TABORA: Askari JWTZ auawa baada ya kupigwa fimbo na wafugaji

Mwanajeshi kuuliwa lazima itatutoa kwenye ufahamu asilia kisa ujeshi!!!!!

Mwanajeshi ni binadamu kama binadamu wengine!!
Ugomvi ulikuwa wa kibinadamu kawaida kabisa, haukuwa ugomvi wa KIJESHI.

Mjeshi Marehemu alipuuza mbinu za medani za kivita hata auliwe kwa mangumi badala ya risasi za moto.

KIKOSI/VIKOSI VYA JESHI VIENDELEE NA SHUGHULI ZAO ZA KILA SIKU WAACHANE NA MPANGO WA KUVAMIA WATU WASIO NA COMBATI NA MABUTI ETI WANAMLIPIZIA ASKARI ALIYEPUNGUKIWA NIDHAMU YA KIJESHI HADI KUULIWA KAMA KUKU.
 
Linapokuja suala la mwanajeshi watu hujitia upofu, kwanini tusiziachie mamlaka husika za kushughulika na matukio.

Au wanajeshi wapo juu ya sheria kwa mujibu wa katiba?

Anyway waliohusika wasakwe popote walipo na sheria ichukue mkondo wake
 
Masai wanaona simba wameisha Na sasa wamegeukia mjeda,Mimi nauhofia huo mziki utakaopigwa Na sijui kama wataendana Na dj
Wapi umejua n mmasai? Au kisa umesikia mfugaji? Tabora hakuna wamasai na kama wapo ni wachache. Wengi wa wafugaji ni Wasukuma huko Tabora.
 
Tizeba Yule mnyarwanda Chasama uliyemkaribisha kwa Rushwa akameza hifadhi ya Mchangani kome Kwa KUJAZA ngombe Tokea Rwanda ukampa na uenye kiti Ccm sengerema! Utawambia Nini waliokuteua kama unabishi tuweke kwenye tovuti ya ikulu mkuu a one harafu usalama wa Taifa wakachunguze? mpee msg tzeba
 
Watu watatu wameuawa kwa nyakati tofauti mkoani Tabora akiwemo Askari wa Jeshi la wananchi wa Tanzania, (JWTZ)aliyepigwa fimbo na wafugaji akiwa katika ujenzi wa nyumba yake, baada ya kuwalalamikia kuwa, ng’ombe wamevamia katika kiwanja chake na kuharibu vitu mbalimbali vya ujenzi.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari mkoani Tabora Kamanda wa polisi mkoani humo ACP Hamis Issa Suleiman, amemtaja marehemu kwa jina la Carritus Mkunozi (35) wa kikosi cha 212KJ, ambapo ugomvi ulitokea baada ya kupishana kauli na wafugaji,na ugomvi kuanza, ambapo alifariki akiwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete muda mfupi,akipata matibabu.

Aidha amesema kuwa katika tukio hilo kundi kubwa la ng’ombe zaidi ya mia mbili,waliokutwa katika kiwanja cha marehemu huyo wanashikiliwa, na muuaji mmoja, huku akiwataja marehemu wengine, waliouawa kuwa ni mama mmoja,mganga wa kienyeji aliyepigwa fimbo kichwani baada ya kuwapa kisogo wauaji waliokuwa wamemwomba maji ya kunywa.

Katika hatua nyingine Kamanda Hamisi Issa Suleiman amesema huko kata ya kijiji cha Motomoto Vumilia wilayani Urambo kijana mmoja kibarua ambaye hakufahamika alipigwa ngumi kifuani na kufariki papo hapo, wakati wakigombea mgao wa posho ya kazi yao.

Chanzo: ITV
Tanzania sasa tusipo angalia tunaelekea kubaya sana
 
Pole yao hawa wafugaji ngoja moto uje sijui kama wataweza kuuzima watafute pakwenda siyo tanznia.
Wewe ni nani hadi uwaamulie pa kuishi?mbona nyinyi vijana wa lumumba njaa inawapelekesha kiasi hicho?
 
Inafika hatua Jeshi inabidi lirudi katika misingi yake ukauzu na kutochekea raia maana hawa watu wanaanzaga hivihivi kwenye taasisi zingine sasa wakifikia kuchezea sehemu ya jeshi na kuona hakuna reaction yoyote ipo siku watajitangazia uhuru wao kwa kuamini Jeshi haliwawezi.
Ubabe wa Jeshi letu hauepukiki kwa matukio kama haya Pumzika kwa Amani Askari wetu.
Wacha ushabiki wa kijinga, hapo inabidi kupata maelezo ya pande zote mbili ili kuweza kuamua siyo unakurupuka tu na kuanza upotoshaji wako
 
Wacha ushabiki wa kijinga, hapo inabidi kupata maelezo ya pande zote mbili ili kuweza kuamua siyo unakurupuka tu na kuanza upotoshaji wako
Sasa maelekezo gani unataka zaidi ya hayo? Umeambiwa kapigwa nyumbani kwake badala ya kuwaambia wafugaji mifugo yao inaharibu mazingira ya nyumba yake. Mbona kila kitu we unaleta upinzani tu we jamaa vipi?
 
Yaani ngumi ya kifua MTU ka rest in peace? Ndio maana mi nilishaachaga haya mambo ya kupigana
 
Inafika hatua Jeshi inabidi lirudi katika misingi yake ukauzu na kutochekea raia maana hawa watu wanaanzaga hivihivi kwenye taasisi zingine sasa wakifikia kuchezea sehemu ya jeshi na kuona hakuna reaction yoyote ipo siku watajitangazia uhuru wao kwa kuamini Jeshi haliwawezi.
Ubabe wa Jeshi letu hauepukiki kwa matukio kama haya Pumzika kwa Amani Askari wetu.

Kunamsamiati unaitwa Demokrasia umetutoa nidhamu watanzania.!
 
Mwanajeshi kuuliwa lazima itatutoa kwenye ufahamu asilia kisa ujeshi!!!!!

Mwanajeshi ni binadamu kama binadamu wengine!!
Ugomvi ulikuwa wa kibinadamu kawaida kabisa, haukuwa ugomvi wa KIJESHI.

Mjeshi Marehemu alipuuza mbinu za medani za kivita hata auliwe kwa mangumi badala ya risasi za moto.

KIKOSI/VIKOSI VYA JESHI VIENDELEE NA SHUGHULI ZAO ZA KILA SIKU WAACHANE NA MPANGO WA KUVAMIA WATU WASIO NA COMBATI NA MABUTI ETI WANAMLIPIZIA ASKARI ALIYEPUNGUKIWA NIDHAMU YA KIJESHI HADI KUULIWA KAMA KUKU.

Wewe ndio mpuuzi kwa hiyo ulitaka afande ajilinde kivita mbele ya Raia, ?

Mwenye uwezo wa kucheza Na wananchi ni polisi tu.

Je angeenda kuvuta SMG Na kuwamiminia risasi ungechangia nini saizi hapa zaidi kumlaumu afande.?

Acha hao wafugaji wakipate walichokiomba.!
 
Sasa maelekezo gani unataka zaidi ya hayo? Umeambiwa kapigwa nyumbani kwake badala ya kuwaambia wafugaji mifugo yao inaharibu mazingira ya nyumba yake. Mbona kila kitu we unaleta upinzani tu we jamaa vipi?
Ilibidi tupate kwanza maelezo ya pande zote mbili kutoka kwa wahusika,wacha ushabiki wako wa kilumumba lumumba
 
Back
Top Bottom