Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,583
- 1,189
SUMA FYANDOMO ATUA MBEYA VIJIJINI KUHAMASISHA WANANCHI KUJIANDIKISHA
"Tujiandikishe ili tuweze kumchagua kiongozi ambaye kila mtu anaona anafaa, kila mtu anayo hiari ya kuchagua Kiongozi ambaye anaona anamfaa. Kujiandikisha na kupiga kura ni haki ya msingi ya kila mtu na ndiyo uzalendo wenyewe" - Mhe. Suma Ikenda Fyandomo, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya
Suma Ikenda Fyandomo amefika katika Mji Mdogo wa Mbalizi Halmashauri ya Mbeya DC Jimbo la Mbeya Vijijini kuhamasisha Wananchi kwenda Kujiandikisha ikiwa imebaki siku moja kumaliza zoezi la Uandikishaji kwenye Daftari la Wapiga Kura wa Serikali za Mitaa
"Sisi wenyewe Wanawake tuendelee kuwahamasisha akina Baba waende wakajiandikishe kwa akina Baba wana mambo mengi, wana kazi nyingi, wana majukumu mengi. Akina Baba ni watiifu wanatusikiliza akina Mama" - Mhe. Suma Ikenda Fyandomo
Aidha, Suma Ikenda Fyandomo amewapongeza Wanawake wa Mbalizi Sokoni kwa kuendelea kujituma kufanya kazi za ujasiriamali kwani huo ndiyo msingi wa kukuza uchumi wa familia zao.
Attachments
-
WhatsApp Video 2024-10-19 at 19.20.58.mp439.6 MB
-
WhatsApp Image 2024-10-19 at 19.39.03.jpeg65.7 KB · Views: 1
-
WhatsApp Image 2024-10-19 at 19.39.06(1).jpeg95.5 KB · Views: 2
-
WhatsApp Image 2024-10-19 at 19.39.04(2).jpeg93.2 KB · Views: 1
-
WhatsApp Image 2024-10-19 at 19.39.04(1).jpeg68.4 KB · Views: 4
-
WhatsApp Image 2024-10-19 at 19.39.04.jpeg65.9 KB · Views: 1