Nakweli bodi wamekosea olduvai iko wilaya ya ngorongoro .mkoa Wa Arusha .sio manyara .hawa nao jipuHivi Ngorongoro ipo Manyara au Arusha?wakenya wapo sahihi kama hata vya kwetu tunakosea.Tunaomba mkuu wa mkoa wa Arusha apinge huu upotoshaji..
Shafi-abeid achana nae !yule punguani wala hastahili kujadiliwaPreta. Safi sana. Brain. Umetoa ufanunuzi mzuri na uliokwenda shule. Hebu nisaidie kutag ujumbe wako huo kwa yule ndugu Shafi_abeid. Nadhani akisoma ujumbe wako huu akaendelea kubishana basi atakua kichaa indeed.
Mimi nilitaka wamshtaki huyo kijana, kwanini atumie jiografia yetu kuitangaza nchi yake? Hii ni hujuma na bodi ya utalii inatoa majibu yasiyo na tija kwwnye sakata hili la kudhurumiwa haki zetu, maana hawajasema ni hatua gani itachukuliwa endapo hali hii itaendelea kujitokeza tena na tena.Hawa TTB ni makenge. Walitakiwa wapost kwenye mitandao mikubwa duniani ikielezea hayo. Ioneshe kwenye ramani location ya Olduvai Gorge ilipo na waweke coordinates sio wanalaumu. Pambaf TTB
Lugha inasumbuaHawa TTB ni makenge. Walitakiwa wapost kwenye mitandao mikubwa duniani ikielezea hayo. Ioneshe kwenye ramani location ya Olduvai Gorge ilipo na waweke coordinates sio wanalaumu. Pambaf TTB
mkuu wameona fursa mm siwalaum ss Tanzania ndiyo vilaza vya kwetu tunashindwa kuvitangaza vipo vitu vingi sana Ila it nashindwa kuvitangaza sijui tatizo lipo wapi hiyo bodi kazi yake niniWakenya wanalaana sana.
LAITI KAMA HILI JAMBO LINGEKUWA LIMEIKUTA KENYA,LINGETREND WIKI NZIMA TWITTER NA KILA MTU ANGAJUA UKWELI.ILA KWA KUWA MITANZANIA NI MIMTU KILA MMOJA NI WA KULALAMIKA TU HATA INAYOJIITA MISOMI.WANACHOWEZA NI MATUSI TUU MITANDAONI.WAKENYA WANASAIDIA KUTANGAZA NCHI YAO MPAKA MITANDAO KIBAO DUNIANI SISI NI WAZEE WA SERIKALI HAIFANYIKumbe na sisi watanzania ni wakenya
View attachment 326577
Hili kanusho mlengwa ni nani?Watanzania au?Maana liko kwa lugha ya kiswahili na msemaji alitumia lugha ya Kiingereza . je wamewasiliana na taasisi husika?BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imekuwa ikifuatilia kwa makini majadiliano yanayoendelea katika mitandao mbalimbali ya kijamii kufuatia video iliyotumwa katika YouTube
na imekuwa ikisambazwa kupitia njia mbalimbali za habari ikimuonesha mtu mmoja kutoka nchi jirani akisema kuwa Olduvai Gorge ambayo kimsingi iko Tanzania kwamba iko Kenya.
Video hii imeibua majadiliano katika mitandao ya kijamii baina ya watanzania na watu wengine ambao wanaitakia mema Tanzania na wanaoelewa vizuri kuwa Olduvai Gorge iko Tanzania.
Bodi ya Utalii Tanzania kama taasisi ya Umma yenye jukumu la kuvitangaza vivutio vyetu vya utalii imeshtushwa na video hii iliyojaa upotoshwaji mkubwa ambao tunaamini mbali ya malengo mengine inalenga kuchafua kazi nzuri ambayo imekuwa ikifanywa na Bodi kwa kushirikiana na wadau wengine katika kutamgaza vivutio vya utalii vya Tanzania ikiwemo Olduvai Gorge.
Tunapenda kuchukua fursa hii kupinga vikali upotoshwaji huu uliofanywa na mtu huyo wakati akihutubia mkutano ambao tumeambiwa ulikuwa ni wa Vijana wa Umoja wa Mataifa uliofanyika Amerika mwezi Agosti mwaka jana.
Tunapenda dunia ifahamu kuwa kama ilivyo kwa Mlima Kilimanjaro, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Zanzibar n.k Olduvai Gorge mahali panapoaminika kuwa ndipo binadamu wa kwanza duniani aliishi na ambako Dr. Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la binadamu huyo wa kale anayesadikiwa kuishi miaka takribani milioni 2 iliyopita iko pia Tanzania na si mahali pengine popote duniani. Eneo hili la Olduvai Gorge liko katika bonde la ufa katikati ya bonde la Ngorongoro na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Manyara nchini Tanzania.
Tunatoa wito kwa watanzania mahali popote walipo kuendelea kuunga mkono juhudi za Bodi ya Utalii Tanzania za kuitangaza Tanzania na vivutio vyake vya Utalii kwa kujibu na kusahihisha papo hapo bila woga mara tu taarifa ya upotoshaji kuhusu nchi yetu inapotolewa iwe ni kwenye mikutano ya ndani ya nchi au ya Kimataifa.
Tunaamini kuwa ni jukumu la kila mtanzania kuitangaza Tanzania na vivutio vyake vya Utalii badala ya kuiachia TTB kazi hii peke yake.
Yawezekana katika mkutano huo wa vijana ambao mjumbe huyo wa nchi jirani alipata fursa ya kuzungumza na kufanya upotoshaji huzo, wajumbe wa Tanzania pia walikuwepo ambao wangweza kukosoa upotoshaji huo papo hapo na kuelezea ukweli na usahihi wa mahali ilipo Olduvai Gorge.
Imetolewa na:
Ofisi ya Uhusiano
BODI YA UTALII TANZANIA