Swali la kukera: CHADEMA kwa sasa inafuata mrengo/itikadi gani?

Hizo tuhuma za ufisadi dhidi ya chenge ni kilio kutoka chadema, lakini akiamua kujiunga hata Leo chadema atashangiliwa na kusafishwa mapema sana.
NNimeuliza nyie CCM mnamuonaje Chenge??? Ni fisadi au mtu safi,na mnawaonaje Tibaijuka,Ngeleja,Masaburi,Kikwete na wenzenu wengine??ni mafisadi au watu safi
 
Wamezidi kukurupuka hawa,wakiona tumekaa kimya wanadhani hatuwezi wajibu,kiuhalisia vijana wa ccm bado watupu sana kutetea wanacho kiamini,na hawawezi leta hoja zenye mashiko,ni kukurupuka tu.. Tumewaachia jukwaa wanashindwa litumia,ngoja turudi
Mkuu si kwamba ni watupu, LA hasha wanajichetua tu kwa sababu ya matumbo yao, siasa zao nizakujipendekeza na huyu mwasisi Wa siasa za INA hii hakika namlaani hata niingia kaburini mzimu wangu utaendelea kulaan hautaacha
 
Wanaendelea kutafuna peza za mamvi, zikiisha watatafuta ajenda nyingine, maana ya ufisadi sasa na wao ni mafisadi zaidi ya papa.
Walimpa moyo kuwa atashinda, kagalagazwa wanasema wanajipanga 2020 wachukue nchi... Wanamtengenezea mazingira ya kujidumbukiza tena ili waendelee kula mkwanja wa mzee wetu..... Kwanini Mbowe hana huruma jamani, wamwabie tu ukweli kuwa mzee pisha tuweke wengine
MBOWE MWONEE HURUMA MZEE WA WATU
 
Someni kwa makini kitabu cha Mzee Mtei, "My Ghost". Chadema inaamini katika ubepari wa Magharibi 100%. Hakuna cha kushoto au kulia na ndio wanafungamana na Republican (USA) na Conservative cha Uingereza ambao ni mabepari waliokubuhu.
 
Sijui una elimu gani,lakini naamini utakuwa mjinga,CHADEMA haijawahi kuwa na Sera za kibepari wala haifuati mlengo wa kibepari,CHADEMA NI MLENGO WA KATI.....sio kushoto wala kulia ni center party...CHADEMA inaamini katika uchumi wa soko huru, na sekta binafsi LAKINI bila kupoka mamlaka ya umma katika maeneo nyeti ya kiuchumi.....sasa we mjinga ubepari hapo upo wapo CHADEMA NI MIXER YA SOCIALISM NA CAPITALISM....Na ndo maana watu binafsi wanaruhusiwa kuendesha uchumi ila kukiwa na usimamizi wa karibu wa serikali,kwa hiyo unavyoleta kitu hapa make sure umesoma sio unakurupuka tu

Safi kabisa wewe msomi. Yaan unaweza hata kumshinda Adam Smith au hata Karl Marx maana umekuja na ''center'' ambayo inaunganisha socialism na capitalism. Mzee nakushauri kadai uprof wako.
 
Unanipangia tena,badala ya kunijibu,acha kuonesha utupu wako
Yanini kutupiana matusi mkuu? Hii ni mijadala ya kisiasa tu. Unakosea sana kuniambia.. ".. Utupu wako.." ila sinaga mazoea ya matusi, Mungu akusaidie ili siku moja usiwe na jazba.
 
Usilete maneno ya kusikia ,Rejea kwenye katiba ya Chadema na uangalie wanavyoishi na kuongoza jamii kama Dar , Mbeya , Iringa , Arusha hapo utajua mlengo wao n UPI. Sio kuleta HISIA NA UKADA HAPA
 
Mkuu si kwamba ni watupu, LA hasha wanajichetua tu kwa sababu ya matumbo yao, siasa zao nizakujipendekeza na huyu mwasisi Wa siasa za INA hii hakika namlaani hata niingia kaburini mzimu wangu utaendelea kulaan hautaacha
Mkuu usikasirike,swali la kukera ni je chadema wanafuata siasa za mrengo gani?..usijenge chuki na binadamu.
 
Ila saiv sio fisadi au mpaka ahamie CHADEMA??
Tatizo lako badala ya kujibu swali wewe unapiga makelele tu.Labda nikufundishe Mzee Mtei alijifungamanisha na Conservative ya Uk ambacho kinaamini katika ubepari...tokea kina Margareth Thatcher,John Mayor na Sasa David Camoron...ikimbukwe Mwl.Nyerere walitofautiana na Thatcher kwa sababu ya siasa za ubaguzi A.Kusini na ndio maana UK waliamisha makampuni yao mengi TZ na Kupeleka Kenya...zikiwamo benki,viwanda na biashara...kwa hivyo tunapouliza tunahitaji kupewa jibu na sio matusi.Je chadema inaamini siasa za itikadi ipi?...pia mkuu nikuulize Mwambigija na wenzake hatma yao vipi?..namkubali sana huyu jamaa.
 
Usilete maneno ya kusikia ,Rejea kwenye katiba ya Chadema na uangalie wanavyoishi na kuongoza jamii kama Dar , Mbeya , Iringa , Arusha hapo utajua mlengo wao n UPI. Sio kuleta HISIA NA UKADA HAPA
Jinsi ulivyoandika tu ni dhahiri hata katiba ya chadema hujawahi kuiona.
 
Wewe huuelewi ubepari nchi kama
Canada
Denmark
Sweden
Holland
Etc elimu,matibabu,ni bure na mataifa ya kibepari
Kwa mujibu wa karl marx ubepari manake ni kugawana utajiri
 
Wewe huuelewi ubepari nchi kama
Canada
Denmark
Sweden
Holland
Etc elimu,matibabu,ni bure na mataifa ya kibepari
Kwa mujibu wa karl marx ubepari manake ni kugawana utajiri
Kwa mujibu wa Mtei ambaye ilifikia hatua ya kuacha uwaziri wa fedha...ilikuwa ni kupinga ugharamiaji wa huduma za kijamii ambayo ndio ilikuwa sera na itikadi ya Mwl.Nyerere...soma vema hoja mkuu.
 
Walimpa moyo kuwa atashinda, kagalagazwa wanasema wanajipanga 2020 wachukue nchi... Wanamtengenezea mazingira ya kujidumbukiza tena ili waendelee kula mkwanja wa mzee wetu..... Kwanini Mbowe hana huruma jamani, wamwabie tu ukweli kuwa mzee pisha tuweke wengine
MBOWE MWONEE HURUMA MZEE WA WATU
Yaah huu ni aina mpya ya unyanyasaji wa haki za binadamu...ipo siku tutauangazia.
 
Back
Top Bottom