Tabia 10 ambazo husababisha UMASKINI

Ethan Cruz

JF-Expert Member
Apr 29, 2021
231
331
1. Kutumia muda mwingi kuangalia TV, sinema au tamthiliya
{ Masaa mengi unayotumia kuangalia TV unaweza kuyatumia kufanya shughuli za kibunifu, na kuutengenezea thamani muda wako. kuangalia TV sio jambo baya lakini kutumia masaa mengi kuangalia TV, sinema au tamthiliya ni hasara}​
2. Kununua chakula (Fast food)
{ Hii ni tabia nyingine ambayo inatajwa ambayo kama hairekebishwi hupelekea umaskini. Kama haukumbuki ni lini ulipika mwenyewe nyumbani kwako kwasababu unanunua chakula wakati wote basi hiyo ni dalili mbaya
Tofauti na hilo, kununua vyakula hivi husababisha matumizi ya pesa makubwa ambayo yanaweza kuepukika. Kwa mfano kama pizza moja ni sh elfo 20, mtu anaweza kutumia robo au theluthi ya pesa hiyo kununua chakula na kupika mwenyewe mlo kamili yaani balanced diet.}

3. Kuchelewa kuamka
{ Tabia hii kufanyika katika umri wa ujana inaelezwa kuwa ni dalili ya kuukaribisha umaskini katika siku za mbeleni
Vijana ambao wanakuwa wazembe kufanya kazi kwa bidii kwenye kipindi chao cha ujana, hufanya kazi zaidi na kwa tabu wakifika umri wa kuanzia miaka 40 tena yawezekana bila malipo makubwa, na hii ni kwasababu hawakutumia vizuri muda wao wa ujana kufanya kazi na kuwekeza kwa ajili ya miaka ya mbeleni }

4. Kulaumu wengine kwa matatizo unayopitia
{ Wataalamu wa uchumi wanaeleza kuwa moja ya tabia zinazoweza kumfanya mtu awe maskini ni pamoja na kulaumu watu wengine kutokana na kutofanikiwa kwako

Jambo baya likitokea, masikini huwa wahanga wa jambo hilo lakini matajiri hulitafakari, na kuangalia sababu halisi ya jambo hilo kutokea kisha kuhakikisha halitokei tena au likitokea haliwaathiri au hata kuhakikisha wanatumia fursa yoyote inayopatikana katika janga hilo ili kunufaika nalo.

5. Kutoweka akiba
Akiba ni jambo la msingi sana katika mapato yoyote yanayopatikana. Akiba ya pesa husaidia pindi likitokea tatizo, inaweza kuwa ugonjwa, safari ya dharura na kadhalika. Kama huna akiba likitokea tatizo itakubidi uuze mali yako yoyote au uchukue mkopo ili kutatua tatizo hilo.

Tofauti na kutokea kwa matatizo, kama umeweka akiba na ikatokea fursa ya wewe kutumia pesa ili kuingiza faida, utanufaika kuliko mtu asiye na akiba, na huo ndio uzuri wa kutunza akiba ya pesa.

6. Kufanya manunuzi yasiyo kwenye mpangilio
{ hi ni kama kuchukua mkopo ili kununua vitu ambavyo havizalishi pesa, kama kuchukua mkopo kununua furniture za ndani, au gari la kutembelea na vinginevyo. hiyo ni hasara na hupelekea umasikini.}

7. Kuzaa watoto wengi
{ Wataalamu wanaeleza kuwa kipato kikiwa kidogo na watoto wakiwa wengi kwenye familia, kiwango cha umasikini kinaongezeka kwenye familia hiyo.
Inaelezwa kuwa matajiri wengi duniani, hawana watoto wengi japo kuwa wanauwezo kifedha na wangeweza kuwahudumia, wanajua ni gharama kuwapa watoto mahitaji yao yote ya msingi, tena kwa wakati.

8. Kutopima afya mara kwa mara
{ Kupima afya mara kwa mara kunasaidia kujua mapema kama una ugonjwa unaoanza mwilini mwako, hii ina faida kwani uwezekano wa kutibiwa na kupona kabisa kwa ugonjwa huo ni mkubwa zaidi lakini pia gharama utakazotumia kwa ajili ya matibabu zitakuwa nafuu kuliko ambazo zingetumika wakati ugonjwa umekuwa mkubwa.
Ni kama ilivyo kwa ugonjwa wa saratani, kujua mapema ndio uhakika kwa ugonjwa huo kutibiwa na kupona mapema tofauti na ukiwa umekomaa, au hata ugonjwa wa kifua kikuu, au figo na magonjwa mengineyo.

9. Kutumia pesa kabla ya kuzipata
{ Kama una tabia ya kukopa pesa kipindi ambacho hauna pesa huku ukitarajia kuzilipa pindi utakapopata pesa, hiyo ni dalili ya umaskini kukunyemelea.
Kuepuka athari hii wataalamu wanashauri kufanya kazi kwanza na kupata pesa kisha uendelee na kufanya matumizi ambayo unayahitaji.}

10. Kuwa na marafiki wasio na malengo makubwa
Marafiki huweza kukusaidia kufikia malengo yako uliyojiwekea, lakini pia huweza kufanya usifikie malengo yako hayo.

Inashauriwa kuwa kama unataka kufanikiwa hakikisha unatumia muda mwingi zaidi na marafiki ambao wana malengo makubwa ya maisha, wanawaza mambo chanya na sio mambo hasi muda wote, ambao wanakukumbusha kufanya vitu vya msingi.

Hii inaweza kuwa kutunza muda, kutokata tamaa kwenye malengo yako au kuwa mbunifu zaidi, na hata kukukosoa kwa tabia ambazo zinarudisha nyumba maendeleo yako.
 
Umenigusa hayo manne ya mwanzo yote nafanya ila kwanzia la 5 had mwsho ndo sifanyi
 
Nakubaliana na wewe kwa asilimia kubwa hasa point namba 7 na ninapingana na wewe pakubwa hoja namba 3.

Hoja namba nne! Kuamka mapema ni relative term. Binafsi mara nyingi huamka saa 4 hadi 6 asubuhi na hulala saa 11 fajri.
Hahahahah hilo la masaa angesema kuwa productive hours zinatakiwa zizidi mapumziko! Sio unapumzika masaa 20 unafanya kazi masaa 4 unless uwe mtoto wa Zakaria au Bhakressa!
 
As long as kufa ni Pie!

Siwezi kujitesa nitafanya the basics tu niishi maisha standard tu! Sina ulazima wa kuendesha gari la million 600 au nyumba ya billion 3 ikiwa ntalala masaa machache kuliko nayokuwa active!

Kula ntakula vizuri, bata ntakula na saving nitafanya! Ila siwezi kujitesa eti natafuta utajiri! I only need economic freedom tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom