beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,366
SIRI IMEFICHUKA! Kumbe vile vibanda vya wajasiriamali (Wamachinga) katika Soko Kuu la Chifu Kingalu vilivyojengwa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Albert Msando kwa kushirikiana na benki fulani, vimegeuzwa mradi wa kupigia pesa na kuiibia serikali? Hatari sana.
Itakumbukwa kuwa DC Msando alisema anakatwa kiasi fulani cha mshahara wake kila mwezi kulipia deni la benki alilokopa ili kujenga vibanda vile, tena alisema anajitolea.
REJEA: Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Albert Msando anasema anakatwa rejesho la mkobo wa kujenga vibanda
Imekuwaje leo anadai alipwe na Halmashauri? Lengo lake lilikuwa ni kufanyabiashara? Kuilaghai Serikali? Kusaka umaarufu wa kisiasa au kutapeli Wajasiriamali?
Tetesi zilianza kuenea kutoka kwa wajasiriamali wenyewe ambao walidai DC aliwaelekeza kulipia kati ya laki 5 mpaka laki 7 kila mwezi kwa kila kibanda, tena fedha hizo alitaka zilipwe kwenye akaunti yake binafsi. Tetesi hizo zikadaiwa ni uzushi.
Yakaibuka madai mengine kwamba baada ya kushindikana kuwalipisha machinga kiasi hicho kufuatia serikali ya mkoa kuelekeza wamachinga walipe tu bei elekezi kwa soko ili kuipatia halmashauri mapato, DC kuona amekwama akaagiza H/Manispaa imrudishie fedha zake takribani milioni 106 ili alipe deni la benki kwa sababu zilitumika kwenye mradi wa maendeleo, jambo ambalo lilipingwa pia kwa sababu sio utaratibu wa serikali mtu binafsi kukopa na kuja kudai bila kufuata sheria na kanuni. Madai hayo nayo akayakanusha kupitia vyombo vya habari na kudai Mkuu wa Mkoa na Mbunge wanakwamisha jitihada za serikali (yeye) kuwasaidia wamachinga.
REJEA: DC Alberto Msando akopa milioni 106 benki ili kuwajengea wamachinga sehemu ya kufanyia biashara
Hivi sasa yapo madai mengine kwamba ameagiza alipwe jumla shilingi milioni 279, huku akitaja majina ya wazabuni wawili waliojenga vibanda hivyo, majina ambayo hayatambuliki na Halmashauri wala mchakato wa zabuni haukufanyika. Na madai haya atayakanusha?
Mbaya zaidi, inasemekana Mkurugenzi na watumishi wa Halmashauri wametishiwa kufukuzishwa kazi endapo hawataidhinisha malipo hayo batili. Kama ni kweli, lazima kuna vielelezo vya barua, wasiogope, waweke mambo wazi.
MY TAKE: Kwa sababu hili ni jambo lenye harufu ya rushwa, wizi na matumizi mabaya ya ofisi na fedha za umma; ipo haja ya TAKUKURU na vyombo vya dola kufika Morogoro na kulichunguza kwa undani.
Inaumiza kusikia watu wanataka kuibia Serikali kwa sababu tu wameaminiwa na kupewa dhamana. Watanzania wa leo sio wajinga kiasi hicho. HILI LISIACHWE LIPITE HIVI HIVI!