Swali: Escrow ilikuwa abrakadabra? Zitto na PAC watujibu

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,280
25,859
Pamoja na Ripoti 'nzuri' ya PAC chini ya Zitto Kabwe iliyojadiliwa na kuazimiwa na Bunge, mambo yanakwenda tofauti. Wapo watu waliohusishwa na kashfa hiyo ya Escrow lakini CCM na Serikali yake wanaendelea kuwaamini na kusonga nao mbele.

Waziri Muhongo (Profesa Sospeter Muhongo) alijiuzulu kutokana na kashfa hiyo ya Escrow. Alikuwa Wizara ya Nishati na Madini. Mwaka huu, amerejeshwa tena kwenye Wizara hiyo hiyo kwa cheo kile kile (Waziri).

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ndugu Eliakim Maswi naye aliondolewa kwa kadhia hiyo hiyo. Lakini, ameendelea kuaminiwa na Serikali na ni jana tu ameteuliwa kuwa Kaimu Naibu Kamishna Mkuu wa TRA.

Wapo Wabunge akina Prof. Tibaijuka, Ndugu Andrew Chenge na William Ngeleja ambao wote walihusishwa na kashfa hiyo lakini CCM imeendelea kuwaamini na wameshinda majimboni mwao. Hata viongozi wa kidini na hata wa kimahama waliohusishwa nao wanaendelea kudunda. kimsingi hapa patakuwa na jambo kubwa.

Kama si PAC kuudanganya umma, basi Bunge limepuuzwa vya kutosha. Ndiyo maana najiuliza, sakata la Escrow lilikuwa si kitu halisi yaani abrakadabra?
 
Kwangu mimi report ya Escrow ndiyo ilikua report mbovu kuliko zote kuwahi kutolewa katika nchi hii. Nadhani 'utoto' wa wanakamati nao ulichangia. Ubora wa report ya Dr. Mwakyembe ulichangiwa zaidi na ukweli uliosemwa wazi na hadharani kwamba kuna mambo wameyaondoa/wameyaficha ili 'kulinda heshima' ya serikali.
 
Last edited:

Umeuliza maswali ya msingi sana lakini naamini maazimio ya bunge kuhusu escrow yatatekelezwa kikamilifu chini ya rais JPM. Kwa hiyo usihusishe CCM na serikali hii. pale penye jinai hakuna atakayesalimika CCM or anyone else. Wewe subiri majipu hayo yatafikiwa maadam sasa safu za watendaji zimekamilika. We want a new Tanzania isiyovumilia uchafu wa aina yoyote.
 
Mkuu Escrow hata kama ingekua ni uzushi mtupu
mradi ilisomwa bungeni na ikapita na kutoka na maazimio
Zitto hawezi kulaumiwa
kama kunakosa itakuwa bunge lote now....

Bunge lilikuwa na nafasi ya kujiridhisha na kila kitu
 
Mkuu Escrow hata kama ingekua ni uzushi mtupu
mradi ilisomwa bungeni na ikapita na kutoka na maazimio
Zitto hawezi kulaumiwa
kama kunakosa itakuwa bunge lote now....

Bunge lilikuwa na nafasi ya kujiridhisha na kila kitu

Nakupata Mkuu. Nauliza maswali haya kwakuwa siamini kinachotokea. Kuna vita dhidi ya ufisadi kweli hapa nchini?
 
Tumuulize huyu Mbadala wa Mrema wa TLP yeye na kamati yake PAC alikuwa na lengo gani?
Pia walikuwa name report mbili kama ilivyokuwa Richmond?
 
Tatizo la Magufuli anawaamini sana TISS..
kwa hiyo TISS wakikupenda hata uwe mwizi kwa Magufuli utapeta
cc @Pasco ....huyo Maswi ni 'mwanakitengo'
mkuu magufuli amekuepo ndan ya bunge lililopta, pengine labda kuna mengi anayajua kuhusu undani wa ESCROW zaid ya sisi wananchi wa kawaida 2navyoifaham ESCROW, haraf pia 2kimnnkuu huyu ztto mwenyewe 'usiamini maneno ya mwanasiasa yeyote hata mm (mwenyewe zitto)' haraf pia mkuu THE BOSS unaposema kwamba maguful anawaamin xana TISS, hv nkuulize labda unafikiri mh. rais amwamini nani mwingine ikiwa hata wanasiasa wenyewe hawaaminiki? mm kwa haya anayoyafanya maguful iman yangu kwa wabunge inazd kufifia naona kama huwa wako pale kufitiniana2, yaan ilianza RICHMOND nafkir mmeona CDM walicho2fanyia kwa lowaxa, imekuja ESCROW nafkir 2meona alicho2fanyia maguful na CCM yake kwa kuwarudsha MUHONGO na MASWI. hawa wanasiasa hawaaminiki kabxa
 
Last edited:
kama anawaamini tiss 100 %
na hao TISS sio waadilifu basi kazi anayo
 
Escrow ilikua nifitina za matajiri kuzibiti wazalendo.
Nashukuru Mheshimiwa rais kaliona hilo.
Magufuli go! go!go!
 
Tumuulize huyu Mbadala wa Mrema wa TLP yeye na kamati yake PAC alikuwa na lengo gani?
Pia walikuwa name report mbili kama ilivyokuwa Richmond?
Maazimio ya PAC ndio yaliyopitishwa?.

Umesahau kama yalikataliwa,ikabidi iundwe kamati ndogo ya mashauliano ambayo na Mbowe,Zitto,Lukuvi na Wasira walikuwa ndani?.

Wakaja na maazimio ya bunge na sio tena ya PAC?.

Chuki na mihemko huondoa maalifa,kama unamchukia Zitto ni wewe.

Badala yakulaumu bunge zima we unaleta chuki zako kwa Zitto.

Weka mihemko pembeni tujenge nchi.
 
 
Deo Fulikunjombe upumzike kwa amani najaribu kuunganisha dots sipati majibu ila kuna siku ukweli utajulikana
Na Ndio maana Kafulila kafanyiwa ubabe tu asishinde ubunge
 
Last edited:
kama anawaamini tiss 100 %
na hao TISS sio waadilifu basi kazi anayo
cha msingi na cha muhimu kwa mh. rais ni kwamba awe 'anachukua za TISS anachanganya na ZAKE' yy anauzoefu na serikal karibia zote zilizopta akiwa wazir kamili na pia kama naib waziri, kwa hyo anajua wapi pa bovu na wapi pazma, au wapi panahtaj kufanyiwa marekebsho, lakini kama mheshmiwa rais akijiloga na kufanya kazi 'kisiasa' kama wanavyodai kina ZITTO and company. nakuhakikishia mkuu maguful hatafka ppte,
 

labda mahitaji ya hii kazi ni makubwa kuliko uwezo wa TISS na washauri wake
 
Mkuu nimependa hiyo pamoja na ripoti 'nzuri'. Hata hivyo, sikumbuki kama watanzania kuna siku tulikuwa la ripoti 'mbaya'.

Kujua kama Escrow ni kitu halisi au la, tunatumia bunge kupitia kwa ripoti ya ile kamati kutafuta majibu. Lakini kwa kuwa Mwenyekiti wa ile kamati kwa maana hiyo bunge kukubali maelezo ya tume ya maadili kwamba mmoja wa wale watuhumiwa ni msafi, hiyo inafuta uhalisia wa kazi ya ile kamati lakini haufuti ukweli kwamba Escrow scandal is real.

Nilitegemea na niliamini kuwa kamati ilifanya kazi nzuri, ikiwa ni pamoja na kuilinda ile ripoti usiku na mchana. Nakumbuka hata wapishi ilibidi watoke majumbani kwao. Kwa kuwa wao kwa maoni yangu kirahisi sana wamenyosha mikono, wananchi tumekwama.

Hivyo basi, matokeo ya ile kamati ilikuwa siasa zaidi. Swali lingine linaingia hapa, je, tunaweza kuamini bila shaka yoyote matokeo ya ripoti za kamati za bunge? Zina tija au nazo ni majipu?

Mwaka 2015 ulikuwa mzuri kwa wale walio amua kujifunza kitu kuhusu siasa za nchi yetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…