Tafakuri ya 2020; Tunamchonga Kagame wetu

lakini tunamuumba Kagame mwingine Museveni mwingine Mugabe mwingin
...mshana, hakuna nchi yeyote Afrika yenye uwezo wa kumuumba Kagame, at least not now. He is unique, among them leaders!
leo hii Rwanda iko vizuri kiuchumi na mambo mengine lakini sio demokrasia
...This is what stands him apart, from the bunch.

...His govt, runs in a very calculated way, wengi hawawezi kuiga as they don't have what it takes, don't care much, or don't have the will power.


PS. Studies on the man by African scholars, will do him and the motherland a great justice.
 
Tanzania na watanzania kwa ujumla ni watu wanao weweseka na mitetemo ya ubabaishaji lkn hata wasijuwe waendako,na utawaona wengi humu wakipingana na tafakari ya mwenzetu huyu lkn wakijisahaulisha kuwa kesho yao niyamashaka zaidi ya kujipendekeza kwa wenyenavyo ama watawala hawana uhakika wa maisha!
Tz pole sana
 
Umeona mbali.Mungu ibariki Zanzibar.Mungu ibariki Tanzaania.Mungu atujalie demokrasia Tanzania.
 
Swadaktaa umekuja na hoja nzuri naungana nawe lakini vema hali isije kufika walipofikia Rwanda lakini pia mambo yasije kufikia ya kama Zimbabwe hapo baadae kuwa na Rais wa maisha
Otherwise umechambua vema na kwa kina
Hata mimi huyo ulie m quote nimemuelewa na hata angalizo lako pia jamani ifike mahala tuwe wa kweli na mifano hai tunayo nchi imefikia pabaya watu wanaitafuna kama yao peke yao bila kuwakazia macho na kutomung'unya maneno wenetu watarithi nini?mashimo matupu baada ya dhahabu kuchimbuliwa?misitu isiyo na wanyama?miaka ileeee nchi inapata uhuru wasomi walikuwa wachache ila waadilifu leo wasomi lukuki ila uzalendo haupo.
 
China, Cuber, Korea Kusini, Ukihujumu Uchumi Adhabua Yake Ni Kubwa Sana.

ADHABU INAMADHUMUNI AU MALENGO MAWILI.
1. Kuumiza.
2. Kufundisha.

Ni Wazi Kwmb Unapotoa Adhabu Kubwa Kwa Kosa Kubwa Itajenga Nidhamu Na Hofu Kwa Wanaotumia Madaraka Vibaya Au Wezi Wa Mali Na Fedha Za Uma.

JPM Mpaka Sasa Anatoa Maamuzi Makali Na Magumu Lakn Anakwamishwa Na Sheria Za Nchi Kwa Kutoa Adhabu Ndogo Kwa Makosa Makubwa.

Mtumishi Kaiba Mabilion Ya Fedha Unamfunga Miaka Mi3 Na Pesa Alizoiba Unamwachia, Lakn Kama Sheria Ingesema Tuwanyonge Hawa Watu Ngekuwa Poa Na Watz Wote Tungejawa Hofu Hasa Viongozi.

Mh.JPM Mimi Namshauri Criminal Procedure, Afumue Criminal Law Pamoja Na Penal Code (Kanuni Ya Adhabu) Ili Kuongeza Ukali Ktk Element Zinazotengeneza Makosa Fulani Fulani Na Pia Kunyima Dhamana Baadhi Ya Makosa Ambayo Leo Hayana Dhamana Wakat Ni Makubwa.

Tanzania Bila Kuendeshwa Kwa Mwendo Wa Udikteta Wenye Uzalendo Nahakika Hatutafika Hata Kidogo Maana Tulishapoteza Dira Muda Sana Na Tulishazoea Wizi Tena Kwa Kuuhalalisha.

Tumuombeeni JPM Jaman Huyu Ndiye Mungu Alotupa Na Anawajali Sana Wananchi Hasa Wa Hali Ya Chini Japo Hawez Kupendwa Na Wote.

Ambaye atagoma kukubaliana na mawazo yako hasa wakati huu watanzania wakiwa wameoza kimaadili, ni lazima atakuwa na mtindio wa ubongo. Kwa stage tuliyofika, tukiondoa mawazo yetu ya kibinafsi, Kiongozi kama Magufuli ndiye nayetufaa. Tulishaoza kimaadili,ili tuweze kurudishwa kwenye mstari ni lazima tubanwe kidogo.
Kwa kukuondezea tu, sheria zetu kama zikifuatwa na kutekelezwa vizuri sio mbaya sana. tatizo tulilokuwa nalo ni kuwa Law enforcers wetu ni waoga na wapambanaji wa matumbo yao. FEDHA KIDOGO TU, wanalainika kam mlenda.
Angalia kwa mfano, sasa hivi JPM anapata mafanikio ya Serilaki yake kwa kutumia watendaji wepi? almost 99% ni wale wale ambao wameachwa na serikali zilizotangulia. Kinachofanya wawajibike sasa hivi ni mtindo wa kuongoza wa kiongozi mkuu, KIONGOZI MKUU ni mkali na hataki ujinga. Waliotanguliza walikuwa walaini wanaondekeza ujinga.
Otherwise, hongera magufuli, hongera president. Piga pini mpaka tunyooke, japo mtaani ni kugumu sana na hela hakuna. TUNYOOSHE TU.
 
Kwa mazingira ya Rwanda na historia yake Kagame asipofanya hivyo kwaajili ya Usalama wa nchi yake hiyo nchi isingekua hapo ilopo, kumbuka hao wapinzani wako nje ya nchi tena nchi zilizosapoti vita vya Rwanda kwahyo ni vibaraka wakubwa wanaotumwa na mabeberu, huwezi kufananisha na Tanzania huku tuko wenyewe hapa nchini na hakuna mpinzani ambae ni tishio kubwa kwa Usalama wa nchi, amini usiamini kila nchi inapambana na kila aina ya mtu au watu wanakweza hatarisha Usalama wa nchi.
 
Umenena Vyema Hapa, Na Unaaposikia Mtu Anaongea Maneno Kama Yako Basi Kajikana Mwenyewe Mara Dufu.
Mimi Nafurahi Sana Huyu Jamaa Anavyotunyosha Yani Mpaka Mwaka Wa Bajeti Naamini Kila Mmoja Atakuwa Kashajipanga Kifikra Na Kufanya Yaliyomema Badala Ya Kuliibia Taifa Ambalo Kila Mmoja Ndiyo Kimbilio Lake.
 
Kinachoendelea Zanzibar kinatisha, wale wote walio kinyume na ccm wanatekwa au kukamatwa live kupata mkong'oto kufungiliwa mashtaka mabaya ya kubuni na kutupwa lumande au kutupwa porini ukiwa hoi.....hali hii haitofautiani sana na huku Tanganyika bara japo huku kwa sehemu kubwa wanaofanyiwa hivyo ni viongozi na wabunge wa upinzani (CHADEMA, kule Zanzibar visiwani ni wanachama, wapenzi, wakereketwa wa CUF na viongozi wao
Kuna hii safu mpya inayoendelea kusukwa na Magufuli safu ya viongozi na wakuu wa idara mbalimbali za serikali...wengi kama si wote ni watu wa NDIO MZEE watu wa maguvu bila hekima wastaafu na vijana wenye uchu wa madaraka na matarajio makubwa...hii ni safu hatari kwa mustakabali wa demokrasia na siasa huru
Inaundwa mahakama ya mafisadi ni jambo jema sana, nchi ilifika mahali ikawa zaidi ya shamba la bibi au mzoga wa kiboko kila mnyama mla nyama alikuja akajing'atia pande lake...lakini hii mahakama ni ya muda...ikishamaliza kesi za mafisadi wote mahakimu na majaji watakuwa hawana kazi. Itabidi watafutiwe kazi second phase ya hii mahakama ni viongozi wa upinzani na wanachama wao..kesi za kubambikiwa zinakuja kesi za kuhujumu uchumi kesi za kuhatarisha usalama wa nchi....hizi zinakuja
Magufuli kasema haitaingilia mambo ya Zanzibar lakini atahakikisha usalama wa watu wa Zanzibar (wanaccm?)manake kinachoendelea huko Mungu pekee ndie ajuaye na ndio hicho hicho kitakachotokea Tanganyika bara 2020
Kwasasa tunamuona ni mzuri sana kwa jinsi ya utendaji wake ambao tuliutamani kwa miaka 30 hivi.kwamba hivi ndivyo mambo yalipaswa yawe bado tuko kwenye kiwewe na shangwe za watu kutumbuliwa majipu..lakini tunamuumba Kagame mwingine Museveni mwingine Mugabe mwingine
Kagame baada ya vita ya kimbari ya 1994 kwa miaka kumi ya kwanza akafanya kazi nzuri sana ikaongezeka mitano akapata sifa kubwa kitaifa na kimataifa leo hii Rwanda iko vizuri kiuchumi na mambo mengine lakini sio demokrasia, siasa huru za uwazi usawa na usalama... viongozi wengi wa upinzani wameuawa na wengine wamekimbia nchi
Kinachotokea kwa sasa kwenye ulingo wa siasa hakina dalili njema huko tuendako
Siongezi kitu hapa maana umeandika ambayo yako mawazoni mwangu.
 
Back
Top Bottom