Taarifa potofu kuhusu wahisani 10 kusitisha misaada yao kwa Tanzania

Mtu yoyote anayejua ukweli juu ya jambo lolote anaweza kulikanusha akiwa na usahihi wa tarifa.
Hivi nyie watu wa lumumba mmelishwa nini ?? Kwa hiyo siku hizi government decisions zinatolewa tu na mtu yeyote ?? Nyie ndio mnaotuma SMS kwa mkurugenzi kuhakikisha flow meters zinafanya kazi

Kwa akili yako hizo balozi zitachukulia hizo kanusho za kina Pole pole kwamba ndio msimamo wa serikali yetu ?
 
TAARIFA POTOFU KUHUSU WAFADHILI 10 KUSITISHA MISAADA YAO KWA TANZANIA

Kumekuwapo taarifa potofu kwamba Wahisani karibu 10 wamesitisha misaada yao kwa Serikali ya Tanzania. Taarifa hizi ni za uongo na upotoshwaji na zinalenga kuleta taharuki miongoni mwa jamii ya watanzania.

Binafsi kama raia ili kujiridhisha nimewasiliana na Wizara ya Fedha na balozi mbili (kupitia Maafisa wao waandamizi) na kote taarifa hizi hazina ukweli wowote.

Kilichotokea ni Mwandishi wa Shirika moja la Habari la nje, kunukuu vibaya mazungumzo ya kiongozi wa Wizara ya fedha wakati wa shughuli ya kutiliana saini msaada uliotolewa na Serikali ya Japani kwa Tanzania.

Kilichotakiwa kuripotiwa ni kwamba, wafadhili hapa Tanzania wanaisaidia Serikali kwa njia mbalimbali ikiwemo (a) Mfuko wa Pamoja wa kusaidia bajeti ya Serikali au "General Budget Support (GBS) (b) Misaada ya Kisekta kama vile kilimo, nishati na usafirishaji pamoja na (c) Misaada kwa miradi.

Kilichotokea ni kwamba nchi wahisani sera zao zimekuwa zikibadilika kipindi hadi kipindi na kupelekea kubadilika kwa mtindo wa kutoa msaada kwa nchi yetu. Nchi kadhaa zimeonelea zisiendelee kusaidia Tanzania kwa mtindo wa GBS na badala yake wanaendelea kusaidia Tanzania katika sekta na miradi husika. Sekta hizi na Miradi hii iko katika vipaumbele vya Serikali.

Mwandishi yule wa Habari alijikanganya na kuchanganya maelezo hayo juu na kujulisha chombo chake cha Habari na hatimaye umma wa watanzania taarifa ambazo sio za kweli.

Rai yangu kwa Wananchi wenzangu, ni kwamba ni kweli misaada ni jambo jema lakini ni bora isije kama itakuwa inakuja katika masharti yanayotweza utu na heshima ya Taifa letu Tanzania.

Humphrey Polepole
Raia wa Tanzania

NB: KESHO ASUBUHI IJUMAA TAREHE 1 NITAKUWA CHANNEL 10 KUENDELEA NA UCHAMBUZI NA UFAFANUZI WA MASUALA HAYA.
Ni kweli hakuna misaada isiyo kuwa na masharti lakini hulazimishwi kupokea na pia kama masharti yake huyawezi tulia kaa kimya tafuta sehemu nyingine ambayo unaweza masharti yake au kama vipiii jitegemee uachane na misaada au mikopo kama unaweza sio unanyimwa kwa kutokukidhi masharti afu ndo huzitaki hizi mbichi viongozi wetu wanatuangusha sana miaka hamsini madarakani leo ndo wanazungumzia kujitegemea kama emergence vile duh
 
TAARIFA POTOFU KUHUSU WAFADHILI 10 KUSITISHA MISAADA YAO KWA TANZANIA

Kumekuwapo taarifa potofu kwamba Wahisani karibu 10 wamesitisha misaada yao kwa Serikali ya Tanzania. Taarifa hizi ni za uongo na upotoshwaji na zinalenga kuleta taharuki miongoni mwa jamii ya watanzania.

Binafsi kama raia ili kujiridhisha nimewasiliana na Wizara ya Fedha na balozi mbili (kupitia Maafisa wao waandamizi) na kote taarifa hizi hazina ukweli wowote.

Kilichotokea ni Mwandishi wa Shirika moja la Habari la nje, kunukuu vibaya mazungumzo ya kiongozi wa Wizara ya fedha wakati wa shughuli ya kutiliana saini msaada uliotolewa na Serikali ya Japani kwa Tanzania.

Kilichotakiwa kuripotiwa ni kwamba, wafadhili hapa Tanzania wanaisaidia Serikali kwa njia mbalimbali ikiwemo (a) Mfuko wa Pamoja wa kusaidia bajeti ya Serikali au "General Budget Support (GBS) (b) Misaada ya Kisekta kama vile kilimo, nishati na usafirishaji pamoja na (c) Misaada kwa miradi.

Kilichotokea ni kwamba nchi wahisani sera zao zimekuwa zikibadilika kipindi hadi kipindi na kupelekea kubadilika kwa mtindo wa kutoa msaada kwa nchi yetu. Nchi kadhaa zimeonelea zisiendelee kusaidia Tanzania kwa mtindo wa GBS na badala yake wanaendelea kusaidia Tanzania katika sekta na miradi husika. Sekta hizi na Miradi hii iko katika vipaumbele vya Serikali.

Mwandishi yule wa Habari alijikanganya na kuchanganya maelezo hayo juu na kujulisha chombo chake cha Habari na hatimaye umma wa watanzania taarifa ambazo sio za kweli.

Rai yangu kwa Wananchi wenzangu, ni kwamba ni kweli misaada ni jambo jema lakini ni bora isije kama itakuwa inakuja katika masharti yanayotweza utu na heshima ya Taifa letu Tanzania.

Humphrey Polepole
Raia wa Tanzania

NB: KESHO ASUBUHI IJUMAA TAREHE 1 NITAKUWA CHANNEL 10 KUENDELEA NA UCHAMBUZI NA UFAFANUZI WA MASUALA HAYA.
Hongera mkuu kwa kutoa elimu na fafanuzi makini kuepusha upotoshaji kwa jamii.
Ndugu polepole bila kufanya hivyo ni shida, kwani tunao watu baadhi wakishirikiana na wakoloni kuhakikisha kama nchi haijikwamui.
Endelea kuelimisha umma.
 
inamaanaa BBC ni waongoo.. akapimwe akili huyu jamaa
Anko kwa taarifa BBC ni chombo cha mkoloni cha kupropagate mambo wayatakayo kwa maslahi yao. Istoshe ni wanadamu, hawajakamilika, wanamapungufu yao.
Take care guy!
 
Back
Top Bottom