Tafakari yetu
JF-Expert Member
- Apr 19, 2021
- 1,505
- 4,425
Kuna suala la wanafunzi watakaoanza kidato cha kwanza ambao hawatakuwa na uwezo wa kununua sare waendelee na zile za shule ya msingi , kauli hiyo ilitolewa na aliyekuwa waziri wa Tamisemi.
Kiukweli nimeona mtazamo wa wengi juu ya suala ,kuna wengine wanasema kwamba sio mbaya waendelee nazo tu kwa sababu sare hazisomi ila ni wanafunzi.
Kuna wengine wanasema kwamba ni vema wakatafuta sare ili kutovunja utaratibu na wanapenda mbali zaidi wakisema sare zina mchango katika kujifunza kwa wanafunzi. Sijui kwa undani umuhimu wa sare na kujifunza kunakoelezewa ,hivyo wataalamu watudadavulie.
Wote, wana hoja za msingi ambao msingi mkuu ni kumpa mtoto fursa ya kupata elimu.
Ninatambua kwamba sasa kuna mabadiliko kwenye wizara ya TAMISEMI na kwamba waziri aliyetoa ushauri huo sasa hayupo kusema lakini tukumbuke tatizo la msingi la wanafunzi kukosa sare litaendelea kuwepo hivyo kama lisipopata muafaka yawezekana kweli wanafunzi wakakosa fursa ya elimu kwa sababu ya sare.
Tanzania ni nchi iliyobarikiwa ardhi kubwa yenye rutuba. Sare za wanafunzi zinatokana na moja ya mazao ya kilimo kama pamba na katani hivyo serikali ihamasishe kilimo cha mazao hayo .
Pia serikali itumie nguvukazi iliyo nayo katika kukuza kilimo cha mazao hayo. Watumike hata wafungwa pia katika kupunguza gharama.
Pia, serikali ije na sare elekezi kwa ajili ya wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza. Kwa mfano, sare za rangi ya bluu na shati jeupo. Serikali kwa kutumia rasilimali ilizonazo kama viwanda watengeneze sare hizo na kuzisambaza mashuleni ambapo mwanafunzi atakayeanza kidato cha kwanza atanunua katika bei ndogo.
Hilo lisiishie hapo tu bali liende hadi kwenye vifaa vingine vya kujifunzia kama madaftari, kalamu na mabegi.
Huu ni muda muafaka kwa serikali kufanya uwekezaji mkubwa na kujenga viwanda vikubwa kwa kazi hii.