Swali la Siku: Jambo gani uliloambiwa utotoni unalohisi ni Upotoshaji ungehitaji kujua Uhalisia wake?

Utotoni ni kipindi ambacho watoto hupokea taarifa mbalimbali, zikiwemo Potofu na Sahihi, na mara nyingi huziamini hadi ukubwani.

Je, kuna Taarifa yoyote uliyoambiwa utotoni inayokupa shaka sasa, na ungependa kupata Uhalisia wake?
Niliambiwa kuwa Al'khaba ni kaburi la Mtume..
Lakini nilivyofuatilia nikajau kuwa kuna jiwe jeusi ndani
Nataka kujua hilo jiwe lilitoka wapi na lina nguvu gani?
 
Mambo niliyoambiwa utotoni na nikawa nayaamini hapo kabla.

1. Babu yangu (rip) ukimeza mbegu ya chungwa au chenza mti utaota tumboni
2. Ukimuua chura wingu litakufunika lakini nilipo kutakana na vijana wenzangu walikuwa wanawaopoa kwa ndoano baada ya hapo wanawaua na kuwazika wakawa wanatengeneza na misalaba 🤣🤣🤣
3. Mimi na ndugu zangu enzi za utoto tulikuwa tunaamini radi ikimulika ni Mungu alikuwa anatupiga picha na Siku tukienda mbinguni tutazikuta huko 😃😃😃
 
Niliambiwa kinyonga akitaka kuzaa hupenda juu ya mti mrefu halafu hujitupa akipasuka watoto hutoka. Na hapa kuna methali moja ilitungwe ikisema hufa kwa uzazi wake =kinyonga.
Nilikuja kugundua kuwa ule ulikuwa ni uwongo baada ya kumkuta kinyonga akitaga.
 
1.Ukipiga mluzi usiku unaita nyoka
2.Ukitembea usiku huku umegeuza chupi utaona mauzauza na wachawi usiku
3.Ukilalia mgongo makalio juu utaguswa na popobawa.
4.Ni mwiko kuomba chumvi usiku,na ikitokea inabidi uiite dawa ya chakula
5.Kuna fulani unaitwa Myegea/sausage tree eti matunda yake ukichanjia mzakali unakua kulingana na tunda linavokua,so husipojipimia saizi mboo inarefuka mpaka miguuni
6.Kwamba bundi anausishwa na uchawi wakati sio.
7.Kuna jamii ya wadudu weusi wanaitwa sungusungu kwamba ukiona wanaingia kwako,kuna dalili ya kupata wageni
8.Viganja vikiwasha utapokea pesa soon
9.Jogoo akiwika usiku eti anabashiri mikosi ni lazima asubuhi achinjweee
10.Mapaka kulia milio ya ajabuajabu usiku eti ni wachawi kumbe ndo kipindi cha kupandana wako mapenzini/mating season
Aisee mambo ni mengi mno ila la KAKAKUONA/Pangolin eti ukimuua utaandamwa na mikosi maisha yako yote,kumbe lengo ni uhifadhi make ingelikuwa Wachina wasingetoboa make ni bonge chakula ya ghali sana kwao
 
Siku yakwanza kula zabibu nikaambiwa nisile nyingi maana mimi ni mtoto!, ati nikila nyingi nitaota usiku vitu vyakutishatisha!.
Nilikula kidogo tu zilizobaki nikawapa waliokuwa wananitisha!, sasa ukweli nishaujua sasahivi si tu kula zabibu napiga na pombe ya zabibu kufidia uongo wao!!..😅
 
Kubatizwa nikiwa mtoto, ni kwa nini nilitekwa kiimani? Sikuwa na uwezo wa kukataa kwa sababu ya utoto, sasa nimekuwa nikagundua ukristu ni biashara. Tusiwabatize watoto, waache wawe watu wazima ili wachague imani yao.
 
Niliambiwa watu ambao wakisimama wima miguu yao imependa kwa nyuma (chini ya magoti) wanakipaji cha kuona memori Kadi. Niliondoka na uzushi huu baada ya kukuta padre mmoja akiwa na miguu iliyopinda kwa nyuma.
 
Back
Top Bottom