Suala la Vyeti Feki ni Mbwa kala Mbwa

Sasa kama mtu ana masters na vyeti vya sekondari amefoji.
Ameajiriwa na anafanya kazi kwa ufanisi mkubwa na pengine ni tegemeo katika taasisi au idara utamfukuza kazi ?
 
Mkuu Mmawia unajisumbua bure na haya matangazo ya tv. Kuna mwaka hapa Waziri wa Kazi alitangaza bonge la biti...oooh ikifika tarehe fulani ya mwezi huu, makampuni yote ya nje yaliyoajiri Watanzania kupitia mawakala wa ajira blah blah....watafutiwa ..... thubutuuu! Mpaka leo tunakodishwa kama maturubai. Mtu tu siku akila pilipili analipuka

ni mwaka jana yule waziri wa kazi alitangaza kiama kwa wageni wote cha ajabu wahindi wanazidi kuongezeka........ kuna kiwanda pale tanga wameleta wahindi 6 waje kujifunza........ vijana wetu wanasumbuliwa ili waondoke wabak wahindi....... hii sirikali imejaa wasanii kuanzia unywele wa kichwan mpk ukucha wa dole gumba la mguu..........
 
Sasa kama mtu ana masters na vyeti vya sekondari amefoji.
Ameajiriwa na anafanya kazi kwa ufanisi mkubwa na pengine ni tegemeo katika taasisi au idara utamfukuza kazi ?
Wasiishie kumfukuza, wampeleke mahakamani. Kwa maana kitendo chake cha kufoji cheti cha sekondari ni kosa la jinai
 
Akiuvaa ukauzu na kuamua kutoa kafara, huu msiba ni wa wengi sana.

Hapa tutapata maajabu ya karne ila asiwanyime vijana wetu ajira kwa kisingizio cha kutafuta vyeti feki.
 
KUNA MRATIBU WA ELIMU KATA NI MWEUPE KIELIMU aka ****** MKOA ANAOTOKEA MKULU INADAIWA ANA SHAHADA YA UALIMU. WATU KAMA HAWA WATATUFIKISHA KULE RAIS NA WAZALENDO TUNAKOTAKA KUFIKA?

ELIMU BILA KUWA NA WASIMAMIZI WENYE WEREDI NI BURE
Hao ndio viongozi wa serikali yetu
 
Hebu jieleze vizuri. Nini hasa unauliza?


Nina uliza hivi.
Ikiwa wenye vyeti feki ndio watendaji na wanategemewa katika kutekeleza sheria.
Kwamfano hizi tetesi kuwa kuna mawaziri wa Jpm baadhi yao wana vyeti feki.

Fikiria mpaka mtu anapita mchakato wote wa kuteuliwa kuwa waziri huku akiwa na vyeti feki sijaona kama kuna nia ya dhati.

Bila shaka umenielewa.
 
Good! lakini kuliangalia tatizo kwa jicho 1 ndiko kunakotupelekea kushindwa mengi. Tatizo la elimu nchi hii ni zaidi ya vyeti fake!
 
Back
Top Bottom