Taarifa kamili kuhusu adhabu ya Dk. Mwaka na wenzake hii hapa kuhusu tiba mbadala na dawa asili

Nakubaliana nawe mkuu lakini hapa tatizo ni elimu! Elimu tunayohitaji haitolewi na Dr. Mwaka bali inapaswa kutolewa na serikali na kwa vile haikuitoa hivyo kututumbukiza kwenye lindi hili la ujinga, sidhani kama kumzuia huyu Mwaka itasaidia bali msaada ilikuwa ni kumguide ili kuwapunguza hawa wahanga wa ujinga wetu!
Ni kweli kabisa ndugu.
 
Mimi nimesoma kidogo na naishi maisha ambayo huwezi kuyaita duni (japo sio bora), nikiugua magonjwa yasiyoeleweka kama kuhisi malaria option yangu ya kwanza huwa ni herbs (mitishamba) na huwa zinanisaidia sana. Sana sana hospitali nakwenda kupima tu na pale daktari anapoona malaria ndio naweza kutumia vidonge huku vikenda simultaneously na mitishamba.
Sio busara kuwakatisha tamaa walioamua kuventure katika mitishamba maana hata makampuni makubwa kama Colgate yanahamia kwenye herbal na hata Glaxo wana dawa nyingi sasa za herbal.
Ku-extract herbal ili kiwe kidonge au syrup na kuifanyia package hiyo juice isichache ndipo penye tatizo, organic chemistry kidato cha sita nilipata zero, huyo Mwaka hata kidato cha pili kama walivyo waganga wengine hana, teknolojia ya kukamua majani ya alovera na kutoa dawa anaweza?
 
Mwaka form six kamaliza
 
kama sharia hii inayotumika ilianza 2002 mbona haya matamko na makatazo hatukuyaona pale Mchungaji mstaafu wa Loliondo akitoa kikombe ?
huyu amesababisha vifo kwa matangazo ambayo yaliwafanya wagonjwa wakimbie vitanda hospital lakini hili baraza halikusikika
bado hatujaona sababu za msingi za kufutwa huduma za kina JUMA ...
hatuja ona mahali ambapo walitangaza kumpa onyo au kutoa ufafanuzi
kuna chuki binafsi ...hatupendi maendeleo ya watu hasa watu fulani kuwa juu ya wateule ....ambao ndio wanatakiwa wawe maaruf peke yao
 
Safi sana ,hasa huyo Fadhili na Mwaka walizidi kwa kweli eti wanapose na vitabu vya morden medicine kabisa,yaani nimefurahi mpaka basi kufungiwa kwa hawa kunguni
 
MI NAONA WANGEONYWA KWANZA NA SIO KUTOA KUTOA KARIPIO KALI NAMNA HII
Logically, hakuna sababu yoyote ya kuruhusu tiba za aina hii kuwa sehemu ya tiba rasmi ktk nchi. Hawa walishakuwa na kilema cha kutosikia na ukiwaangalia usoni, walishaona wateja wao ni mabwege tu. Hawajali hata aina ya matangazo yao.

Kuna mtu amedokeza kidogo jambo ambalo nimelisikia. Wanaongeza nguvu za kiume kwa kusaga viagra na kuweka kwenye magome ya miti! Watu kama hawa wanaweza sababisha vifo vya watu kwa utapeli tu!
 
Safi sana ,hasa huyo Fadhili na Mwaka walizidi kwa kweli eti wanapose na vitabu vya morden medicine kabisa,yaani nimefurahi mpaka basi kufungiwa kwa hawa kunguni
Hili ndo tatizo kwao. Hawa ni wenye elimu ya asili, sasa wanajidai kurubuni wagonjwa kwa kuweka vitabu vya watu walioenda shule za maana. Ni vizuri kama wataendelea kujitangaza kwa kutumia ndoto zao au urithi wa madawa ya babu zao badala ya kutumia biolojia ambayo pia wanaikosea na kuzungumza yasiyoeleweka.

Lakini, ni kwa nini wateja wakubwa wako ktk miji? Vijijini tunawezasema ni elimu ndogo na uchache wa hospitali, Hapo dar kuna nini? hapo Mwanza, morogoro, arusha, nk. kuna nini? mbona ignorance inakuwa kubwa mijini?
 
kama sharia hii inayotumika ilianza 2002 mbona haya matamko na makatazo hatukuyaona pale Mchungaji mstaafu wa Loliondo akitoa kikombe ?
huyu amesababisha vifo kwa matangazo ambayo yaliwafanya wagonjwa wakimbie vitanda hospital lakini hili baraza halikusikika
bado hatujaona sababu za msingi za kufutwa huduma za kina JUMA ...
hatuja ona mahali ambapo walitangaza kumpa onyo au kutoa ufafanuzi
kuna chuki binafsi ...hatupendi maendeleo ya watu hasa watu fulani kuwa juu ya wateule ....ambao ndio wanatakiwa wawe maaruf peke yao
Naomba nikuulize kwa moyo wote, tena mweupe. Kwa elimu yako ambayo naamini ni kiwango tosha hadi kufikia kuwa mchangiaji hapa JF. Je, nawe unaamini kabisa hawa ni waganga wanaoisaidia jamii? Leo hii Zaidi ya 90% ya magonjwa yanatibiwa hospitalini, yale yasiyo na tiba yanatangazwa hivyo. Hao wanaojiita waganga hawawezi tibu hayo magonjwa na bado wanajitangaza wanatibu. Mtu anasema anazibua mirija ya uzazi kwa akina mama wakati ni upuuzi. Mtu anasema anatibu ngiri kwa kunywa mizizi michungu wakati ni upuuzi mwingine tu!

Je, unaamini waachwe waendelee kupotosha umma kwa sababu tu ni mafanikio yao? Sekta ya tiba haitaruhusu kitu kama hicho kwa sababu kuchezea tiba ya mwingine kunaweza kuleta matatizo hata kwa asiyehusika. Usipomtibu mgonjwa wa TB, wengine tutaambukizwa, na sisi hatukubali.
 
Back
Top Bottom