msemaji wa chama duh...kaz ipo
 
Familia yangu peke yake ni zaidi ya watu hamsini na sote ni wanachama wa CCM. Ni kweli chadema inaongoza Arusha kwa Sasa, Lakini CCM bado ipo, na inarudisha hadhi yake Arusha.
Umenifanya ni cheke sana mm....Arusha ipi hiyo ,hadhi ya CCM inapungua kila uchwao.....hapa .....diwani mmoja tu...haya msalimie yule aliyekuwa mayor wa kichina Lymo
 
Back
Top Bottom