mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,234
- 4,602
Nipende kuipongeza japo kinafiki Mamlaka ya Maji DAWASA kwa kutupoza machungu ya kutokuwa na maji takriban wiki nne. Binafsi natambua kuwa suala la huduma ya maji ni gumu sana hivyo lawama haziepukiki.
Natamani kuwepo na taarifa ya ratiba ya mgao wa maji kwa maeneo ambayo yana changamoto hasa huku Tabata na Maeneo mengine.
Naamini wananchi tukishakuwa na taarifa sahihi inaweza kusaidia kuondoa kero hii. Haiwezekani mkate maji mwezi mzima kimya kimya bila taarifa, huko ni kutudharau wateja wenu.
Halafu ule mradi wa ujenzi wa kuongeza msukumo wa maji mlioahidi unaisha Aprili, please naomba mkamilishe kwa wakati ili kuondoa mateso haya.
Tabata Bonyokwa tunawapenda sana DAWASA na Waziri wetu wa Maji.
Pia naomba muifufue akaunti yenu ya DAWASA hapa JF. Tokea Aprili 2021 mmesepa, sasa mtasikilizaje kero za wateja wanaotumia JF?
Ni mimi Msemaji wa Suala la Maji Tabata Bonyokwa
Pia soma

- KERO - DAWASA mnazingua, mimi si wa kuamka usiku kukinga maji ya mvua ya matumizi ya nyumbani
- DOKEZO - Tabata Bonyokwa hatujaona tone la maji wiki ya tano sasa, DAWASA mnatuona manyani?
- KERO - DAWASA mnazingua, mimi si wa kuamka usiku kukinga maji ya mvua ya matumizi ya nyumbani
- Bonyokwa Wakumbukwa: DAWASA wanajenga kituo cha kusukuma maji (Booster pump), ujenzi wafikia 30%