Swali Fyatu: Walitaka Rais afanye nini hasa baada ya ripoti ile?

Mi nipo naangalia hatma ya hili sakata
Ila serekari ya ccm imeharibu sana hii nchi.
Sasa inatakiwa kujirekebisha kwani haya yote ni zao la ccm

Walio fanya madudu hayo
ndio hao mnawadekia barabara na kuwazungushia mikono
 
Suluhu? Container zilizokamatwa bandarini ambazo kamati imegundua kuna udanganyifu inataka suluhu? ....Suluhu na wezi? ....Kuwa na Mkataba wowote si room ya kutaka majadiliano hata kwenye uvunjifu wa wazi wa sheria ambao unataka serikali kuchukua hatua mara moja ....
Haya amini unavyoamini. Mi niliyashuhudia ya Bakhresa, Samaki nk. Huwezi kujadili jambo la namna hii bila kuwa na tripartite committee.
 
SWALI FYATU:
Baada ya ripoti ya jana, na yote yaliyosemwa, Rais alikuwa anatakiwa afanye nini? Aunde kamati nyingine kuthibitisha matokeo ya kamati ile; au aanze tena uchunguzi wa kuchunguza alichounda kuchunguzwa? Tuchukulie kwa mfano baada ya ripoti ile iliyojaa "madoido" ya Prof. Mruma, Rais angesema ni ripoti nzuri anawashukuru halafu watu wakaondoka zao bila hatua yoyote kali; kwamba alitaka kujua tu kinachoendelea; ni sauti gani zingepazwa? Siyo kwamba Magufuli angeonekana anambeba tena Muhongo?

Sasa baada ya madudu yote yale kuibuliwa Magufuli kweli alikuwa na kitu kingine cha kufanya? Baadhi yetu tunategemea ataenda mbele zaidi maana japo jana limeripotiwa sana la Muhongo lakini tayari kuna watu wengine wengi wamekwenda na maji na kupoteza nafasi zao na sitoshangaa wengine wakajikuta kizimbani.

Lakini zaidi ni hii kampuni ya ACACIA; majibu yake yamejaa ujanja wa maneno na inapuuzia ukweli ambao wengi wetu tunaujua - Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye ufisadi wa kutisha. Suala la ufisadi Tanzania halijakoma kwenye sekta moja; sekta ya madini ni miongoni mwa sekta ambazo zimeathirika sana na ufisadi. Zipo ripoti nyingi zinazoonesha jinsi makampuni makubwa ya uchimbaji madini yanavyotumia mbinu mbalimbali nyingine za kibabe (bullying tactics) katika kuzibana nchi na serikali zisizokaa kwenye mstari wao.

Namna pekee ya kuelewa uzito wa ripoti hii na hatua za Rais ni kuangalia ufisadi kama sehemu kubwa ya haya yanayotokea. Ni nani ambaye hajui jinsi gani ni rahisi kupenyeza rupia ili kupitisha au kujaza fomu fulani ziseme kile ambacho kitaridhisha macho ya wakubwa fulani?
Binafsi nilitarajia hatua kali zaidi kuliko hizi; ikiwemo kuifungia kampuni ya ACACIA kufanya kazi za uchimbaji madini Tanzania kwa miaka kumi ijayo! Ni lazima tufike mahali tujue kuwa kuna umasikini unaoweza kutokana na mtu kupoteza vitu fulani; lakini umaskini wetu sisi ni wa kuamua kwa hiari na kwa kushirikiana sisi kwa sisi kupoteza mali zetu ili tusiwaudhi wakubwa.
Kama ACACIA inaona imeonewa na haiwezi kufanya kazi Tanzania na kuwa yaliyosemwa yote ni uongo (hii ndio maana ya ripoti yao!) njia pekee ni kuondoka na kuacha madini na michanga yetu! Ili tuishi katika kujidanganya sisi wenyewe.

Wakati umefika tuwe tayari kuwaudhi wakubwa ili angalau watoto wetu waje kufurahi mbeleni. Ndugu zetu wanaotaka tuingiwe na hofu ya kuwa sasa tutakiona cha moto wanasikitisha sana; ina maana wenzetu hawa watakuwa wanapiga magoti kila wakipigwa mikwara na makampuni haya makubwa? Ina maana wenzetu watatuma washenga kwenda kuwabembeleza wasiondoke?

Tumenyonywa kiasi cha kutosha; ni kweli! Lakini itakuwaje kama sisi wenyewe tunalilia tunyonywe tena tunawashikia mirija wakubwa hawa na kuichomeka hata sehemu ambazo hazitajiki ili watunyonye hadi chembe za mwisho za supu ya mifupa yetu?
Una hoja ya msingi.
 
Yaani, wameniudhi sana nilivyosoma. Kimsingi wanasema Taifa zima sisi ni waongo; wao wanachosema ni kweli tu. Na ni kana kwamba wanadai yale ambayo weupe wengi walikuwa wanadai zamani; moral high ground. Kwamba, wenzetu hawa hawawezi kututapeli sisi maskini, kwamba kwa vile wao ni kampuni kubwa basi hawawezi kufanya ufisadi. kana kwamba sisi sote hatujui jinsi makampuni makubwa yanauza hisa NY hadi London yalivyosababisha mgogoro wa kiuchumi sababu ya ufisadi tu mwaka 2008; na yote yalikuwa yanakaguliwa vizuri na kupewa hati 'safi'!
Wanasaidiwa na watu tunaowategemea kuchukua nchi hapo baadae sijui inakuwaje!!!
 
Mababu zetu waliingia mikataba mingi 'mibovu' kwa sababu kubwa mbili ya kwanza
ni kutokujua (ignorance) na ya pili waliwaamini wazungu (bona fide).

Kwetu sisi sababu kubwa siyo ujinga tena - kwani tuna watu wengi wamesoma kama hawa wengine; sababu yetu kubwa ni kutumia nafasi hii kujinufaisha (opportunism) .

Kwa hivyo wao waki declare contents zao kwenye bills of lading au customs au what not sisi tunaamini kwa sababu tunaamini wazungu wanajua zaidi na wanatutakia mema na hivyo hawawezi kutudanganya! Kosa hili la mababu tunalirudia sana.

Sababu nyingine hata hivyo ni kwa sababu tuna woga; huu woga unatokana na mabaki ya athari za fikra za kutawaliwa (colonial legacy's mentality). Tangu kutawaliwa fikra zetu bado hazijafunguliwa vya kutosha kuweza kujiamini.

Kumbe basi, matatizo yetu ya leo yanatokana na sisi wenyewe. Watu wanataka kujinufaisha kwa haraka na kutokana na madaraka yao. Mababu zetu hawakufanya hivyo ili wajinufaishe; walifanya hivyo wakiaminishwa kuwa wanaisaidia jamii yao. Hawa ndugu zetu wanajua kabisa wanachofanya wanachoombea ni kuwa wasijwe kukamatwa.
Katika sababu ulizoeleza wino mwekundu ni sababu halisi. Tuna 'greedy' kwamba kwavile watu wanapata 10% au ni sehemu ya Bodi hakuna anayefikiri nchi.

Mikataba ipo kwa miaka 16 kelele zimepigwa, viongozi walikuwepo. Nini kilitokea?

Pili, ignorance unayosema ni kweli. Hoja zikiletwa bungweni na hasa na wapinzani, viongozi walioko leo walitumia Bunge kuzifinyanga. Sababu ni greedy ingawa leo wanaonekana tofauti

Ni kiongozi gani katika waliopo aliyekuwa hayupo serikalini miaka 16 iliyopita?
Je, hakuna aliyeona uozo huo hadi taarifa ya Jana?

Tusiwalumu wazungu sisi ndio tatizo wala siyo ignorance.
Kilichopo ni ujinga, ubinafsi na woga.Watu wanaogopa nafasi zao badala ya masilahi ya Taifa.

Hatua za jana ni nzuri, lakini je, zimezingatia hali iliyopo?
Tunakumbuka mikataba tuliyopeleka mahakamani na kushindwa?
Kwanini tumeshindwa kuvunja mkataba wa IPTL?

Watakokwenda mahakamani ni wale waliohusika na mikataba miaka 16 iliyopita. Tutashindwa

Muhimu ni hatua za dharura, kisha hatua za muda mrefu ambazo ni kuwaweka wazi wote waliohusika kutufikisha hapa miaka 16 iliyopita

Hoja hiyo inaji 'defeat' na ukweli kuwa wanajuana,ni waoga, greedy ni mwongozo.

Hawataweza kuwachukulia hatua kwasababu ya woga uliosema na ubinafsi
 
Hao watu wajanja sana na wataalamu wa kucheza na maneno. Mimi nadhani na sisi tuanze kujitambua, hii ya kuandika mikataba kizungu tukatae...wao si ndiyo wafanya biashara, basi lugha yetu ndiyo iwe base wakitafsiri kikwao tunasema hatukumaanisha hicho...Hii ndiyo janja yao...Ukisoma hii claim yao unaona wameanza kuchomekea misamiati ya kijanja kutafuta pa kutorokea...

Mkuu;
Lugha iliyotumika hapo ndiyo lugha utakayoenda kuitumia kule mahakama ya biashara. Hata wale wavietnam ndiyo hiyo waiitumia lakini bado wakatubwaga na masamaki yetu wenyewe.
Kitu hapa ni kuwa, Chunguza kila aliyehusika wa hapa nyumbani mfano; Uliteuliwa kwenda kuusoma mkataba tarehe 12/4/2002. Uliporudi kutoka huko, ghafla maisha yako yakabadilika. Umenunua kagari, umejenga kanyumba Kigamboni, ukajenga kengine Kijichi na kengine tena hukooo. Ukabadili kale kagari, ukanunua Prado, ukabadili hotel ya kula mchana ukaenda kula skyways. Bado mambo zako ni za hali ya juu tu. Lazima ukamatwe, ufilisiwe, utupwe Segerea ueleze ulikoipata tangu buku ya kwanza hadi leo una milioni 100 bank. nadhani kwa jinsi hii, tutawafanya wengine kina joka la makengeza macho yao yapone.
Ndipo tuyadhibiti hayo makampuni na mengine yoote yajayo. Wadhani wanaotumwa kwenda kusaini hawaijui lugha au hawaisomi tu baada ya kuweka mfukoni chao. Yale mafweza ya uswiss yako wapi?? Kimyaaaaa. I wish I kuldu be a president wallah. Mngeuona moto wa jehanam ukiwachoma hapa hapa tz.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Off topic:
96% ya wafanyakazi wa hii migodi ni watanzania, miaka takribani 18 tulishindwa ku plant watu wetu wa usalama wenye elimu ya miamba kupiga ushushushu.
Nafikiri hapakuwa na "political will" . Nafikiri walioingia hii mikataba mibovu walijua exactly nini wanafanya.
 
Off topic:
96% ya wafanyakazi wa hii migodi ni watanzania, miaka takribani 18 tulishindwa ku plant watu wetu wa usalama wenye elimu ya miamba kupiga ushushushu.
Kabla hata ya kuhangaika ku plant mashushushu (Ingawa lazima walikuwepo) hii mikataba mibovu iliingiwa na hawa hawa Watanzania.
 
Wazo zuri na la kizalendo, lakini je MKATABA TULIOSAINI NAO UNASEMAJE?

Unafikiri kwa maneno matupu watavunja huo mkataba na kwa hasira waondoke?, kuna legal battles we have to fight!
Mkuu huu ni wizi na haumo katika mkataba.

Mkataba hauna kipengele kinachosema "Thou shall steal minerals from Tanzania if you can"

Kampuni inasema (mfano) 'nasafirisha mchanga huu wenye kilo 1 ya dhahabu' kumbe una kilo 10. Huu ni wizi, period. Na wamekuwa wakifanya hivi siku zote.

SULUHU
1. ACCACIA wapewe mchanga wao lakini wailipe serikali kulingana na viwango vya madini vilivyoonwa na tume.

2. Serikali iweke wataalam huru kupima kiasi cha madini iliomo kwenye makanikia yanayosafirishwa kwa kipindi cha mwaka mmoja.

3. Wastani wa vipimo hivi vichukuliwe kuwa ndio viwango vya madini kwenye haya makanikia tangu kampuni ianze kusafirisha mchanga.

4. Kampuni iifidie Serikali tofauti ya walochokuwa wanalipa hapo nyuma na ambacho wangelipa kufuatia wastani mpya uliopatikana katika hatua ya 2 na 3.
 
Aagh nimechoka kusoma comment za watu waoga na wasiojiamini, Magu sio mjinga aliyaona yote hayo watu waoga wanayoyasema, na ndio maana kaunda kamati mbili, moja imemaliza, tuisubili ile ya wanasheria ndio tutachonga vizuri sasa.

Kwa sababu watu waoga wanachokijadili hapa, ni cha kisheria ambacho bado ripoti yake haijatoka.

Kamati ya Mruma imeeleza kinaga ubaga aina za madini zilizokutwa kwenye mchanga unaozuiliwa bandarini, na kwenye document zilizoonyeshwa ni aina tatu tu,

Pili kamati imeonyesha kiwango kilichopatikana kutokana na sampuli zilizochukuliwa kutoka kwenye hayo makontena ambacho ni tofauti na kile kilichoonyeshwa kwenye document.

Tatu kamati imepima uzito halisi wa container na kukuta tofauti na ulioonyeshwa kwenye document.

Katika akili tu za kawaida hata kama haujaenda shule hapo hauoni haya makampuni ya madini yalivyokuwa yanatuibia.?

Niachie hapo tutafute kwenye sheria ya kodi ndio mtamjua Mzee Mwanakijiji anachoomanisha.

kiukweli ACACIA wanatapatapa, na hawaoni pa kutokea.
 
Mkuu huu ni wizi na haumo katika mkataba.

Mkataba hauna kipengele kinachosema "Thou shall steal minerals from Tanzania if you can"

Kampuni inasema (mfano) 'nasafirisha mchanga huu wenye kilo 1 ya dhahabu' kumbe una kilo 10. Huu ni wizi, period. Na wamekuwa wakifanya hivi siku zote.

Wao lab wanayopeleka kupima mchanga imesema ina kiwango A, B, C

Na sisi lab ya tume yetu imeleta majibu kuwa kuna kiwango X, Y, Z

Unless uwe na ushahidi kuwa Lab yao ilileta results kama za tume yetu kisha Wakazibadiri kimagumashi ili kutudanganya then hapo unapoint.

Otherwise Neutral Lab ikutanishe wataalam wa pande mbili then wafanye analysis kwa pamoja na kwa uwazi Waone nani yuko more authentic!, then hapo ndo tutapata basis ya maamuzi bora ya kuchukulia hatua na maamuzi mengine mbeleni!
 
Kwahiyo mzee Mwanakijiji tuwasemehe waliotufikisha hapa.
Kwanini tuwasamehe; tulipopewa nafasi ya kuwabadilisha tukawachagua hao hao! badala ya kutaka wao tu wabadilike labda na sisi inabidi tuangalie kwanini tumebadilika.
 
Wao lab wanayopeleka kupima mchanga imesema ina kiwango A, B, C

Na sisi lab ya tume yetu imeleta majibu kuwa kuna kiwango X, Y, Z

Unless uwe na ushahidi kuwa Lab yao ilileta results kama za tune yetu kisha Wakazibadiri kimagumashi ili kutudanganya then hapo unapoint. Otherwise Neutral Lab ikutanishe wataalam wa pande mbili then wafanye analysis kwa pamoja na kwa uwazi Waone nani yuko more authentic!, then hapo ndo tutapata basis ya maamuzi bora ya kuchukulia hatua!

Na hiyo neutral lab; ikionesha kile kilichooneshwa na Kamati ya Mruma; tutafute lab nyingine ndugu yangu kuthibitisha ni nini kimeonekana?
 
CCM mna vituko mnajitekenya na kucheka wenyewe,leo unazungumzia ufisadi uliosababisha na nyie wenyewe....by the way kwa nini Magufuli asiwafukuze tu hao majamaa?? kama rispoti imebaini bayana kuwa wameshiriki kwenye wizi Magufuli atoe maamuzi awafukuze
Kwa kweli kwa ile hotuba yake ya jana ingekuwa vema kama ACACIA wangefukuzwa tu atuachie mashimo yetu matupu. Tatizo ni kwamba utashi wa kisiasa una mipaka ya kisheria na ndo maana hotuba ilipaswa kuwa ya jiutendahi zaidi badala ya kuwa kama hukumu fulani. Kama ni kweli wameiba na ushahidi upo, mahakama ni raisi na ni vema awafukuze tu!
 
Na hiyo neutral lab; ikionesha kile kilichooneshwa na Kamati ya Mruma; tutafute lab nyingine ndugu yangu kuthibitisha ni nini kimeonekana?

Kwa sasa tuna matokeo ya chunguzi mbili, ya kwanza ni ile TMAA na hao Barick waliyokuwa wakitumia on their daily basis.

Ya pili ni hii ya Tume, Unless labda kama hawa Barick walikuwa "wanatemper" na Matokeo ya Labs basi kila mmoja ataendelea kushikilia upande wake na msimamo wake, Sasa what will be the way forward kama kesi ikifika kortini?
 
SWALI FYATU:
Baada ya ripoti ya jana, na yote yaliyosemwa, Rais alikuwa anatakiwa afanye nini? Aunde kamati nyingine kuthibitisha matokeo ya kamati ile; au aanze tena uchunguzi wa kuchunguza alichounda kuchunguzwa? Tuchukulie kwa mfano baada ya ripoti ile iliyojaa "madoido" ya Prof. Mruma, Rais angesema ni ripoti nzuri anawashukuru halafu watu wakaondoka zao bila hatua yoyote kali; kwamba alitaka kujua tu kinachoendelea; ni sauti gani zingepazwa? Siyo kwamba Magufuli angeonekana anambeba tena Muhongo?

Sasa baada ya madudu yote yale kuibuliwa Magufuli kweli alikuwa na kitu kingine cha kufanya? Baadhi yetu tunategemea ataenda mbele zaidi maana japo jana limeripotiwa sana la Muhongo lakini tayari kuna watu wengine wengi wamekwenda na maji na kupoteza nafasi zao na sitoshangaa wengine wakajikuta kizimbani.

Lakini zaidi ni hii kampuni ya ACACIA; majibu yake yamejaa ujanja wa maneno na inapuuzia ukweli ambao wengi wetu tunaujua - Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye ufisadi wa kutisha. Suala la ufisadi Tanzania halijakoma kwenye sekta moja; sekta ya madini ni miongoni mwa sekta ambazo zimeathirika sana na ufisadi. Zipo ripoti nyingi zinazoonesha jinsi makampuni makubwa ya uchimbaji madini yanavyotumia mbinu mbalimbali nyingine za kibabe (bullying tactics) katika kuzibana nchi na serikali zisizokaa kwenye mstari wao.

Namna pekee ya kuelewa uzito wa ripoti hii na hatua za Rais ni kuangalia ufisadi kama sehemu kubwa ya haya yanayotokea. Ni nani ambaye hajui jinsi gani ni rahisi kupenyeza rupia ili kupitisha au kujaza fomu fulani ziseme kile ambacho kitaridhisha macho ya wakubwa fulani?
Binafsi nilitarajia hatua kali zaidi kuliko hizi; ikiwemo kuifungia kampuni ya ACACIA kufanya kazi za uchimbaji madini Tanzania kwa miaka kumi ijayo! Ni lazima tufike mahali tujue kuwa kuna umasikini unaoweza kutokana na mtu kupoteza vitu fulani; lakini umaskini wetu sisi ni wa kuamua kwa hiari na kwa kushirikiana sisi kwa sisi kupoteza mali zetu ili tusiwaudhi wakubwa.
Kama ACACIA inaona imeonewa na haiwezi kufanya kazi Tanzania na kuwa yaliyosemwa yote ni uongo (hii ndio maana ya ripoti yao!) njia pekee ni kuondoka na kuacha madini na michanga yetu! Ili tuishi katika kujidanganya sisi wenyewe.

Wakati umefika tuwe tayari kuwaudhi wakubwa ili angalau watoto wetu waje kufurahi mbeleni. Ndugu zetu wanaotaka tuingiwe na hofu ya kuwa sasa tutakiona cha moto wanasikitisha sana; ina maana wenzetu hawa watakuwa wanapiga magoti kila wakipigwa mikwara na makampuni haya makubwa? Ina maana wenzetu watatuma washenga kwenda kuwabembeleza wasiondoke?

Tumenyonywa kiasi cha kutosha; ni kweli! Lakini itakuwaje kama sisi wenyewe tunalilia tunyonywe tena tunawashikia mirija wakubwa hawa na kuichomeka hata sehemu ambazo hazitajiki ili watunyonye hadi chembe za mwisho za supu ya mifupa yetu?

That's not how it works. Hawa serikali na ACACIA ni two parties in a contract. One party (serikali) is claiming to be defrauded by another party (ACACIA). Serikali ilipaswa kuunda tume huru, isiyohusisha watu wake walioteutliwa na serikali peke yake. Sasa ona jinsi ambavyo ACACIA wanasema hawakubaliani na findings za tume. Kwenye mahakama yeyote iliyo huru findings za hii tume haziwezi kutumika kama ushahidi wa kutolea hukumu kwasababu "bias" ilianzia kwenye uundwaji wenyewe wa hii tume. Findings za hii tume zinaweza kuwa za kweli, lakini ili kuepuka utata wa kisheria na maswali juu ya validity ya hizi findings serikali ilipaswa kuunda tume huru. I would have reacted the same way if I were ACACIA. Now, the government is the one using bullying tactics against ACACIA.
 
Mkuu;
Lugha iliyotumika hapo ndiyo lugha utakayoenda kuitumia kule mahakama ya biashara. Hata wale wavietnam ndiyo hiyo waiitumia lakini bado wakatubwaga na masamaki yetu wenyewe.
Kitu hapa ni kuwa, Chunguza kila aliyehusika wa hapa nyumbani mfano; Uliteuliwa kwenda kuusoma mkataba tarehe 12/4/2002. Uliporudi kutoka huko, ghafla maisha yako yakabadilika. Umenunua kagari, umejenga kanyumba Kigamboni, ukajenga kengine Kijichi na kengine tena hukooo. Ukabadili kale kagari, ukanunua Prado, ukabadili hotel ya kula mchana ukaenda kula skyways. Bado mambo zako ni za hali ya juu tu. Lazima ukamatwe, ufilisiwe, utupwe Segerea ueleze ulikoipata tangu buku ya kwanza hadi leo una milioni 100 bank. nadhani kwa jinsi hii, tutawafanya wengine kina joka la makengeza macho yao yapone.
Ndipo tuyadhibiti hayo makampuni na mengine yoote yajayo. Wadhani wanaotumwa kwenda kusaini hawaijui lugha au hawaisomi tu baada ya kuweka mfukoni chao. Yale mafweza ya uswiss yako wapi?? Kimyaaaaa. I wish I kuldu be a president wallah. Mngeuona moto wa jehanam ukiwachoma hapa hapa tz.

Ndugu yangu pamoja na hao makuwadi wao pia huwa wanajificha huko huko kwenye lugha ya kuazima...Hivi unafikiri waarabu huwa wanaandika kwa lugha ya kizungu mikataba yao? Huu ujinga upo na sisi tu...What is mahakama ya kibiashara by the way kwani lazima uwe signatory? Hivi nchi yetu ikikataa kuingia huko ikaamua kulima mahindi yake na kuyala nani atakaye kuja kugonga hodi kwa mwenzake kama siyo wao? Hizo nchi unazifahamu lakini? Nyingi maji ya bahari tu ndiyo rasilimali zao hata bustani ya miti wanaita forest yet matumizi yao na style yao ya maisha tukinuna tu huku kwenye nchi zetu hakuna hata pumzi ya kuishi wataipata...Ni unyonge wa akili tu na manipulation zao ndizo zinazowafanya kuendelea kujidai vijogoo...Unajua walicho kifanya Doha hao Brazil na alies wake hadi kuwalazimisha kugeuza mchezo wa international trade? Jamani eeh ebu tuendage kusoma shule na siyo kutalii huko ndiyo utafahamu michezo yao ya kidoli wanayotuchezea.

Hapa Africa ikisimama kiume na kuamua kwenda na BRICS watakuja wenyewe kupiga magoti...Tubadile kabisa na lugha za kuobgea tuanze huongea hu hai uone kama hawakuja mbio na misaada kedekede...Acheni utani, its time for Africa and o other countries of the world to say no to this nonsense!
 
Back
Top Bottom