Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,825
- 13,584
Mradi huo uliofadhiliwa na SUWASA na kusimamiwa na Fundi Sanifu Ujenzi, Mkami Magesa, umehusisha ulazaji wa mabomba yenye kipenyo cha inchi 2 kwa urefu wa mita 300. Kazi zilizofanyika katika mradi huu ni pamoja na ununuzi wa mabomba, uchimbaji wa mitaro, ununuzi wa viungio, ujenzi wa chemba, na uwekaji wa alama za njia za mabomba ya maji. Jumla ya gharama ya mradi ilifikia shilingi 2,730,000.
Diwani wa Kata ya Mungumaji, Mhe. Hassan Shaban Mkata, ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuboresha huduma ya maji hapa nchini, hatua iliyosaidia upatikanaji wa huduma hiyo katika maeneo mengi, ikiwemo kata yake ya Mungumaji.
Wakazi wa eneo hilo, Ibrahim Haji na John Joseph, walieleza furaha yao kuhusu upatikanaji wa maji safi, wakisema kuwa huduma hiyo itarahisisha shughuli za kila siku na kuokoa muda mwingi ambao walikuwa wanatumia kutafuta maji kutoka maeneo ya mbali.
Imetolewa na
Neema Lulandala-Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma-SUWASA
Neema Lulandala-Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma-SUWASA