Kwenye topic ya Income distribution ya Economics kuna kitu kinaitwa Pareto Optimality:
Pareto optimality, is a state of allocation of resources in which it is impossible to make any one individual better off without making at least one individual worse off.
Kwa mtizamo wa namna hiyo, sisi tusiokuwa nacho tunaona kabisa kwamba chanzo cha sisi kukosa ni wale wenye nacho, na ikitokea nao wakakosa labda sisi tutakipata.
sababu kuu ni kuongezeka kwa gap kati ya walio nacho na wasio nacho swala ambalo limetengeneza chuki dhidi ya wasionacho.
Lingine, je nyie mnapokuwa nacho mnawahurumia wasio nacho?. watanzania wengi wakipata huwadharau walio chini na kuanza kujiwekea tabaka. Sasa msitegemee walio chini watawaheshimu.
Kuhusu kufurahia majipu mnadhani kuna atakayesikitika mwizi wa Mali za umma akihukumiwa? Mbona vibaka wakichomwa moto mtaani mnafurahi??
Hili tatizo mkuu lina mizizi halijaibuka tu ghafla. Wakati wa mwalimu Jk Nyerere huduma zajamii zilikuwa juu kiasi kwamba hakukuwa na tofauti kati ya maskini na tajiri (katika huduma za jamii)
Mtoto wamkulima namtoto wa waziri walisoma shule Moja, walikalia dawati moja nk. Vilevile Mzee mwenye nacho na asiyenacho walitibiwa hospitali moja nakuhudumiwa na nesi na Dr huyohuyo.
Hiyo ndo ilikuwa Tanzania ambayo ilikuwa moja, kilammoja alikuwa ndugu wa mwingine bilakujali ni nani, anatokea wapi na ana nini ama hana nini.
Tulipofika mahala tulatupana kilammoja akaanza kuangalia tumbo lake lishibe kwanza, nahata akishashiba haishii hapo tu bali alishe mpk mbwa wake kwanza. Hapo ndotulipotengeneza hii chuki tunayoona ndani ya jamii.
Msidhani matukio yaubadhirifu wamali za umma kama TWIGA kupandishwa ndege, Eppa, Escrow nk kwamba wasionacho hawafuatilii na haiwaumi. Inawama sana sema hawajui wamlaumu nani na wamsamehe nani. Kwahiyo ukiunganisha yote hayo+ ugumu wamaisha, hiyo chuki itaendelea kuwepo nakwa viwango vya kutisha huko mbele ya safari. Ni suala la wakati tu.
Solution nikuhakikisha umaskini unapungua haraka iwezekavyo hasahasa kwa kuanzia nakuboresha huduma muhimu za jamii kama Elimu sawa, matibabu nk.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.