TAKUKURU mchunguzeni Mkuu wa Wilaya Morogoro, anaitumia ofisi yake vibaya

Napia atenguliwe wakati uchunguzi ukiendelea.
Viongozi wengi wanaiba pesa za umma/wananchi.
Wezi hawakubaliki katika namna yeyote ile.

Kwa kweli tuhuma hizi ni nzito na zinaleta taswira mbaya kwa Serikali, ikibidi kupisha uchunguzi itakuwa vizuri zaidi.
 
SIRI IMEFICHUKA! Kumbe vile vibanda vya wajasiriamali (wamachinga) katika Soko Kuu la Chifu Kingalu vilivyojengwa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Albert Msando kwa kushirikiana na benki fulani, vimegeuzwa mradi wa kupigia pesa na kuiibia serikali? Hatari sana.

Itakumbukwa kuwa DC Msando alisema anakatwa kiasi fulani cha mshahara wake kila mwezi kulipia deni la benki alilokopa ili kujenga vibanda vile, tena alisema anajitolea.

REJEA: Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Albert Msando anasema anakatwa rejesho la mkobo wa kujenga vibanda

Imekuwaje leo anadai alipwe na Halmashauri? Lengo lake lilikuwa ni kufanya biashara? Kuilaghai Serikali? Kusaka umaarufu wa kisiasa au kutapeli Wajasiriamali?

Tetesi zilianza kuenea kutoka kwa wajasiriamali wenyewe ambao walidai DC aliwaelekeza kulipia kati ya laki 5 mpaka laki 7 kila mwezi kwa kila kibanda, tena fedha hizo alitaka zilipwe kwenye akaunti yake binafsi. Tetesi hizo zikadaiwa ni uzushi.

Yakaibuka madai mengine kwamba baada ya kushindikana kuwalipisha machinga kiasi hicho kufuatia serikali ya mkoa kuelekeza wamachinga walipe tu bei elekezi kwa soko ili kuipatia halmashauri mapato, DC kuona amekwama akaagiza H/Manispaa imrudishie fedha zake takribani milioni 106 ili alipe deni la benki kwa sababu zilitumika kwenye mradi wa maendeleo, jambo ambalo lilipingwa pia kwa sababu sio utaratibu wa serikali mtu binafsi kukopa na kuja kudai bila kufuata sheria na kanuni. Madai hayo nayo akayakanusha kupitia vyombo vya habari na kudai Mkuu wa Mkoa na Mbunge wanakwamisha jitihada za serikali (yeye) kuwasaidia wamachinga.

REJEA: DC Alberto Msando akopa milioni106 benki ili kuwajengea wamachinga sehemu ya kufanyia biashara

Hivi sasa yapo madai mengine kwamba ameagiza alipwe jumla shilingi milioni 279, huku akitaja majina ya wazabuni wawili waliojenga vibanda hivyo, majina ambayo hayatambuliki na Halmashauri wala mchakato wa zabuni haukufanyika. Na madai haya atayakanusha?

Mbaya zaidi, inasemekana Mkurugenzi na watumishi wa Halmashauri wametishiwa kufukuzishwa kazi endapo hawataidhinisha malipo hayo batili. Kama ni kweli, lazima kuna vielelezo vya barua, wasiogope, waweke mambo wazi.

MY TAKE: Kwa sababu hili ni jambo lenye harufu ya rushwa, wizi na matumizi mabaya ya ofisi na fedha za umma; ipo haja ya TAKUKURU na vyombo vya dola kufika Morogoro na kulichunguza kwa undani.

Inaumiza kusikia watu wanataka kuibia Serikali kwa sababu tu wameaminiwa na kupewa dhamana. Watanzania wa leo sio wajinga kiasi hicho. HILI LISIACHWE LIPITE HIVI HIVI!
Moja yawez kubwa majungu kama majungu meengine., Pili Kama alikopa hizo fedha mkataba c ilikuwa halmashaur itamrudishia, Kwan Miradi mingapi ambayo halmashaur wanakopa na wanarudisha fedha hizo. Ukwel yeye alibeba dhamana kupitia mshahara wake Ili wamachinga wapate maeneo ya kufanya biashara.

Kulipwa ni Haki yake. Mlipeni achen Janja Janja ya kumchafua.
 
Ni muhimu TAKUKURU wachunguze madai yote kwa kina. Ni hatari sana mtumishi wa umma kutajwa tajwa kwenye mambo kama haya.

Majizi Yapo Ndugu Zangu Kitendo Cha Kutajwa Tu Mwenyekiti Wake Na Chongolo, Shaka Wangemweka Kando Ila Wanaye Tu, Ccm Imeoza Jamani

Moja yawez kubwa majungu kama majungu meengine., Pili Kama alikopa hizo fedha mkataba c ilikuwa halmashaur itamrudishia, Kwan Miradi mingapi ambayo halmashaur wanakopa na wanarudisha fedha hizo. Ukwel yeye alibeba dhamana kupitia mshahara wake Ili wamachinga wapate maeneo ya kufanya biashara.

Kulipwa ni Haki yake. Mlipeni achen Janja Janja ya kumchafua.

Hayo unayosema sio yake. Yeye alinukuliwa akisema anajitolea mshahara wa uDC na hatarajii malipo. Leo anakuja kudai kwa nguvu na vitisho juu ndio inatia mashaka. Na hajahukumiwa, nimewaomba TAKUKURU wachunguze, hilo lina ubaya gani?
 
Moja yawez kubwa majungu kama majungu meengine., Pili Kama alikopa hizo fedha mkataba c ilikuwa halmashaur itamrudishia, Kwan Miradi mingapi ambayo halmashaur wanakopa na wanarudisha fedha hizo. Ukwel yeye alibeba dhamana kupitia mshahara wake Ili wamachinga wapate maeneo ya kufanya biashara.

Kulipwa ni Haki yake. Mlipeni achen Janja Janja ya kumchafua.
Wewe itakuwa nii CHAWA wa Msando.
 
Msando mzee wa deal. Watu hawajui pesa anatoa wapi! Acheni wivu mwacheni DC apige kazi acheni majungu! Kama alitoa pesa zake kusaidia watu sasa akizidai kuna ubaya gani? kwani ye padri!! wamlipe tu.
 
SIRI IMEFICHUKA! Kumbe vile vibanda vya wajasiriamali (wamachinga) katika Soko Kuu la Chifu Kingalu vilivyojengwa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Albert Msando kwa kushirikiana na benki fulani, vimegeuzwa mradi wa kupigia pesa na kuiibia serikali? Hatari sana.

Itakumbukwa kuwa DC Msando alisema anakatwa kiasi fulani cha mshahara wake kila mwezi kulipia deni la benki alilokopa ili kujenga vibanda vile, tena alisema anajitolea.

REJEA: Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Albert Msando anasema anakatwa rejesho la mkobo wa kujenga vibanda

Imekuwaje leo anadai alipwe na Halmashauri? Lengo lake lilikuwa ni kufanya biashara? Kuilaghai Serikali? Kusaka umaarufu wa kisiasa au kutapeli Wajasiriamali?

Tetesi zilianza kuenea kutoka kwa wajasiriamali wenyewe ambao walidai DC aliwaelekeza kulipia kati ya laki 5 mpaka laki 7 kila mwezi kwa kila kibanda, tena fedha hizo alitaka zilipwe kwenye akaunti yake binafsi. Tetesi hizo zikadaiwa ni uzushi.

Yakaibuka madai mengine kwamba baada ya kushindikana kuwalipisha machinga kiasi hicho kufuatia serikali ya mkoa kuelekeza wamachinga walipe tu bei elekezi kwa soko ili kuipatia halmashauri mapato, DC kuona amekwama akaagiza H/Manispaa imrudishie fedha zake takribani milioni 106 ili alipe deni la benki kwa sababu zilitumika kwenye mradi wa maendeleo, jambo ambalo lilipingwa pia kwa sababu sio utaratibu wa serikali mtu binafsi kukopa na kuja kudai bila kufuata sheria na kanuni. Madai hayo nayo akayakanusha kupitia vyombo vya habari na kudai Mkuu wa Mkoa na Mbunge wanakwamisha jitihada za serikali (yeye) kuwasaidia wamachinga.

REJEA: DC Alberto Msando akopa milioni106 benki ili kuwajengea wamachinga sehemu ya kufanyia biashara

Hivi sasa yapo madai mengine kwamba ameagiza alipwe jumla shilingi milioni 279, huku akitaja majina ya wazabuni wawili waliojenga vibanda hivyo, majina ambayo hayatambuliki na Halmashauri wala mchakato wa zabuni haukufanyika. Na madai haya atayakanusha?

Mbaya zaidi, inasemekana Mkurugenzi na watumishi wa Halmashauri wametishiwa kufukuzishwa kazi endapo hawataidhinisha malipo hayo batili. Kama ni kweli, lazima kuna vielelezo vya barua, wasiogope, waweke mambo wazi.

MY TAKE: Kwa sababu hili ni jambo lenye harufu ya rushwa, wizi na matumizi mabaya ya ofisi na fedha za umma; ipo haja ya TAKUKURU na vyombo vya dola kufika Morogoro na kulichunguza kwa undani.

Inaumiza kusikia watu wanataka kuibia Serikali kwa sababu tu wameaminiwa na kupewa dhamana. Watanzania wa leo sio wajinga kiasi hicho. HILI LISIACHWE LIPITE HIVI HIVI!
Haikuwa busara kuanzisha mradi ule pale kwenye like Soko Kwa sababu kutokana na hivyo vibanda vya Msando Frem zisizo Ndani ya Soko kuu zimekosa wateja na pia kuongeza msongamano
 
Back
Top Bottom