Taarifa muhimu toka kamati tendaji ya CUF kwa watu wote

Lipumba anaongoza mpaka sasa 2-0 ngoja mpambano uendelee
Anaongoza kwa lipi??? Hizo mbili amfunge maalim ama??? Maalim alishakuwa makam wa rais na akaunda baraza la mawaziri na cuf yake huyo lipumba alishawahi kuwa na hata halmashauri moja huku bara toka aanze kuwa mwenyekiti wa cuf????

Hivi leo hii cuf ikifa nani ana lakupoteza maalim au lipumba?? Cuf zanibar haihagawanyika sasa lipumba bila cuf zanzibar anaweza kusimama peke yake na kukijenga chama upya kma alishindwa kwa miaka 20??

Eti hizo 2-0 ni zipi
 
Kama akina mkwawa wangekuwa walalamishi hadi sasa nchi isingekuwa na uhuru - mnatakiwa kuazimia nini mfanye iwapo vyombo vya dola mnavyotupia lawama vitawapokonya ushindi
Mkuu waliwahi kuandamana mwaka 2001 wakapigwa risasi na kuuawa watu kibao na maelfu wakakimbia zenji na kuwa wakimbizi.

Wakaja tena wakasusa ili at least nafsi ziwasute bado tu mmeonekana kutojali kilio cha wazenji wapenda haki
Haya wakishiriki uchaguzi wakiporwa ushindie bado wwe unawakejeli eti walalamishi???
Sasa ulitaka wafanyeje??

Wwe unajua kabisa wakialika al shabaab au ISIS iwasaidie kwenye jihad uko zanzibar hali itakuwa mbaya zaidi na pengine tukazaa somalia nyingine na mwisho wa siku nchi itabakia magofu kma syria......najua tukifika huko tutaheshimiana ila je we ndio unaona hilo ni suluhisho yaani tuanzishe timbwili timbwili na tufadhili vikundi vya magaidi kma anavyofanya mtu fulani kule kenya??

Eti hya wasilalamike unataka wafanyeje maana ni kma wametumia mbinu zote za kikatiba kudai haki yako wwe unataka wafanyeje labda??
 
Mkubali mkatae NCHI HII HAKUNA UPINZANI TENA.......haiwezekani miaka nenda rudi VIONGOZI WA UPINZANI NI WALE WALE na hii ndio inayopekea mpaka UPINZANI UNAPOTEA NCHI HII kwanini ninasema hivi....
ninasema hivi nikiwa na maana ya kwamba hakuna kitu muhimu sana katika maendeleo kama kuruhusu FIKRA MPYA NA MAWAZO MAPYA kutoka kwa watu wengne hapa namaanisha HIVI VYAMA PINZANI VIONGOZI WAO WOTE WALIOPO WAKUBALI KUWAJIBIKA KWA KUACHIA Mdaraka na kuruhusu WATU WENGNE WAONGOZE na ndicho tunachokiona kwa CCM sasa.....IMEKUJA SAFU MPYA KABSA ambayo mpaka imepelekea UPINZANI KUFA na kuonekana kama MATAPELI FULANI na CCM kuonekana kama ndio mkombozi wao..........Chaguzi ndogo zilizofanyika ni kipimo tosha kabsa kuthibitisha hili NA WAPINZANI WANABAKI WANA LIA LIA ETI CCM inatumia DOLA.....sasa kama inatumia dola kwanini mnaendelea kushiriki hizi CHAGUZI na mnatumia kodi za watanzania kwenye CHAGUZI ambazo mnajua kabsa mwisho wa siku CCM itarumia DOLA na kushinda????
\hivi tukisema nyie ni majizi mnatumia kodi zetu kupitia RUZUKU sivyo ndivyo tutakuwa tumekosea????
Na itakuwa vipi kama tukisema MNAJUA KABSA HAMNA TENA MVUTO kwa wananchi kwa sasa na mnabaki mnasingizia DOLA kama DEFENCE MECHANISM ya kuendelea KUWA MAJIZI YA ruzuku yetu?????
Nchi haina upinzani ina walaji tu na kama tutaweza kufuta ruzuku kwa vyama vya siasa ndio mwisho wa upinzani kwani misaada ya kutoka ulaya kwa vyama vya upinzani umekuwa kiduchu kwani nao pia wameshituka kwamba fedha zao zinawanufaisha baadhi ya viongozi tu ambao pia wamekuwa viongozi wa kudumu kwenye vyama vyao. Katiba mpya iondoe ruzuku kwenye vyama vya siasa
 
Unasema Maalim ni Mwenye Msimamo?

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni ule ule lakini

1964-1987 alikuwa Muumini wa Serikal mbili

1987-1995 alikuwa Muumini wa Muungano wa 'Nkataba'
1995- 2015 alikuwa Muumini wa Muungano wa Serikal tatu

2015- to date ni Muumini wa Muungano wa Nkataba

Kabla ya kutimuliwa CCM 1987 alikuwa ni Muumini wa Mapinduzi Matukufu ya 1964

Alipotimuliwa Yale MapinduZi yakawa Haramu

Alivyoingizwa kwny Serikal ya Umoja wa Kitaifa 2010 yakawa Matukufu na akawa anahudhuria kila Mwaka kwny Maadhimisho

Alipotoswa 2015 baada ya Uchaguzi Yale MapinduZi yamerudi kuwa Haramu
Mkuu mbona unashindwa kureason kma mtu anayejielewa mwenye elimu walahuvya darasa la saba???
Misimamo maana yake ni kung'ang'ania kitu kimoja miaka 50??? Yaani ulitaka msimamo wake wa 1964 ausimamie hadi leo?? Mazingira hayabadiliki?? Kwa hyo nyerere akiefuta vyama vingi na baadae kuviruhusu naye alikuwa hana misimamo?? Kwa hyo kuanzisha ujamaa na baadae nchi kuwa ya sio ya kijamaa nako kunamfanya nyerere kutokuwa na misimamo???

Mkuu kigezo kimoja cha uongozi ni kuwa flexible kwa mabadiliko ya mazingira na mfumo wa sehemu uliopo mfano husemi sitiation ilikuwaje alipokuwa anasupport serikali mbili?? Huelezi katiba ilikuwaje,hali ya kisiasa ilikuwaje zanzibar,huelezi kero za muungano zilikuwaje afu unataka mtu asibadilishe mtazamo??

Msimamo kwa mawazo yangu ni kusimamia kile unachokiamini kwa nguvu zote sema usilinganishe na mtazamo....... mtazamo utabadilika ila msimamo haubadilikagi yye hapo anataka zanzibar iheshimiwe ndani ya muungano whether serikali ziwe tatu mbili au 10 ila msimamo wa maalim kwenye maslahi ya zanzibar haujawahi kutetereka??? Na huo ndio msimamo hayo ya idadi ya serikali ni mtazamontu kuendana na mazingira na ndio maana utaskia sheria zinafanyiwa marekebisho sio kwamba hazina msimamo sheria zetu au bunge letu ila wanabadilisha mitazamo kuendana na mazingira yaliyokuwepo.

So usilete uchambuzi eti mwanaume ameoa wanawake tatu ndani ya miaka 5 hivyo hana msimamo bila kuelezea je maisha ya ndoa yalikuwaje?? Sababu ya ndoa kuvunjika ni zipi??je dini inaruhusu?? Yaani leta uchambuzi wa 360 degrees kutuonyesha msimamo wa maalim ukiyumba sio unaleta one side analysis na HALO ERRORS hapa bila bila hoja za maana.

Hyo SUK na sherehe za mapinduzi ni taratibu za kikatiba tu yye maalim bibafsi anatakiwa kuzifuata whether alipenda au hakupenda.... kumbuka wananchi ndio walitaka serikali ya umoja wa kitaifa na ipo kisheria hyo serikali sasa ulitaka akatae kuwa makam wa rais wakati wazenji walitaka?? Au ulitaka asihudhuriw wakati kaamua kuwa serikalini tayari iwehe asihudhurie sherehe ambazo zimezaa serikali ambayo na yye ni makam wake?? Inaingia akilini mkuu??

Eti??
 
Nchi haina upinzani ina walaji tu na kama tutaweza kufuta ruzuku kwa vyama vya siasa ndio mwisho wa upinzani kwani misaada ya kutoka ulaya kwa vyama vya upinzani umekuwa kiduchu kwani nao pia wameshituka kwamba fedha zao zinawanufaisha baadhi ya viongozi tu ambao pia wamekuwa viongozi wa kudumu kwenye vyama vyao. Katiba mpya iondoe ruzuku kwenye vyama vya siasa
Unauhakika na unachokisema?? We chama kma cuf au chadema unafkiri hyo ruzuku wanayopata inatosheleza kila kitu?? Kukodi chopa wakati wa kampeni au hta kujenga ofisi mikoa yote unafkiri kwa hyo ruzuku inatosha??
Mkuu usitoe mawazo kishabiki kma hao viongozi wanapenda pesa unafkiri cuf ingejitoa serikali ya zanzibar?? Seif angekataa kutulizwa na umakam wa rais?? Unajua posho na marupurupu ambayo anayakosa kwa kukataa kuwepo serikalini?? Then ndio aje ahemee ruzuku ya pesa za chama wakati alikuwa na uwezo wa kuvuna zaidi ya hizo kma angekuwa SUK!!
Mkuu badilisha reasonin yako upinzani sio uadui na kma hauna hoha kaa pembeni kuliko kujidhalikisha kwa hoja za kitoto kiasi hiko
 
TAARIFA KUHUSU KIKAO CHA KAMATI YA UTENDAJI YA TAIFA YA THE CIVIC UNITED FRONT(CUF - CHAMA CHA WANANCHI) KILICHOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO OFISI NDOGO YA MAKAO MAKUU YA CUF ILIYOPO VUGA, ZANZIBAR TAREHE 2 FEBRUARI, 2017

Kamati ya Utendaji ya Taifa ya The Civic United front (CUF - Chama Cha Wananchi) imefanya kikao chake cha kawaida katika ofisi ndogo ya makao makuu iliyopo Vuga, mjini Zanzibar tarehe 2/2/2017. Kikao hicho kimeongozwa na Katibu Mkuu wa Chama, Maalim Seif Sharif Hamad, ambaye kwa mujibu wa Katiba ya Chama ndiye Mwenyekiti wa kikao hicho.

Kikao kilihudhuriwa na wajumbe wote halali wa kikao hicho waliopaswa kuhudhuria isipokuwa Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Wanawake CUF (Taifa), Bi. Fatma Kalembo ambaye ni mgonjwa.

Kikao hicho kilipokea na kujadili kwa kina ajenda kadhaa ikiwa ni pamoja na kupitia na kuthibitisha mikhtasari ya vikao vilivyopita na yatokanayo na vikao hivyo, Taarifa ya wizi wa fedha za ruzuku ya Chama, Taarifa rasmi kuhusu uchaguzi mdogo wa Ubunge wa Jimbo la Dimani, Zanzibar na Uchaguzi wa Madiwani katika Kata 20 za Tanzania Bara uliofanyika tarehe 22/2/2017, Taarifa ya hali ya kisiasa nchini, na ajenda kuhusu programu ya ujenzi na uimarishaji wa chama kwa upande wa Tanzania Bara na Zanzibar.

Baada ya mjadala wa kina wa ajenda hizo, Kamati ya Utendaji ya Taifa imefikia maamuzi yafuatayo;

1. Kuhusu wizi wa fedha za ruzuku ya Chama;

Kamati ya Utendaji ya Taifa imeipongeza Bodi ya Wadhamini ya The Civic United front (CUF - Chama Cha Wananchi) kwa hatua ilizozichukua kukabiliana na wizi huo uliofanywa kwa lengo la kukihujumu chama kwa mashirikiano kati ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, Benki ya NMB na mtu anayeitwa Ibrahim Lipumba na genge lake. Kamati ya Utendaji ya Taifa inaunga mkono maamuzi ya Bodi ya Wadhamini ya kuazimia kuchukua hatua za kisheria haraka na kuhakikisha kuwa wahusika wote wa wizi huo wanafikishwa katika vyombo vya sheria.

2. (a) Kuhusu Uchaguzi mdogo wa Ubunge wa Jimbo la Dimani Unguja, Zanzibar:

Kamati ya Utendaji ya Taifa inawapongeza na kutoa shukrani za dhati kwa wananchi wa jimbo la Dimani, wanachama, na viongozi wa CUF wa ngazi mbalimbali kwa kujitolea kwa hali na mali kufanikisha kampeni za uchaguzi wa jimbo la Dimani kwa kiwango cha hali ya juu kulikowafanya CCM kukata tama. CCM walijua wamekataliwa na wananchi wa Dimani na kwa hivyo kuamua kutumia vyombo vya dola kulazimisha ushindi usiokuwepo. Kamati ya Utendaji ya Taifa inawataka wananchi na wanachama wote kutokata tamaa kwani CCM imejiaibisha yenyewe na kudhihirisha kwamba imepoteza mvuto na sasa haina uwezo wa kushinda uchaguzi wowote Zanzibar bila ya kutumia nguvu za vyombo vya dola. Hali ilivyokuwa Dimani imethibitisha tena maamuzi ya Wazanzibari waliyoyafanya kupitia uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 ambapo walikigaragaza vibaya Chama cha Mapinduzi(CCM) hadi wakaona hawana njia zaidi ya kuufuta uchaguzi kwa njia za haramu zisizokubalika na wala kuwa na nguvu za kikatiba na Sheria.

Kamati ya Utendaji ya Taifa inawapongeza na kuwashukuru viongozi wote wa vyama rafiki katika UKAWA wakiwemo Mheshimiwa Edward Lowassa (Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na Waziri Mkuu mstaafu), Mheshimiwa Salum Mwalimu (Naibu Katibu mkuu Chadema - Zanzibar), Mheshimiwa Tundu Lissu, (MB), Mheshimiwa Said Kubenea (MB), Mheshimiwa Janet Fussi, Mheshimiwa Kombo Hamad (NCCR) na viongozi wa vyama vyengine kwa ushirikiano wao katika uchaguzi huu na kushiriki moja kwa moja katika mikutano ya kampeni na mashauriano mbalimbali kufanikisha ushindi wa CUF na wananchi wa Jimbo la Dimani katika uchaguzi huu. Tunapenda kuwahakikishia kuwa CUF, ikiwa ni Taasisi makini na imara, itaendeleza ushirikano huu na kamwe haitayumbishwa na vibaraka wachache wanaotumiwa na Serikali ya CCM kuvunja umoja wa vyama vyetu ambao umekuwa na manufaa makubwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na ni tishio kwa uhai wa CCM kuendelea kuiongoza Tanzania.

2. (b) kuhusu Uchaguzi wa Kata 20 za Tanzania Bara uliofanyika tarehe 22/1/2017;

Wananchi wameonyesha wazi wazi kuwa wameichoka CCM ambapo mbali na kushinda kata nyingi, idadi ya kura za wapinzani zimeongezeka kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na kwa upande wa CCM kura zimeshuka sana. Hii ni dalili tosha kuwa Watanzania wamechoshwa na CCM na sera zao za kitapeli na zisizotekelezeka. Aidha, uchaguzi umejidhihirisha wazi kuwa vyama vya upinzani makini vina kila sababu ya kuunganisha nguvu ya pamoja ili kuishinda CCM na kuhakikisha kuwa kwa pamoja tunapambana na vibaraka wanaotumiwa na serikali ya CCM kutaka kujinufaisha binafsi na kuacha lengo kuu lenye maslahi mapana ya kufanya MABADILIKO makubwa ya mifumo ya uendeshaji nchi kwa manufaa ya watanzania wote.

3. Kuhusu Taarifa ya Hali ya Kisiasa nchini;

(a) Kamati ya Utendaji ya Taifa imesikitishwa na hali ya kuyumbishwa kwa uchumi wa nchi kunakofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano na kusababisha hali mbaya ya maisha kwa Watanzania kwa kusitisha ajira, kuvuruga mfumo wa biashara na wafanyabiashara, thamani ya dola kupanda na shilingi kuporomoka, kutokuheshimiwa kwa misingi ya demokrasia na chaguzi huru na haki kulikopelekea nchi nyingi za washirika wa maendeleo (wahisani) kusitisha kutoa fedha za kusaidia miradi ya maendeleo katika bajeti kuu ya serikali, kauli za dharau na kejeli zilizotolewa na Rais Magufuli kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera na kitendo cha Serikali ya CCM kuzitumia fedha za rambirambi zilizotolewa na Watanzania na nchi marafiki kinyume na matarajio na namna ilivyokusudiwa.

(b) Kitendo cha Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Magufuli kuhujumu vyama vya upinzani kufanya shughuli zake za kisiasa kwa mujibu wa Katiba za nchi na sheria ya vyama vya siasa nchini, kuwafunga jela wawakilishi wa wananchi kwa hila na njama za kutaka kudhoofisha wapinzani akiwemo Mbunge wa Kilombero, Mheshimiwa Peter Lijualikali, pamoja na kumnyima dhamana Mbunge wa Arusha Mheshimiwa Godbless Lema kwa mashtaka yanayodhaminika kisheria, ukiukwaji wa haki za binaadamu na uminywaji wa haki za kidemokrasia nchini ni jambo linalohitaji kupingwa na kila mpenda amani na maendeleo ya nchi yetu.

4. Kuhusu programmu ya ujenzi na uimarishaji wa chama Tanzania Bara na Zanzibar:

Katika hatua na mikakati ya kuimarisha Chama, Kikao cha Kamati ya Utendaji ya Taifa kimeandaa programu ya ujenzi na uimarishaji wa Chama kwa upande wa Tanzania Bara na Zanzibar. Kamati inawaomba Watanzania kuendelea kukiunga mkono chama cha CUF kukabiliana na changamato zilizopandikizwa kwa lengo la kuhujumu juhudi za ukombozi wa nchi yetu kisiasa, kiuchumi, na kijamii. Kamati inawataka wananchi, wanachama na viongozi wa CUF kushiriki kwa upana katika program hizo za chama ili kuendelea kupata elimu muhimu ya haki za msingi za kila mwananchi na kuhamasika kudai haki sawa kwa wananchi wote ikiwemo madai ya kupata Tume Huru za Uchaguzi nchini kabla ya uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020.

MWISHO:

The Civic United Front (CUF - Chama Cha Wananchi) na viongozi wake kinawahakikishia Watanzania wote kuwa kitaendelea kusimamia maslahi mapana ya Taifa letu na kushinda changamoto za kupandikizwa zenye lengo la kutaka kukihujumu Chama na mfumo wa demokrasia nchini. Kamati ya Utendaji ya Taifa inawahakikishia wanachama na Watanzania wote kuwa CUF ni taasisi yenye viongozi imara na makini, tunajua na ndivyo ilivyo kuwa hakika itashinda mapambano haya ya ndani na nje ya Chama na itaibuka ikiwa CUF imara zaidi na CUF yenye nguvu zaidi.

HAKI SAWA KWA WOTE

Imetolewa na:

Kamati ya Utendaji ya Taifa
The Civic United Front (CUF-Chama Cha Wananchi)

Joran Lwehabura Bashange
K/Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara
na Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi CUF-Taifa
Tarehe 3 Februari, 2017
Seif usitudanganye bwana,kamati yako hiyo haitambuliwi na msajili wa vyama.Kwahiyo kikao na maazimio yenu ni porojo tupu !
 
Mkuu mbona unashindwa kureason kma mtu anayejielewa mwenye elimu walahuvya darasa la saba???
Misimamo maana yake ni kung'ang'ania kitu kimoja miaka 50??? Yaani ulitaka msimamo wake wa 1964 ausimamie hadi leo?? Mazingira hayabadiliki?? Kwa hyo nyerere akiefuta vyama vingi na baadae kuviruhusu naye alikuwa hana misimamo?? Kwa hyo kuanzisha ujamaa na baadae nchi kuwa ya sio ya kijamaa nako kunamfanya nyerere kutokuwa na misimamo???

Mkuu kigezo kimoja cha uongozi ni kuwa flexible kwa mabadiliko ya mazingira na mfumo wa sehemu uliopo mfano husemi sitiation ilikuwaje alipokuwa anasupport serikali mbili?? Huelezi katiba ilikuwaje,hali ya kisiasa ilikuwaje zanzibar,huelezi kero za muungano zilikuwaje afu unataka mtu asibadilishe mtazamo??

Msimamo kwa mawazo yangu ni kusimamia kile unachokiamini kwa nguvu zote sema usilinganishe na mtazamo....... mtazamo utabadilika ila msimamo haubadilikagi yye hapo anataka zanzibar iheshimiwe ndani ya muungano whether serikali ziwe tatu mbili au 10 ila msimamo wa maalim kwenye maslahi ya zanzibar haujawahi kutetereka??? Na huo ndio msimamo hayo ya idadi ya serikali ni mtazamontu kuendana na mazingira na ndio maana utaskia sheria zinafanyiwa marekebisho sio kwamba hazina msimamo sheria zetu au bunge letu ila wanabadilisha mitazamo kuendana na mazingira yaliyokuwepo.

So usilete uchambuzi eti mwanaume ameoa wanawake tatu ndani ya miaka 5 hivyo hana msimamo bila kuelezea je maisha ya ndoa yalikuwaje?? Sababu ya ndoa kuvunjika ni zipi??je dini inaruhusu?? Yaani leta uchambuzi wa 360 degrees kutuonyesha msimamo wa maalim ukiyumba sio unaleta one side analysis na HALO ERRORS hapa bila bila hoja za maana.

Hyo SUK na sherehe za mapinduzi ni taratibu za kikatiba tu yye maalim bibafsi anatakiwa kuzifuata whether alipenda au hakupenda.... kumbuka wananchi ndio walitaka serikali ya umoja wa kitaifa na ipo kisheria hyo serikali sasa ulitaka akatae kuwa makam wa rais wakati wazenji walitaka?? Au ulitaka asihudhuriw wakati kaamua kuwa serikalini tayari iwehe asihudhurie sherehe ambazo zimezaa serikali ambayo na yye ni makam wake?? Inaingia akilini mkuu??

Eti??

Ngoja nikupe Mifano machache ya Watu Wenye Misimamo!

Mohamed Mursi aliekuwa Rais wa Kidemokrasia wa Egypt Huyu alisimamia Msimamo wake na Chama chake cha Uslamic Brotherhood wa tangu 1922 wa kutoitambua Israel na kufuata Misingi ya Kiislam na hata alipoingia Madarakani hakusaliti wenzie hata alipotakiwa na Madola Makubwa Pamoja na Vitisho vya kupinduliwa na akapinduliwa na sasa yupo Gerezani anasubiri hukumu ya Kifo lakin hajabadili Msimamo bila ya kujali sisi huo Msimamo tunakubaliana nao au laa lakin kwa kuwa ndio Msimamo wake basi hajabadilika.

Donald Trump Huyu hataki Waislam, Waarabu, Weusi na waamerica wengine haijalishi anaungwa Mkono au laa lakin kwa kuwa ndio Msimamo alioombea kura kabaki nao hivyo hivyo.

Yasser Arafat; Huyu alitambua Dola ya Palestina ni lazima Mji Mkuu ni Jerusalem Mashariki na hakubadili Msimamo huo wakati Chama chake cha Fatah kikitambulika Kama cha Kigaid na Isarel na hata walipomfuta kwny orodha ya Magaidi hakubadili Msimamo

Nelson Mandela alitambua kuwa Utawala wa Makaburu si Halali na hakuwahi kubadili Msimamo huu akiwa Kwny Mapambano, akiwa Gerezani na hata alipotoka Gerezani alipopata Madaraka na hata alipostaafu hakubadili Msimamo lakini Huyu Wa Kwenu Akiwa kwny Fursa kidogo nae anaimba Mapinduzi Matukufu na anaamuru Wafuasi wake washiriki Sherehe zote na Mbwembwe zote za Mapinduzi lakini akitoka kwny Fursa ya Madaraka a narudi kuhubiri kuwa MapinduZi Yale yaliondosha Serikali Halali ya Mohamed Shamte!

Msome Oscar Kambona Huyu alitambua Azimio la Arusha halifai na halifai akiwa Rafiki na Waziri wa Nyerere na Mpaka yupo Ukimbizini mpaka anafariki Ughaibuni 1997 bado aliamini na alisimamia anachokiamini na huo ndio msimamo

Sheikh Ponda Issa Ponda yeye Huwa anaamini CCM haifai kuongoza Nchi bila ya kujali Rais wa Nchi ni Wa dini yake au kinyume chake.

Hamis Mgeja Huyu Tangu 1995 aliamini Lowassa anafaa kuwa Rais na tangu Wakati huo bila ya kujali kapata au hajapata yeye
Kasimamia Msimamo wake na hata ilipobidi aachie Madaraka yake ya Uenykt wa CCM Mkoa alikubali kuachia kusimamia kile anachokiamini kuwa Lowassa anafaa kuwa Rais na anampigania mpaka Leo na hata kwny Kashfa ya Richmondi tofauti na Wengine wengi yeye tangu Wakati huo anaamini Lowassa hahusiki na mpaka Leo kabaki na Msimamo huo

Tukio limekwisha tokea 1964 lakin Leo unasema lilikuwa Tukufu na kesho unarudisha tafsiri Mpya kwa Tukio lile lile kuwa lilikuwa haramu na Misimamo yako kutegemea Fursa uliyonayo Wakati huo sio Tukio lenyewe halafu eti huo unaitwa Msimamo usioyumba!

Hakuna Binadamu Mwenye Sifa mbili kwa Wakati mmoja!

1) Kuwa na Msimamo usioyumba

2) Kuwa Flexible kutokana na flexibility ya mazingira

Huwezi kumsifia Sultani Seif kwa kuwa Flexible kutokana na Mazingira na hapo hapo ukamsifia kwa kuwa na Msimamo usioyumba!
 
Huyu Maalim ni kama taahira Fulani hivi! Eti ccm imeshinda kwa nguvu ya dola jimbo la Dimani! Hivi anajua hilo jimbo miaka yote ni la chama gani? Je anaweza kuweka matokeo hapa ili tuone tofauti ya kura na tujue wamepishana kwa kiwango gani? Aache usanii huyu mzee, eti anaswali! Anaswali Wakati si mkweli si bora ale kitimoto tujue moja!
 
Ngoja nikupe Mifano machache ya Watu Wenye Misimamo!

Mohamed Mursi aliekuwa Rais wa Kidemokrasia wa Egypt Huyu alisimamia Msimamo wake na Chama chake cha Uslamic Brotherhood wa tangu 1922 wa kutoitambua Israel na kufuata Misingi ya Kiislam na hata alipoingia Madarakani hakusaliti wenzie hata alipotakiwa na Madola Makubwa Pamoja na Vitisho vya kupinduliwa na akapinduliwa na sasa yupo Gerezani anasubiri hukumu ya Kifo lakin hajabadili Msimamo bila ya kujali sisi huo Msimamo tunakubaliana nao au laa lakin kwa kuwa ndio Msimamo wake basi hajabadilika.

Donald Trump Huyu hataki Waislam, Waarabu, Weusi na waamerica wengine haijalishi anaungwa Mkono au laa lakin kwa kuwa ndio Msimamo alioombea kura kabaki nao hivyo hivyo.

Yasser Arafat; Huyu alitambua Dola ya Palestina ni lazima Mji Mkuu ni Jerusalem Mashariki na hakubadili Msimamo huo wakati Chama chake cha Fatah kikitambulika Kama cha Kigaid na Isarel na hata walipomfuta kwny orodha ya Magaidi hakubadili Msimamo

Nelson Mandela alitambua kuwa Utawala wa Makaburu si Halali na hakuwahi kubadili Msimamo huu akiwa Kwny Mapambano, akiwa Gerezani na hata alipotoka Gerezani alipopata Madaraka na hata alipostaafu hakubadili Msimamo lakini Huyu Wa Kwenu Akiwa kwny Fursa kidogo nae anaimba Mapinduzi Matukufu na anaamuru Wafuasi wake washiriki Sherehe zote na Mbwembwe zote za Mapinduzi lakini akitoka kwny Fursa ya Madaraka a narudi kuhubiri kuwa MapinduZi Yale yaliondosha Serikali Halali ya Mohamed Shamte!

Msome Oscar Kambona Huyu alitambua Azimio la Arusha halifai na halifai akiwa Rafiki na Waziri wa Nyerere na Mpaka yupo Ukimbizini mpaka anafariki Ughaibuni 1997 bado aliamini na alisimamia anachokiamini na huo ndio msimamo

Sheikh Ponda Issa Ponda yeye Huwa anaamini CCM haifai kuongoza Nchi bila ya kujali Rais wa Nchi ni Wa dini yake au kinyume chake.

Hamis Mgeja Huyu Tangu 1995 aliamini Lowassa anafaa kuwa Rais na tangu Wakati huo bila ya kujali kapata au hajapata yeye
Kasimamia Msimamo wake na hata ilipobidi aachie Madaraka yake ya Uenykt wa CCM Mkoa alikubali kuachia kusimamia kile anachokiamini kuwa Lowassa anafaa kuwa Rais na anampigania mpaka Leo na hata kwny Kashfa ya Richmondi tofauti na Wengine wengi yeye tangu Wakati huo anaamini Lowassa hahusiki na mpaka Leo kabaki na Msimamo huo

Tukio limekwisha tokea 1964 lakin Leo unasema lilikuwa Tukufu na kesho unarudisha tafsiri Mpya kwa Tukio lile lile kuwa lilikuwa haramu na Misimamo yako kutegemea Fursa uliyonayo Wakati huo sio Tukio lenyewe halafu eti huo unaitwa Msimamo usioyumba!

Hakuna Binadamu Mwenye Sifa mbili kwa Wakati mmoja!

1) Kuwa na Msimamo usioyumba

2) Kuwa Flexible kutokana na flexibility ya mazingira

Huwezi kumsifia Sultani Seif kwa kuwa Flexible kutokana na Mazingira na hapo hapo ukamsifia kwa kuwa na Msimamo usioyumba!

Mbona hatuelewani vitu vidogo ushasema msimamo wa trump ni kuwa hataki waislam kwa hyo kuwakataza wasiingie siku tisini sio milele ila siku tisini tu je ina maana amekosa msimamo wake juu ya waislam?

Nshakwambia seif msimamo wake ni zanzibar HURU iheshimiwe kwenye muungano haya ni wapi seif ameridhia tanganyika iendelee kuiburuza zanzibar??? Seif bado ana msimamo ule ule wa zanzibar huru shida wwe unaangalia idadi ya serikali anazopendekeza sio msimamo wake.

Mapinduzi cuf wanayatambua shida ni kwend akwenye sherehe tu si ndio?? Alienda mara zile kwa sababu alikuwa ameridhika na uendesheaji wa serikali ssa leo hii kuna mkwamo wa kissiasa na dhulma afuate nni kwenye sherehe hizo?? Ila kesho wakipata muafaka ataenda kwenye sherehe ila kimsimamo CUF wanatambua mapinduzi ya 1964 shida ni kusherehekea ssa kma wwe unafkiri kusherekea tu kwa kupiga mizinga ndio kuenzi mapinduzi basi utamuona maalim ni mjinga kutokwenda kwenye sherehe zile.

FLEXIBILITY NA MSIMAMO VIPO mfano msimamo wa SEIF NI ZANZIBAR HURU ila jinsi ya kuifikia zanzibar huru inahitaji FLEXIBILITY YA MAZINGIRA....... msimamo unahitajila kwenye LENGO ila flexibility inahitajika kwenye PROCESS mfano kwa seif ni kuwa LENGO lake ni zanzibar huru na huo ndio msimamo ulipo ila jinsi ya kufikia zanzibar huru kuna PROCESS na ndio imehitaji flexibility kuendana na mazingira ndio maana anaweza support serikali za idadi tofauti kutokana na mazingira yalivyo na hali ya kisiasa but MSIMAMO upo kwenye LENGO ambalo ndio ZANZIBAR HURU unaielewa mkuu.

Hao kina mandela pia wanamisimamo sema kwenye process walikuwa flexible mfano alianzisha tu mikutano na kupinga ukaburu kwa sera na hoja kiamani zaidi ila baadae akabadilisha ikawa ya RADICAL na akaishia kuanzisha umkhonto we sizwe ambapo ilikuwa ya KIMAPIGANO ZAIDI baadae alipotoka tena mbona hakutaka watumie VITA kumtoa kaburu??? Hapo huoni mandela alikuwa flexible kuendana na mazingira??? Alipoona makaburu hawataki kuachia madaraka kwa amani na yye akaanza kupambana nao kwa mtutu.......then later akakataa mtutu tena sasa unataka kusema mandela naye hana msimamo??

Kwa muktanda huu mandela alikuwa na LENGO la kumtoa kaburu na hapo ndipo msimamo ulipo sema kwenye PROCESS ya kumtoa kaburu alikuwa flexible ndio maana akabadilisha kutoka kuwa mtu wa amani hadi kuanzisha kikundi cha kigaidi sasa tukirudi kwa maalim kwa mfano huu huoni msimamo wake bado upo kwenye lengo la kudai zanzibar huru ila kwenye process ndip anakuwa flexible kwa kubadili mbini za kuifikia zanzibar huru ikiwemo kudai serikali za idadi tofauti????

Emu Tuanzie hapo
 
Huo Msimamo wa Zanzibar huru aliukataa kwenye Kikao muhimu zaid kwny History ya Zanzibar Jan,1984 Tena akiwa against Rais wa Znz au Kumsaliti Mzee Jumbe ndio Msimamo unazungumzia?
 
Huo Msimamo wa Zanzibar huru aliukataa kwenye Kikao muhimu zaid kwny History ya Zanzibar Jan,1984 Tena akiwa against Rais wa Znz au Kumsaliti Mzee Jumbe ndio Msimamo unazungumzia?
Wekeni hansard hapa sio maneno ya kwenye khanga tu hamjawahi kuyathibitisha inakera kwa kweli...... kwa hyo unataka kusema maalim alikataa zanzibar huru akataka iendelee kuburuzwa na muungano ambao tanganyika ndio amevaa hilo koti??

Asee ukiniwekea hapa hansard ya kikao ndio ntaamini maalim ni mnafki.
 
Back
Top Bottom