Tafadhalini sana, tusipende kuchukulia mfano Rwanda kuhusu UCHOCHEZI na Vyombo vyetu vya Habari

Wiki hii tu, Lowassa kalalamika kuna gazeti limetoa habari za uongo kwamba amesema CCM itashinda uchaguzi mdogo wa madiwani Arumeru.
Kwahiyo huo ni uchochezi ambao hukumu yake ni kufungiwa kwa gazeti? Nafahamu kwamba kilichofanywa na gazeti hilo ilikuwa ni tafsiri ya gazeti kutokana na kile alichokizungumza Lowassa.
 
Kwahiyo huo ni uchochezi ambao hukumu yake ni kufungiwa kwa gazeti? Nafahamu kwamba kilichofanywa na gazeti hilo ilikuwa ni tafsiri ya gazeti kutokana na kile alichokizungumza Lowassa.
Kama gazeti halina waandishi wenye uledi wakutafsiri vyema habari ndogo kama hiyo bora lifungiwe na Rais atawafungia kweli wakiendelea kuleta udaku wa vijiweni.
 
magazeti hayo yameanza lini uchochezi,na huo ujinga wa watanzania kuamini uchochezi wanaotoka lini? awamu hii tutasikia mengi.
Muda mrefu tu. Jiulize kwanini sheria za makosa ya mitandao na huduma za habari zililetwa kwa ajili gani.
 
Mkuu nionavyo ni njia tuu yakuwatia hofu wananchi na waone kama kuna uchochezi wa vyombo vya Habari. Chunguza sana TV stations nyingi za ndani zimeingiza baridi yakutosha katika kutoa Habari.
Nionavyo inaandakiwa TBC 2 ambayo ni ruge TV ili kuweza kupotosha umma. Zipo Habari ambazo zinakosa kurushwa kwasababu yakuogopa mamlaka za juu.
Nakumbuka ile kauli ya Mbowe wakati wakushinikiza kuwapo maandamano. Akisema Magufuli akimaliza kukamata viongozi wakaisha atahamia kwenye vyombo vya habari na hayo ndio yanajitokeza sasa.
Watanzania haswa wamiliki wa vyombo vya habari inabidi kukaa chini kwa umoja na kujadili hili swala kwa kina na mapana. Ethics za uandishi ndio mwongozo wa kutoa habari na isiwe kwa utashi wa mtu mmoja. Ile kauli ya udicteta sasa inajidhihirisha wazi na viongozi wa dini mtakuja kulaumiwa sana na watanzania hapo baadae.
Viongozi wa dini kusema kwamba Magufuli ni chaguo la Mungu ni kumvisha ngozi ya kondoo wakati ni chui mla watu. Wapo wanaoumia kwa namna tofauti kutokana na maelekezo ya kutoka juu. Angalieni hilo na mpaze sauti kwa waumini na viongozi wasikie.
 
Muda mrefu tu. Jiulize kwanini sheria za makosa ya mitandao na huduma za habari zililetwa kwa ajili gani.

wile kama sheria ya huduma za habari ingekuwa ya kawaida zile m10 zilikuwa za nini?.
 
Kama gazeti halina waandishi wenye uledi wakutafsiri vyema habari ndogo kama hiyo bora lifungiwe na Rais atawafungia kweli wakiendelea kuleta udaku wa vijiweni.
Unafikiri habari zinazozungumziwa na Rais ni zile zinazohusu CCM kushinda uchaguzi Arumeru?!
 
wile kama sheria ya huduma za habari ingekuwa ya kawaida zile m10 zilikuwa za nini?.
Sijui vizuri kuhusu hizo shutuma za mil 10 kwa wabunge naamini hata wewe huna info za kutosha kuhusu hiyo scandal. Lakini kwakweli na uwazi nimependa hiyo sheria ya habari.
 
Unafikiri habari zinazozungumziwa na Rais ni zile zinazohusu CCM kushinda uchaguzi Arumeru?!
Ukiwa na mtazamo mmoja tu lazima utapinga kauli ya Rais lakini ukifuatilia haya magazeti wanapenda kuandika habari ambazo hawana uwakika nazo na wanaumiza watu wengi siyo tu Rais na nilitolea mfano wa Lowassa makusudi kuonesha vitendo vyao vinagusa wengi.
 
Mfano wako sio halisi. Na kama unatumia mfano huo kukubaliana na kauli ya Rais katika hili la kufungia magazeti utakuwa unashiriki kuminya haki za msingi za binadamu, ambazo ni pamoja na uhuru wa kufikiri na kuwa na mawazo tofauti na wengine.
 
Ili mtukufu kuongea kilugha kwenye mikutano ya kiserikali huu sio uchochezi
 
Bwana Mkubwa anataka habari za kumsifu tuu ,sii vinginevyo
Yeye ndio mjuzi,mweledi wa kila kitu na ndivyo anavyojiona
Ingawa wengine tunamuona ni mshamba tuu
Wabunge wa Dar es salaam waliwahi kumuita WAKUJA
 
Mfano wako sio halisi. Na kama unatumia mfano huo kukubaliana na kauli ya Rais katika hili la kufungia magazeti utakuwa unashiriki kuminya haki za msingi za binadamu, ambazo ni pamoja na uhuru wa kufikiri na kuwa na mawazo tofauti na wengine.
Siyo halisi? Wakati tukio/jambo limetokea. Kwa mtazamo wangu sheria mpya inasaidia kuweka msingi bora wa kutoa maoni na mawazo bila kukwaza au kuumiza wananchi wengine. Pia sheria inasaidia au itasaidia kupunguza usambazaji wa habari za uongo ambazo zinatishia usalama na umoja wa taifa letu. Period.
 
Ni dhambi kubwa sana kuuambia umma kua vyombo vyetu vya habari vinaweza kusababisha hali kama ya 1994, hii sio sawa! Tunatiana hofu bila sababu yeyote.

Hivi ni lini gazeti la Mtanzania, Tanzania Daima au Mwananchi limeandika kuhusu ukabila, udini, ukanda, rangi yetu au nafasi ya mtu kwenye jamii? Tusome tu historia ili tufahamu vyema UCHOCHEZI ulikuwa ukifanywa na vyombo vya habari huko Rwanda enzi hizo kabla ya Genocide.

Mwaka juzi huko Zanzibar tuliona na jinsi watu walivyobeba mabango kuwaponda wenzao kwa kuwabagua kwa rangi na kanda zao. Hao waliyafanya hayo wako wapi hivi sasa?

Tujaribu kuyachunga haya kwa u makini mkubwa ili kuilinda nchi yetu.
Mkuu, uhuru wa vyombo vya habari huwa na maana sana kama kila mtu akitambua kuwa hakuna kisicho na mipaka duniani.

Mwisho wa uhuru wako ndio mwanzo wa uhuru wa mwenzako. Hakuna uhuru wenye kufanana na soko la bangi duniani. Unapozidi uhuru ni mwanzo wa maumivu na uonevu kwa yule ambaye hana uwezo wa kujitetea.

Jamii za kiafrika zinashindwa kabisa kuheshimu uhuru wa mtu. Ndio maana uchawi na uonevu wa kila aina umejaa. Kila mtu anajiona anayo haki ya kumuumiza kisaikolojia mwenzake, bila ya hata kufikiria kwamba anayeumizwa na mtu kama muumizaji.

Rwanda na mauaji ya 1994, ni mambo yaliyoanza kimchezomchezo tu. Mtu anakula vizuri na familia yake, basi anajiona anayo kila haki ya kuwaudhi wengine, ukiuliza kisa unaambiwa na uhuru wa mtu kupewa na kupokea taarifa!.

Tanzania tusifike huko kipumbavu tu, na tunazo akili pamoja na utashi wa kukataa this kind of stupidity.

Mkuu, mimi na wewe tunayo haki ya kuongea tutakacho lakini hatuna haki ya kuharibu akili za watu kwa kisingizio chepesi cha uhuru wa habari.
 
Wiki hii tu, Lowassa kalalamika kuna gazeti limetoa habari za uongo kwamba amesema CCM itashinda uchaguzi mdogo wa madiwani Arumeru.
Namuonea huruma.mzazi wako maana akidhani kupata kumbe amepatikana.
 
Mtukufu anataka.kusifiwa tu.Na yalaumu Magazeti wameshindwa kabisa kusifia Mtukufu.Ningekuwa Mimi.ningemsifia sana tu.Mfano Mtukufu karuhusu kujenga nyumba za wahanga Bukoba,au Mtukufu ameamua kuwapa walofikwa na Jana chakula.Kwanini wasimsifu mtukufu??
 
Mkuu, uhuru wa vyombo vya habari huwa na maana sana kama kila mtu akitambua kuwa hakuna kisicho na mipaka duniani.

Mwisho wa uhuru wako ndio mwanzo wa uhuru wa mwenzako. Hakuna uhuru wenye kufanana na soko la bangi duniani. Unapozidi uhuru ni mwanzo wa maumivu na uonevu kwa yule ambaye hana uwezo wa kujitetea.

Jamii za kiafrika zinashindwa kabisa kuheshimu uhuru wa mtu. Ndio maana uchawi na uonevu wa kila aina umejaa. Kila mtu anajiona anayo haki ya kumuumiza kisaikolojia mwenzake, bila ya hata kufikiria kwamba anayeumizwa na mtu kama muumizaji.

Rwanda na mauaji ya 1994, ni mambo yaliyoanza kimchezomchezo tu. Mtu anakula vizuri na familia yake, basi anajiona anayo kila haki ya kuwaudhi wengine, ukiuliza kisa unaambiwa na uhuru wa mtu kupewa na kupokea taarifa!.

Tanzania tusifike huko kipumbavu tu, na tunazo akili pamoja na utashi wa kukataa this kind of stupidity.

Mkuu, mimi na wewe tunayo haki ya kuongea tutakacho lakini hatuna haki ya kuharibu akili za watu kwa kisingizio chepesi cha uhuru wa habari.
Uchochezi ni UPI??Shida Mtukufu hataki.kuona negative party ya utawala wake.Anataka kusifiwa tu.Ila yeye wanayohaki ya kutukana na kukashifu wengine.Na hasa Wapinzani. Lakini wengine hawana haki ya kukosoa pale anapokosea.Uhuru wetu kama unamipaka.hata Uhuru wake lazima uwe na mipaka.Tukikubaliana kwamba Uhuru wake.uwe na miaka.na wa kwetu uwe na miaka.basi hata Katiba itajeshimiwa.maana hata yeye hayuko.juu.ya katiba.Daima ukiheshimu wenzako lazima utaheshimiwa.Mtukufu wetu ni Kinara wa Matusi,majivino,kashfa kwa Wapinzani, ubaguzi,chuki na visasi.Aanze kubadilika Wakati ndiyo sasa
 
Namuonea huruma.mzazi wako maana akidhani kupata kumbe amepatikana.
Watu kama nyie uwa mnasikitisha sana. Mkiishiwa hoja mnaanza kuandika mambo ya ajabu..eti unawaonea huruma wazazi wangu wakati unakuta wako hata kausafiri hujawanunulia.
 
Siyo halisi? Wakati tukio/jambo limetokea. Kwa mtazamo wangu sheria mpya inasaidia kuweka msingi bora wa kutoa maoni na mawazo bila kukwaza au kuumiza wananchi wengine. Pia sheria inasaidia au itasaidia kupunguza usambazaji wa habari za uongo ambazo zinatishia usalama na umoja wa taifa letu. Period.
Angalau umeanza kuelewa. Sasa niambie nani anayeweza kuthibitisha kama habari fulani ni ya uongo au la? Sheria mpya haiwezi kusaidia kuweka msingi bora, bali inaweka vitisho ili kupunguza kasi ya kuibua maovu. Utawawekaje wanadamu sheria ya kutoa maoni wakati wanapozaliwa tu wanakuwa huru kutamka kitu! Unawawekeaje wanadamu sheria ya kutoa maoni ili hali una mahakama ambazo zinasubiri mtu anayehisi ametendewa ndivyo sivyo na mtoa habari?

Wanahabari wanafundishwa kitu kinaitwa "media law". Na wanahabari sio wajinga mno kiasi ambacho kinajaribu kuonyeshwa sasa. Hapo nikikuomba utuonyeshe habari moja tu ambayo inatishia usalama na umoja wa taifa letu utapata shida kuipata, na hata kama utaipata inaweza kuwa ni kwa mujibu wa unavyoona wewe. Katika jamii ambayo kutwa nzima inapambania madaraka na kutawala, tafsiri ya neno "kutishia usalama na umoja wa taifa letu" kuiachia kwa mtu mmoja au kundi tu la watu wachache ni hatari zaidi, bali kuachia vyombo kama mahakama, japo uhuru wake nao unatia shaka, lakini angalau inaweza kuwa hatua nzuri zaidi.
 
Irrelevant example.....kamwe huwezi kulinganisha ya Rwanda na Tanzania hata Kenya na Tanzania.

Nilimsikia wakati akiongea hiyo habari jana. Alipomaliza nikapiga magoti nikasema 'Ee Mungu umsaidie rais wetu, umpe hekima ya kuongoza, kinywa chake ukitawale wewe ili maneno yanayotoka yawe matamu yasije yakawa ni kiberiti katika msitu mkavu'
Ameen !
 
Back
Top Bottom