Tahadhari na gari toyota rav 4 T129DEZ

Wandugu nimeona ni bora nika share hili jambo nanyi ili mchukue tahadhari.
Hilo gari linatumika kwenye uwizi wa vifaa vya magari.

Nilikuta likiwa limepaki karibu kabisa na gari langu mida ya saa 4 usiku, walipo niona wa kaingia kwenye gari na kuondoka. Kutizama gari tayari walisha vunja kioo kidogo na bonet walisha fungua.nikakimbizana nao nikafanikiwa kusoma hizo no za gari.

Nime report hili swala polisi wiki ya pili sasa mara mpelelezi hajapangwa na mara ya mwisho nimeambiwa file limepotea niende nika andike tena maelezo. Nime amua kutokwenda na kulireport hili jambo hapa.
Jeshi letu la Polisi siku hizi kama hujulikani na polisi yoyote utaisoma namba,jeshi la polisi kwenye kutoa msaada wana mapungufu kwa kweli,rushwa imekithiri wamekuwa mstari wa mbele kukuongezea mzigo baada ya kukupa msaada,na kwenye rushwa siku hizi wanatamka wazi kabisa lete kitu kidogo haya basi unaweza hata mtoa ili kesi yako ifuatiliwe kwa makini lakini ufuatiliaji hamna,ukipewa mpelelezi mimi huwa nashindwa kuelewa hivi wanapelelezea kesi ofisini maana huwa hawendi hata eneo la tukio sasa wanamkamataje mtuhumiwa, polisi wanatakiwa wabadirike mafunzo ya pale ccp wanapewa ni mazuri ila wakiingia mtaani wanabadirika hawa jamaa ni jipu
 
Back
Top Bottom