TAKUKURU yaanika mali za Sh. Bilioni 3.5 za aliyekuwa mhasibu wake Godfrey Gugai

Acha porojo kijana! Kama hujui history za watu kaa kimya! Mengi hajawahi shona viatu,huyo lugumi hajawahi shona viatu, ni janja janja zao tu,ndo maana lugumi kwa sasa anafilisiwa,Mali zake nyingi zimekanatwa
Hahahahah your living in darkness my brother, open your mind, unasoma sana magazeti na kufatilia matamshi ya viongozi ila hujui reality, kaa tu ukiamini unachokiamini ila ukweli hubaki kuwa ukweli. Siku ukipewa mrejesho na hao waliotangaza kukamata mali za Lugumi ni tag na mimi.
 
HATIMAYE Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imeanika mali za aliyekuwa Mhasibu Mkuu wake, Godfrey Gugai, ambaye utajiri wake unakadiriwa kuwa wa thamani ya Sh. bilioni 3.5.

Miongoni mwa mali zinazomweka mhasibu huyo katika kundi la matajiri katika nchi hii inayotambuliwa kimataifa kama mojawapo ya mataifa maskini, ni pamoja na viwanja 37, maghorofa saba, nyumba za kawaida tisa, magari matano na pikipiki.

Maghorofa, nyumba za kawaida na viwanja vya mhasibu huyo ambaye alishafukuzwa kazi tangu mwaka jana viko kwa mtawanyiko katika maeneo mbalimbali nchini yakiwamo ya ghali karibu na bahari, Kigamboni na Mbweni jijini Dar es Salaam na pia Bagamoyo mkoani Pwani. Kwingineko kuliko na mali hizo ni Kinondoni (Dar), Musoma, Nyegezi na Kiseke jijini Mwanza.

Hata hivyo, chanzo cha uhakika kimeiambia Nipashe kuwa hivi sasa mali hizo ziko chini ya himaya ya Takukuru, baada ya kuzinasa kufuatia idhini ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyotokana na ombi la taasisi hiyo.

Mei 9, mwaka huu, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilitoa amri ya zuio la mali za Gugai ambaye anakabiliwa na tuhuma za kujilimbikizia mali kinyume cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya mwaka 2007.

Amri ya zuio la mali za Gugai ilitolewa na Mahakama hiyo kutokana na ombi la Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) chini ya kifungu namba 38(1)(a) na (b) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya mwaka 2007 katika shauri namba 13 la 2017.

Mali hizo ni nyumba saba za ghorofa moja moja zilizopo maeneo ya Wilaya ya Kikondoni jijini Dar es Salaam, nyumba nane, viwanja 37, magari matano na pikipiki moja.

Katika orodha ya mali hizo zinazoshikiliwa na Takukuru, na ambayo Nipashe imeona nakala yake, inaonyesha kuwa mali za mhasibu huyo wa zamani zilizowekewa zuio la Mahakama ni nyumba nne za ghorofa moja moja zilizoko kiwanja na 64 kitalu Ununio, Kinondoni, Nyumba tatu za ghorofa moja zilizoko kiwanja na 150 kitalu 8 Bunju na Kinondoni, nyumba nne zilizoko Kiwanja na 225 Kitalu 6, Mbweni JKT, Kinondoni.

Nyingine ni nyumba zilizoko kwenye kiwanja namba 62 na 63 kitalu C, Kinondoni, nyumba iliyoko kiwanja namba 29 kitalu L, Majita, Musoma, nyumba namba 713 PPF Kiseke, Mwanza na nyumba iliyoko kwenye kiwaja namba 438 bloku D, Nyegezi, Mwanza.

VIWANJA 37

Katika orodha ya viwanja ni pamoja na kiwanja namba 14 kitalu J, Bunju, Kinondoni, Kiwanja namba 47 kitalu B, Mwongozo, Kigamboni, kiwanja namba 184 kitalu B, Buyuni,Temeke, kiwanja namba 103 Kitalu L, Kaole, Bagamoyo, kiwanja namba 104 Kitalu L, Kaole, Bagamoyo na kiwanja namba 209 kitalu B, Kibaha.

Vingine ni kiwanja namba 195 kitalu 3, Kihonda, Morogoro, kiwanja namba 993 kitalu L, Kiegeya, Morogoro, kiwanja namba 868 Kitalu Q, Lukobe, Morogoro, kiwanja namba 34 kitalu K, Kisasa B, Dodoma, kiwanja namba 32 kitalu N, Itega, Dodoma, kiwanja namba 39 Kitalu M, Itega, Dodoma, kiwanja namba 24 kitalu B, Chidachi, Dodoma, kiwanja namba 64 Nzuguni, Dodoma, kiwanja namba 230 Kitalu B, Nyegezi, Mwanza na kiwanja namba 439 Kitalu D, Nyegezi, Mwanza.

Viwanja vingine ni kiwanja namba 275 Kitalu 2, Nyamhongolo, Mwanza, kiwanja namba 277 kitalu 2 Nyamhongolo, Mwanza, kiwanja namba 296 kitalu 2, Nyamhongolo, Mwanza, kiwanja namba 297 kitalu 2, Nyamhongolo, Mwanza, kiwanja namba 286 kitalu G, Nyamagana, Mwanza, kiwanja namba 287 kitalu G, Nyamagana, Mwanza, kiwanja namba 90 kitalu 5, Bugarika, Mwanza, kiwanja namba 126 kitalu A, Makoko, Musoma, kiwanja namba 622 kitalu A, Gomba , Arusha, kiwanja namba 621 na 623, kitalu A, Gomba na Arusha, kiwanja namba 737 kitalu C, Mwambani, Tanga

Kiwanja namba 1,2 na 3 kitalu J, Mwambani,Tanga, kiwanja namba 4 kitalu J Mwambani, Tanga, kiwanja namba 5 kitalu J, Mwambani Tanga, kiwanja namba 18 kitalu J, Mwambani Tanga, kiwanja namba 7,9 kitalu J, Mwakidila, Tanga na kiwanja namba 11, 13 kitalu J, Mwakidila, Tanga

ORODHA YA MAGARI

Orodha ya magari ya mhasibu huyo wa zamani Takukuru inahusisha magari matano ambayo ni gari namba T 180 DBQ , Mitsubish Canter; gari namba T 581 BQU, Toyota Hillux; gari namba T 814 CSC Nissan Murrano; gari namba T 679 ASD Toyota RAV 4 na gari namba T 913 DHE Suzuki. Pia inashikiliwa pikipiki yenye namba zz usajili MC 837BCL

Kutokana na maombi ya DPP mahakama imeamuru mali zilizotajwa za Gugai ziwe chini ya zuio la Mahakama.

Pia mawakala wake na watu wengine wote wanaomwakilisha wamezuiwa kuuza au kuhamisha umiliki au kuweka dhamana mali zote zilizowekewa zuio.

Aidha, Msajili wa hati ameagizwa kusajili zuio hilo kama kizuizi dhidi ya mali zote zilizotajwa.

Pia Msajili Msaidizi wa magari ameagizwa asiruhusu uhamishaji wa umiliki wa vyombo vya moto vilivyowekewa zuio mpaka mahakama itakapoelekeza vinginevyo.

View attachment 510928


Tanzania ya Kikwete. Nyumba nyingi kwenye maeneo haya zikichunguzwa kwa makini, zimejengwa na pesa za wananchi. Bei za nyumba zilipanda juu, mteja alikuwa ni serikali, pesa za kuwapa huduma watu zikiibiwa bila ya control. Haya HUYU ndiye. Muhasibu wa Kuzuwia Rushwa nchini, je alikuwa akifanya haya bila bosi wake kujuwa? Ndiyo maana hata Pamoja na upungufu wa Rais Magufuli, bado sijaona kuna mwingine anaweza kupambana na hawa wezi wachache waliokuwa wakiwadhurumu na kuitafuna Tanzania ya walio wengi. Wanaiba utafikili wataishi milele, kifo kwao hakitatokea. Kama kuna wezi wengine matumbo moto, waisome namba. Hata kama nyumba imeandikwa jina la jamaa, Tanzania ni rahisi sana kumchunguza mtu, wengi sisi. Ni masikini, mala Nina nyumba ya million 300, na sifanya kazi, ama kipato changu kidogo, nitaeleza nimeoata wapi za kujenga? Watanzania ni woga, kuhoji Mtanzania ni rahisi sana kama amebeba cha wizi atasema tu. Musema kweli mpenzi wa MUNGU
 
kweli aisee huyu alikuwa kauzu sana


Siyo peke yake, Tanzania ilikuwa na wizi wa ajabu, HUYU ni mmojawapo tu tena ni small fish. Kuna wezi waliokuwa wakisaidiwa na wahindi pesa zao ziko nje ya nchi. Na wako wengi wenye majumba na plots kama huyu. Ndiyo maana wengi Watanzani ni masikini wa kutupa. Lawama zote ni uongozi mbovu wa serikali zilizopita.
 
Hii nchi wapigaji ni wengi sana!

Uongozi chini ya Kikwete nchi ilitafunwa na kuwachwa mifupa mitupu. Sijui Kikwete uso anauweka wapi kwa haya na uongozi wake mbovu. Watu kama hawa waliwaibiwa Watanzania wenzao kama Hakuna serikali wala Rais
 
kwa sasa naweka orodha kidogo....ila ikibidi nitaweka orodha yake yote hadharani.

LONG FELLOWS GROUP

MBEZI BEACH, DAR ES SALAAM



Godfrey Gugai - Mjumbe
 
Mkuu punguza akili na mawazo ya kimasikini, kila kitu kinawezekana katika hii dunia as long as unapumua. Bhakheresa alikua muuza karanga wakati anaanza ujasiriamali, Mengi alikua mshona viatu tu, Lugumi alikua mshona viatu tu, juhudi zako na connection ulizonazo ndio zitakufanya ufanikiwe katika maisha.

Lugumi huwezi kuita hayo ni mafanikio, huo ni wizi na dhuruma ya watu unaowaibia. Kufanikiwa ni kufanya kazi na kuchuma kwa haki. Huu ndiyo upungufu wa Watanzania wengi, hatutofautishi kati ya wezi na wanaofanikiwa kwa kufanya kazi, wote tunawasifu.
 
wakuu huyu jamaa nasikia alikuwa ni mhasibu wa PCCB,kwa mwenye taarifa zake zaidi tunaomba atueleweshe kama hiyo orodha hapo chini ni kweli inamuhusu,hii nchi tumuache tu mheshimiwa atunyooshe,mtu mmoja utitiri wote huo wa mali and yet utakuta ana ndugu wamekosa msaada wa ada tu..waafrika aliyetulaani mungu anamuona hakika!View attachment 510944
Wacha tunyooshwe. Ndio maana mi nasema kuna watu mtandaoni hapa wanatetea mambo bila kujua wanatetea watu kama hawa! Sasa Serekali ilikuwepo, sheria zilikuwepo hata ufuatiliaji hapana si rahisi kupata mali zote hizo hata ukifanya biashara gani kwa muda mfupi aliokuwa kazini!
 
wakuu huyu jamaa nasikia alikuwa ni mhasibu wa PCCB,kwa mwenye taarifa zake zaidi tunaomba atueleweshe kama hiyo orodha hapo chini ni kweli inamuhusu,hii nchi tumuache tu mheshimiwa atunyooshe,mtu mmoja utitiri wote huo wa mali and yet utakuta ana ndugu wamekosa msaada wa ada tu..waafrika aliyetulaani mungu anamuona hakika!View attachment 510944
Wacha tunyooshwe. Ndio maana mi nasema kuna watu mtandaoni hapa wanatetea mambo bila kujua wanatetea watu kama hawa! Sasa Serekali ilikuwepo, sheria zilikuwepo hata ufuatiliaji hapana si rahisi kupata mali zote hizo hata ukifanya biashara gani kwa muda mfupi aliokuwa kazini!
 
Mjini hapa kuna watu walizipiga.. Hasa kama huyu ni CA je aliyekuwa boss wake atakuwa anamiliki mali na utajiri wa kiasi gani?
 
Back
Top Bottom