Takriban raia 132 wa Tanzania wanaoishi nchini Msumbiji wamefurushwa nchini humo

Huyo anae bisha ni mpumbavu na taahira wa akiri huku ni noma yaani zaidi ya noma na wote waishio katika wilaya ya montipuez wamepewa siku tano tu kuondoka hailishi una mali hauna wewe toka tu
Duuuh mshua alikimbilia huko sjui kama kapona##warudi tuu
 
Kuna taarifa tangu jana zilikuwa zikisambaa katika mitandao ya kijamii, kuhusu watanzania waishio Msumbiji wamekamatwa na serikali ya huko na kuuwawa!ikiwa ni pamoja kuwekwa jela kwa kilichoelezwa kuwa waondoke Msumbiji sikwao!! na hata kama ulikuwa na karatasi halali za kuishi huko na kufanya kazi wametiwa ndani pia ,na hawakuwa na mda wakusoma dokment za mtu yoyote!! hata pasi za kusafiria zimechomwa!! hadi jana watu walikuwa hawatoki ndani!!!Inasadikika watu 4 walipoteza uhai!.Na hilo katika kipindi cha PowerBreakfast cha Clouds amesikika mtu akiojiwa na Clouds kuhusu hali ya huko na alikuwa akiomba msaada.
Hivyo tunaomba serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje ichunguze hizi tuhuma.
Bwana yule yeye wala hajali tena kimoyomoyo anasema waache wafe tu

Hajishughulishi kabisa na watz waishio huko as long as hayupo ndugu yake aishie huko
 


Idadi ya Watanzania waliofukuzwa Msumbiji imeongezeka mpaka kufikia 132, huku idadi hiyo ikitarajiwa kuongezeka zaidi kutokana na operesheni ya kuwarudisha nyumbani wahamiaji haramu.
Akizungumzia suala hilo leo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Dk Suzan Kolimba pichani amesema operesheni hiyo haijawalenga Watanzania pekee bali raia wa nchi nyingine walioingia Msumbiji kinyume cha utaratibu.
Dk Kolimba amesema mji wa Montepuez uliopo jimbo la Cabo Delgado una Watanzania 3,000 wanaoishi huko na kwamba idadi ya watakaoondolewa inaweza kuongezeka zaidi.

"Tunaendelea kufuatilia tuhuma za baadhi ya Watanzania kwamba walifanyiwa ukatili wakati wanarudishwa nyumbani ili tujue hatua za kuchukua. Maofisa wetu wanashirikiana na serikali ya Msumbiji katika kuhakikisha Watanzania hawapati matatizo katika operesheni hiyo," amesema.
 
Mi naipenda Serikali ya Israeli yaani wakisikia mtu wao mmoja tu kaguswa weee watalaani vikali halafu wanawatuma wale Vijana wa Yossi Cohen ni wakali sana kwa hizo issue
 
Daah hakyamungu tunaonewa sisi sijui nani amemuanza mwenzake huko , serikali haitakurupuka lazima waandae environment nzuri ya kidiplomasia, hatukuzaliwa wagomvi sisi lakini hata babu yetu alitueleza upole wetu usizidi sana, aah wale na Malawi bana sawa bana sijui tumewakosea nini wanatupiga, Nasisimka sana kwa kweli aaah serikaliiiii sema sema, ongea nao kidiplomasia kwanza aaaah natetemeka
 
Kila watu warudi kwenye nchi zao bwana acheni kulalama na kumbwera kama hamna kwenu. Huko uliko ni nchi za wenyewe lakini bado unan'gang'àna tu, kwani kurudi kwenu mnapata shida gani?
 
Jamani jamani hali sio hali wilaya ya montepuez kuna JAMAA sasa ivi akitaka kunyanganywa gari lake na police lkn akawabia hii sitoi ni nimgaie muuza vocha kama mzaha tu JAMAA kampa kadi na funguo za gari yule muuza vocha na kumwambia nimekugaia gari iyo mbele ya police.oneni hali ilivyo nafikiri wazeni zaidi ...
 
Ila hawa msumbuji si tuliwasaidia sana kupata uhuru na wanajeshi wetu walipoteza maisha huko wengi tu
 
Ficha upumbavu wako
Huu ni uchochezi usio na maana
MOTOCHINI sijui unawaza kwa kutumia kiungo gani cha mwili. kwa vyovyote vile akili utakuwa umeiweka rehani na kuitupilia mbali kwenye dust bin. Wabongo wengi huku nje wanakufa sana tu na sometimes serikali haijui chochote kinachoendelea. Kuna wabongo wenye vibali/documents na wengine wamezamia/hawana vibali. Kwa mfano, RSA kuna wabongo wengi wako gerezani kwa makosa mbalimbali mengi yakiwa ya uhalifu. Kuna wengine huuawa na Polisi na ni vigumu kupata taarifa zao. Ishauli serikali yenu ianze jitihada za makusudu za kujua raia wake walioko nje ikiwa ni pamoja na kufuatilia maendeleo yao.
 
Nimemsikiliza sana Naibu Waziri wa Mambo ya nje akihojiwa kuhusu wanavyotendewa Watanzania walioko huko Msumbiji na matesa wanayopata nimepata mashaka kama utendaji ndani ya wizara hiyo uko sawa.

Haiwezekani Naibu waziri azungumze katika hali ya kutetea serikali ya Msumbiji kwa unyanyasaji wa raia wetu kuwa ni zoezi la kawaida wakati wanawake na watoto wanateseka kwa kuweka mahabusu siku tatu bila chakula wakati wengi wao wana vibali halali vya kuishi huko.

Serikali ndiyo ilipaswa kuwa ya kwanza kulaani jambo hilo ili Msumbiji wachukue hatua kwa maofisa wake wanaofanya mambo hayo, lakini sisi tunaona kuwa kufanya hivyo kuta leta hali ya kutoelewana. Unaelewanaje na serikali inayo nyanyasa raia wako? Yale mambo ya kihistoria inaonekana wenzetu wamesha sahau au kuyadharau.

Waziri achukue hatua haraka au awajibike kwa kushindwa kusimamia majukumu hayo muhimu ya wizara ya nje. Leo ni Msumbiji, kesho yaweza kuwa Zambia au Kenya.
 
Waliokuwa wakimbizi wa Burundi nchini Tanzania zaidi ya 152,572 walioingia nchini humo tangu mwaka 1972, wamekabidhiwa vyeti vya uraia wa Tanzania na kuwa huru kuishi kama Watanzania wengine.
Wakimbizi hao walikuwa wameomba uraia wa Tanzania mwaka 2008 na kupewa na waziri wa mambo ya ndani mwaka 2010, sasa ni halali kuchagua na kuchaguliwa katika nafasi mbalimbali za uongozi zikiwemo za udiwani na ubunge.
Akizungumza wakati wa ugawaji wa vyeti hivyo, mkuu wa makazi ya Mishamo, Frederick Nisajile alisema ugawaji wa vyeti hivyo ulianza Novemba 24 mwaka 2014 katika makazi ya Katumba mkoani Katavi magharibi mwa Tanzania ambako watu 56,554 walipewa vyeti vya uraia na baadaye kuhamia katika makazi ya Ulyankulu mkoani Tabora, magharibi mwa Tanzania ambako wakimbizi 43,453 tayari wamepewa vyeti hivyo.
Kwa upande wake msemaji wa wizara ya mambo ya ndani, Isaack Nantanga amesema hatua ya Tanzania kuwapa uraia wakimbizi hao ni kutokana na hiyari yao na kwamba serikali ya Tanzania ilishauriana na Burundi na hatimaye kukubaliana wapatiwe uraia wanaotaka wa kuwa Watanzania.
Hata hivyo si mara ya kwanza kwaTanzaniakutoa uraia kwa wakimbizi wanaoishi Tanzania kwa muda mrefu. Tanzania imefanya hivyo kwa wakimbizi wa Burundi na Somalia ambao wameishi Tanzania kwa miaka mingi.
===============================

w
alioingia nchini humo tangu mwaka 1972, wamekabidhiwa vyeti vya uraia wa Tanzania na kuwa huru kuishi kama Watanzania wengine.

Pia kuna wakati tuliona kwenye vyombo vya habari kuwa viongozi wanawaomba wakimbizi kuomba uraia ili wabaki kuwa Watanzania.

Hii hali sijawahi kuisikia kwenye nchi zingine, au sisi ndio wapole sana na hatuna uchungu na rasilimali au nchi yetu?.

Warwanda nao wanataka kututawala maporini mifugo wanaingiza wapendavyo. Tunachukiwa hata na wamalawi pia wazambia. Wakongo ndio kwao kabisa.

Sijui hii imekaaje?
 
Back
Top Bottom