Suzan Peter Kunambi ateuliwa Katibu Mkuu UWT Taifa

Sawa komredi. Ila nauliza tu ni kwa nini kila kiongozi wa kitaifa wa chama akiteuliwa huwa anapewa sifa kedekede na makada wenzake kuwa kamati kuu imepatia kumteua ila akiachwa hakuna sababu za msingi zinazotolewa?

Akiteuliwa mpya naye anamwagiwa sifa pomoni.
 
Hivi kwanini mtu mwenye akili timamu akisha jiunga na hicho chama hua anakua kama amerukwa na akili..🤔
Yaani yanakuaga kama mataarihi....☹️
Mnatia kinyaa sana....😖
Mixxuuuu....😏
 
SUZAN PETER KUNAMBI NI TUNU KWA UWT TAIFA

Na Comrade Ally Maftah
KING OF ALL SOCIAL MEDIA

Kwanza kabisa nitoe pongezi sana kwa chama chetu kikiongozwa na Mwenyekiti wetu Dr Samia Suluhu Hasan.

Kikao cha Halmashauri kuu wa CCM Taifa kilichoketi majuzi Afisi za Makao Makuu ya CCM Zanzibar kimetuletea zawadi ya katibu wa UWT Taifa Ndugu Suzan Peter Kunambi.

SUZAN PETER KUNAMBI NI NANI.
Suzan ni mtangazaji na mwandishi wa habari kitaaluma ambae amefanya mafunzo hayo katika chuo cha Royal Colage na Chuo kikuu cha Zanzibar, na baadae akawa mwandishi wa habari na mtangazaji wa shirika la habari Zanzibar ZBC. ambapo alikuwa kiunganishi kati ya wananchi na serikali kwa kuwasemea wananchi matatizo yao, Suzan alijitoa kwa hali na mali katika kutetea wananchi, kutunza mazingira, kukemea maadili mabaya na kuhimiza ufanyaji kazi kwa bidii kupitia kipaji na nafasi yake ya utangazaji.

Kabla ya kuteuliwa kuwa katibu wa UWT Taifa alikuwa mkuu wa mkoa wa Unguja Magharibi, ambapo alikuwa kipenzi cha wananchi kwa utendaji kazi wake wa kujituma, kutafiti na kushughulikia matatizo ya wananchi.

NAONA NINI UWT.
UWT wamempata katibu anayeendana na hali ya sasa ya technolojia inayokwenda kasi na mabadiliko ya kimitazamo, ni kama UWT imempata mlezi, ambae natailea kuendana na maadili yanayohitajika na kuendana na kazi ya utafutaji.

HONGERA SANA SUZAN PETER KUNAMBI ( KATIBU UWT TAIFA ) - CHAMA KINAJIUNDA, CHAMA KINA HAZINA

NDIMI
Comrade Ally Maftah
Mjumbe Mkutano Mkuu wa CCM & WAZAZI MKOA WA DAR ES SALAAM
Mnatia aibu sana, halafu cha kushangaza wenyewe hamna aibu.

Halafu hiyo King of all social network ulipata copyright kutoka kwa original author Le Mutuz Mobimba Boma Ye? Au ndio maccm kama kawaida yenu kila kitu nyinyi mnakwapuwa tu?
 
Wadau hamjambo nyote?

=======

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imemteua Suzan Peter Kunambi kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT).

Kamati hiyo imeketi chini ya Makamu Mwenyekiti wake ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi, leo Jumapili, Mei 19, 2024 katika kikao chake maalumu, kilichofanyika Afisi Kuu ya CCM, Kisiwandui, Zanzibar na kufanya uteuzi kwa niaba ya halmashauri Kuu ya chama hicho.

HUUU UKOOO MUNGJ MWEMA WAMEANZA KUUKUMBUKA DAH AISEEE

MZEE KUNAMBI ALIIPAMBANIA SANA CCM ENZI ZAKE
 
Back
Top Bottom