You are damn right, huyo jamaa ni vema kuzuiia msg zake, he/she is uncouth and uncultured, tuna rais mzuri na mpenda Tanzania na haijawahi kutokea tangu Mwl Nyerere na mhe Sokoine waondoke!!!!!Kujua kiingerea siyo sifa! Halafu mods iweni wazalendo, mada zinazolenga kumwaibisha Rais wetu fanyeni utaratibu wa kuwa zinaondolewa haraka iwezekanavyo na mhusika kula ban ya maisha kwa ID zake zote!
Mungu ametupa Rais mzuri kama jibu la maombi na kilio cha watanzania halafu anatokea mnufaika wa ufisadi na hasira zake za kitumbuliwa majipu anaanza kumdhalilisha kiongozi wetu MKUU haikubaliki kabisa!
Halafu watu wengine wanashabikia tu vitu vya kijinga bila kujua vina lengo la kumkatisha tamaa kiongozi wetu asiendelee kutumbua majipu! Baba Magufuli usikate tamaa! Kuna watu wanavaa nguo za kijani lakini wana hasira Kali maana hata huko kwenye ukijani majipu yapo lundo! Acha yatumbuliwe tu! Hivi unadhani songo mbingo inayoendelea kwenye umeya wa jiji la Dar ni nini kama siyo kunusuru majipu ya kufa MTU kwenye huo ukijani?
Hata kwenye ubluu majipu yapo tusidanganyane! Ngoja ruzuku ya vyama vya siasa ifuatiliwe mpaka SHILINGI ya mwisho tuone kama kwenye "PIPOOOOS" kuko salama!
Majipu hayana itikadi! Magufuli yatumbue yote!! Kejeli kama hizi zidharau tu na songa mbele!