TAKUKURU Arusha yabaini watumishi wawili kutengeneza control number bandia na kutengeneza kampuni hewa ili kuchepusha pesa!

Sasa ulitaka anyamaze au apuuzie kwa sababu ya Mfumo mbovu!

kwaupande wako mtu kuwajibika kwanini asisifiwe!
Kuna faida gani ya kutumia gharama kuzunguka huku hakuna positive effect? Kunyamaza hapana kwa sababu analipwa fedha za kodi yetu. Suluhisho ni kuleta mabadiliko ya mfumo.
 
Kuna faida gani ya kutumia gharama kuzunguka huku hakuna positive effect? Kunyamaza hapana kwa sababu analipwa fedha za kodi yetu. Suluhisho ni kuleta mabadiliko ya mfumo.
mabadiliko ya mfumo yanaletwa na utayali wa wananchi na sio mtu 1.

Kama wananchi hawajawa tayali kwa mabadiliko ni ngumu kwa mtu mmoja.

Yeye anafanya kwa nafasi na uwezo wake! Wewe kama raia imefanya nini ?
 
Takukuru Mkoa wa Arusha imesema Watumishi wawili wa Halmashauri ya Jiji La Arusha wanadaiwa kughushi Namba ya Mlipakodi na Kampuni hewa ya kulipia mapato

Hii ni baada ya RC Makonda kuagiza ufanyike uchunguzi

Source Jambo TV

Mlale Unono 😄😄🔥

=====
Tuhuma za kughushi nyaraka, uchepushaji wa makusanyo ya Serikali na ubadhirifu wa fedha za umma, zimechukua sura mpya baada ya watumishi wawili kudaiwa kuhusika kutengeneza namba bandia ya mlipakodi na kampuni hewa ya kulipia makusanyo hayo.

Kutokana na uchunguzi huo wa awali kubainisha hilo, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Arusha, inafanya uchunguzi wa mfumo mzima wa malipo ili kubaini kampuni nyingine hewa na namba bandia za mlipakodi zilizotumika kuchepusha kodi au mapato yoyote katika halmashauri hiyo.

Takukuru imefanya uchunguzi huo ikiwa ni agizo la Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda kufuatia tuhuma zilizowasilishwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala wa Utalii Tanzania (Tato), Wilbard Chambulo kudai kulipa kodi ya huduma Sh24 milioni, lakini akapewa risiti ya Sh3.6 milioni.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumapili Mei 26, 2024, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Arusha, Zawadi Ngailo amesema uchunguzi wa awali umebaini watumishi wawili wa halmashauri hiyo wamehusika kughushi nyaraka ikiwamo kutengeneza namba bandia ya mlipakodi na kutumia kampuni hewa kulipia mapato.
Hii ipo karibu halmashauri nyingi sana nchini.

Pesa ZINACHOTWA nchi hii kwenye kiwango cha kutisha.

Akina Kinana na Nchimbi kazi yao ni kumbeza Makonda, wakati wao hakuna jipya wanalofanya kusaidia wizi.
NCHI INALIWA VIBAYA
 
Back
Top Bottom