Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 13,092
- 23,449
Kwanza naomba niwaombe moderators msipeleke huu uzi jukwaa la dini, kwa sababu lengo hasa ni kujadili maadili ya wanasiasa wetu Tanzania katika kuvumiliana na kudumisha maadili yao ya kidini.
Nimetafakari sana juu ya usemi kwamba kwa tajiri kuingia ufalme wa mbinguni ni sawa na ngamia kujaribu kupita tundu la sindano. Hata nikajiuliza, ikiwa ni ngumu hivyo kwa matajiri, vipi wanasiasa?
Tatizo la tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu bila shaka linatokana na tamaa ya kupata faida kwa dhuluma au ufisadi. Lakini si matajiri wote wako hivyo, na hata historia inaonyesha kuna matajiri wengi walikuwa katika mstari wa kupata ufalme wa Mungu.
Vipi wanasiasa? Hebu tuchukue hapa kwetu Tanzania. Mara nyingi sana nimeshuhudia, wanasiasa wa dini moja, huenda hata wanakwenda kanisa au msikiti mmoja, lakini katika mambo ya siasa wanakuwa ni maadui wakubwa! Mifano iko tele ya jinsi wanasiasa wetu wa dini moja, au kanisa moja, au msikiti mmoja, wakichukiana kwa kiwango cha juu kwa kuwa wako katika vyama mbalimbali. Hata imetokea kwamba wanasiasa wetu kwa tofauti za itikadi zao za kisiasa, wanaona ni kosa kutembeleana hospitali au misibani, japo wanaweza kuwa wa dini moja!
Na vipi basi kuhusu kusema uongo? Je inawezekana ukawa mwanasiasa na ukawa mkweli mbele za Mungu siku zote? Je kuwa mwanasiasa kunatoa nafasi ya kuwa mkweli kulingana na misaafu inavyotaka? Vipi ahadi kwa wananchi? Vipi kuambiwa kusema uongo ili kuepusha wananchi wasije juu dhidi ya chama au serikali?
Na vipi kuhusu kupanga mbinu za kukandamiza wanasiasa wengine, au vikundi vya kijamii, au taasisi, au kuwanyanyasa, mara nyingine hata kuamrisha wengine wafungwe jela au kupigwa pasipo makosa kwa kuwa tu mna uwezo wa kuwafanyia hivyo japo mnajua hamwatendei haki? Vipi yale tunayowatendea wapinzani wetu katika chama kimoja au cha upinzani pale tunapogombea nafasi za kisiasa kama ubunge au hata uraisi? Vipi suala la kulipiza kisasi, au hata tu kuwa na moyo wa kutaka sana nafasi itokee ili kulipiza kisasi!
Vipi suala la wizi, uwe wa fedha au wa kura, ili mwanasiasa mwingine, japo mko dini moja, asifanikiwe? Vipi udanganyifu kwa wananchi kuhusu matumizi ya fedha za serikali, hata kama ni kweli yalifanyika kwa faida unazodhani ni za serikali?
Kwa hiyo basi nimejiuliza, kwa namna siasa za nchi yetu zinavyokwenda, kwa kiasi kikubwa kukosa kuvumiliana, wanasiasa wetu wana nafasi rahisi zaidi kuigia ufalme wa Mungu kuliko matajiri, au ni tembo kupita tundu la sindano?
Kwa wanasiasa wote watakaosoma huu uzi, ningeomba mjitafakari sana, kuwa kwenu wanasiasa kunawaweka wapi katika suala na Ufalme wa Mungu, kulingana na mnavyowatendea wanasiasa na watu wengine, mara nyingine hata wale mlio dini moja, kanisa moja au msikiti mmoja! Kumbukeni huwezi kuwa na kipindi cha kuwa mtu wa siasa, na mtu wa dini, na ukadhani hilo ni sawa mbele za Mungu. Uko upande mmoja au mwingine.