Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 7,428
- 9,894
Swamidwa Habidadi ni kutoka Burkina Faso ambaye ni mkulima mwenye mafanikio makubwa. Alianza kilimo akiwa na umri mdogo wa miaka 16 baada ya wazazi wake kufariki dunia, na kwa sasa amejitolea kikamilifu katika shughuli za kilimo kuliko masomo yake.
Aligawa shamba alilorithi kutoka kwa wazazi wake, ambalo lina ukubwa wa hekta 6, na kupanda mazao mbalimbali kama mchele, mahindi, maharage, soya, na matunda. Sehemu nyingine ya shamba lake imetengwa kwa ajili ya kilimo cha mazao ya viwandani. Shamba hili ndiyo tegemeo lake kuu la kipato.
Mwaka huu, Swamidwa amevuna mavuno makubwa ya mazao; magunia 10,000 ya mahindi, magunia 8,000 ya mchele, na magunia 5,000 ya karanga. Pia, ana mifugo mingi ikiwa ni pamoja na ng'ombe zaidi ya 900 na mbuzi 500. Ameajiri jumla ya wafanyakazi 40, ambao ni wanaume 20 na wanawake 20, na ana trekta kwa ajili ya kurahisisha shughuli za kilimo.
Swamidwa pia ni mfanyabiashara aliye na magari kadhaa ya kifahari, yakiwemo BMW 4, Mercedes Benz wagon 2, na Range Rover 3. Anamiliki gari la Vx Hilux na pia amewanunulia wafanyakazi wake pikipiki 40 kwa ajili ya kurahisisha usafiri wao. Amejenga hoteli kubwa tatu katika eneo lake.
Mbali na mafanikio yake ya kilimo, Swamidwa ni mtoaji mkubwa wa misaada kwa jamii yake. Ameleta umeme na maji safi katika eneo analoishi, na kwa ujumla ni mtu muhimu na tegemeo kubwa kwa jamii inayomzunguka. Yeye ni mfano wa mtu mwenye mafanikio makubwa kupitia kilimo na kujitolea kusaidia wengine.