Swali kwa CHADEMA: Lowassa aliwaeleza nini hadi mkamkubali?

Lowassa sasa yuko CHADEMA. Ni mwanachama halali. Lowassa amehamia huko akitokea CCM yetu. Iliripotiwa kuwa Lowassa alijieleza mbele ya Kamati Kuu ya CHADEMA kiasi cha kukubaliwa kujiunga nao na baadaye kuwa mgombea wao wa Urais mwaka jana.

Ilielezwa kuwa Lowassa alijieleza vya kutosha juu ya makandokando yake ya ufisadi anaoshutumiwa nao. Ikasemwa kuwa Lowassa alijieleza kwa hatua kuhusu kashfa anazohusishwa nazo,ikiwemo kashfa ya Richmond. Hatimaye akakubaliwa. Akajiunga nao.

Sasa maswali,Lowassa alieleza nini hasa? Alimtaja nani? Alisema kwanini hutajwa yeye? Mlithibitishaje maelezo yake,yaani ukweli wa alichokisema?

Nakala kwa:
Tumaini Makene
freeman mbowe
Ben Saanane
Yericko Nyerere
mpk
Salary Slip na wengineo

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Iringa)

Alimtaja mmiliki halisi wa Richmond,IPTL na ESCROW Account Scandle
 
Back
Top Bottom