Uchaguzi 2025 TAKUKURU hamuoni hizi Rushwa: Rais Samia achangia milioni 35, Mbunge na Mkuu wa Mkoa Songwe waongeza Milioni 11.5

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Nov 17, 2023
1,454
4,129
Wakuu,

Screenshot 2024-12-30 135153.png

Rais Samia Suluhu Hassan amechangia Shilingi Milioni 35 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa kanisa la Mtakatifu Petro la Anglikana Dayosisi ya Kusini Magharibi Tanganyika lililopo katika Jimbo la Makambako mkoani Njombe ambalo limeanza kujengwa kwa nguvu za waumini na wadau wachache maendeleo wa mkoa huo.

Akikabidhi mchango huo kwa niaba ya Rais wakati wa harambee iliyofanyika kanisani hapo katika kata ya Maguvani, mkuu wa mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka amesema Rais anatambua mchango wa makanisa katika kudumisha amani nchini huku akiwataka wananchi kuendelea kuunga mkono juhudi za Rais kwa kufanya kazi ili kukuza uchumi wao.

Kwa vimbwanga na vituko vingine kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ruka hapa: Uzi Maalum wa Vibweka na Hekaheka za wanasiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

1735556025612.png

Askofu wa Kanisa Anglican dayosisi hiyo Mathew Mhagama ameshukuru kwa dadaka hiyo huku wakiahidi kutumia kwa uaminifu kulingana na maombi ya kanisa.

Jumla ya Shilingi Milioni 60,123,000/= kati ya Milioni 310,000,000/= zinazohitajika kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa kanisa pamoja na ununuzi wa gari zimepatikana huku Mbunge wa jimbo la Makambako, Deo Sanga akichangia mil 5 na mkuu wa mkoa wa Songwe Daniel Chongolo akichangia mil 6.5

1735556087113.png
 
Samia anayanunua makanisa yote kuanzia kwa Mbowe huko mpaka kusikojulikana.

Mpaka Wazanzibari wamekasirika misikitini wanasema mbona rais hawakumbuki na wao?
 
Back
Top Bottom