Tabora wamwambia Ditto kalale, yeye ajibu waambieni wake zenu!

akatuni001ur3.jpg

Si unaona nimerudi sasa mtanikoma bado nasubiri wanirudishie ile bastola yangu kibindoni.

Credit:Mjengwa blog
 
Haki ya nani hii ni Zarau kwa wananchi wa Tanzania.Yaani muuaji ndo anajibu hoja za wananchi.I am sure ana backup ya wakubwa ndo maana anajua hatuwezi mfanya chochote.Hayo ndo mambo mengine yanayozidi kuichafua CCM hakuna discipline ndani ya chama.
Tena utaona hakutakuwa na measures zozote zitakazo chukuliwa.Enzi za mwalimu huyo angetia Adabu tuu ila sasa nani wa kumkemea?
 
Jamani wanawake mko wapi? Dito anapowaambia mkalale ana maana gani zaidi ya kuwaonyesha dharau isiyo na kifani? Arudishwe Lupango huyu bwana akiokota hata jiwe atadhuru raia wema
 
Hii kauli ya Ditto kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa na serikali,ni aibu kubwa kwa serikali,wananchi wa Tabora pamoja na wanajamii wote,nawaombeni haya mambo yasiishie hapa,inabidi huyu mtu achukuliwe hatua.Amewadhalilisha wanawake wote,gender issues,hii ni poimt ya kummaliza kabisa na chama chake kinachowakumbatia watu wenye matatizo ya akili.Tena nasikia wapiga kura wengi wa ccm huwa ni wanawake,sasa huu ni wakati wa kujenga chuki baina ya ccm na wanawake,patamu hapo.Ditto utaimaliza ccm,umeshajenga chuki baina ya vijana na ccm,makonda na wapiga debe,madereva wa daladala,hawa wote wapo against nawe,achilia mbali wapenda haki wote tunaokuona hufai,kiongozi mzima unatembea na silaha mchana utafikiri upo Darful.Tuwasiliane na TAMWA kwenye issue hii.
 
haya Ni Matusi Ya Wazi Kabisa, Huyu Muuaji Anawatukana Akina Mama Na Sikutegemea Kwa Mtu Mwenye Akili Iliyokaa Sawa Kutoa Maneno Kama Haya Mbele Ya Wananchi.

Bibi Helen Kb Na Ananilea N Chukueni Hatua Juu Ya Udhalilishaji Huu Wa Akina Mama Zetu. Yeye Ndiye Anayestahili Kwenda Kulala, Tena Segerea. Ni Bora Angejibu Kalaleni Wenyewe, Lakini Waambieni Wake Zenu Wakalale, Hii Akili Ni Mbopvu

Hebu Wana Jf Ileteni Hii Kauli Ya Huyu Muuaji Tuichambue Vizuri
Pamoja na yote hii staili yako ya uandishi kwa kila neno kuanza na herufi kubwa inashangaza na kuchanganya sana...
 
Huyu ditto ni nani ktk nchi yetu?? je ni mungu mtu?? kwa nini mtuhumiwa aongozane na delegate ya serikali?? ina maana serikali iko proud naye na hakika wanajua wanachokifanya... wanabadilisha njigi ionekane njege.

Lakini ukitembea na mwizi nawe........
Unauliza ni nani katika nchi hii? Jibu lake ni kuwa alikuwa Bestman katika ndoa ya Mkwere! fullstop.Kwa hilo ktk nchi hii anaruhusiwa hata kubaka hadharani kisha wakasema HAKUKUSUDIA BALI ALIPATA HAMU YA GHAFLA. Mkihoji?, "mna wivu wa kijinga"
 
Ditopile should be in prison for delberate murder. What an arrogant person!
 
Maandishi hayasomeki kwa ufasaha.. hivyo kupunguza uwezekano wa kuelewa mtoa mada anakusudia nini!

wewe nae...........changia point bana, si kukosoa "staili" ya uandikaji ya mtu. Huko kwako kunaitwa kufilisika na kwenda personal pasipo na sababu ya maana.
 
Inashangaza sana. Pesa za kugharamia hizo ziara za mawaziri kueleza uzuri wa bajeti zilipitishwa kwenye bajeti ipi? Huu ni ufujaji wa pesa ambazo hata hivyo hazitoshi! Hebu fikiria, hizo hela zingejenga hata shule kadhaa tunazochangishwa kila siku. Bw Kandoro haoni aibu kusema atakata mishahara ya wafanyakazi ati kugharamia majengo (siyo shule) yatakayoitwa "shule za serikali", ilhali wenzie wanafuja hela kuelezea kitu ambacho kila mtu alisikia kwenye redio, televisheni au kusoma magazetini. Pengine mawaziri wetu hawajui kwamba watu wenye kiu ya taarifa kiasi cha kukubali kuhudhuria mikutano ya kisiasa ndio haohao wanaofuatilia kwa makini habari redioni, magazetini na luningani, kwa hiyo wanayajua haya yote, waliyasikia yalipokuwa bado ya moto. Wale wanaoenda kwenye mikutano kufuata bendi au pilao (kama ipo) huwa hawasikilizi kinachozungumzwa!

Yule adui "ujinga" bado yupo kwa kiwango cha juu sana, na hatari iliyopo ni kwamba ameivamia serikali yote! Au labda adui amevamia watu wote kwa hiyo vyovyote tutakavyochagua tutapata wajinga tu? Hali ni mbaya! Na tutazidi kuzalisha wajinga kupitia hizi shule zisizo na walimu, watoto wanaenda kushinda kwenye maeneo yanayoitwa shule ambayo hayana uongozi, kutwa nzima wanacheza na kufundishana matusi, kweli sijui hali itakuwaje.
 
"Sisi kamwe hatuwezi kupuuzia kauli za kina (Freeman) Mbowe na Kabwe) Zitto kama ulivyotuambia, wale ni mashujaa wetu&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG]; ni wakombozi wa wananchi maskini kama sisi," alisema Ponda.
 
Back
Top Bottom