Pre GE2025 Stephen Wasira: Wanaogawa hela nawajua, Wapinzani watafaidika kama chaguzi zetu zitakuwa za Rushwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
May 16, 2024
2,299
6,314
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) bara, Stephen Wasira, amewataka wanachama wa CCM katika wilaya za Karagwe na Kyerwa kupunguza matumizi ya fedha katika michakato ya uchaguzi wa ndani ya chama.

Akizungumza na wanachama wa CCM siku ya Jumapili mkoani Kagera, Wasira amekemea vikali tabia ya baadhi ya wagombea kutumia fedha kuhonga wapiga kura badala ya kutegemea maoni halali ya wanachama.

"Mnazidi mno kufanya chaguzi za pesa, biashara gani hiyo? Mwenyekiti wa CCM Kyerwa, waambie watu wako wapunguze sana hela. Wanapata hela za kahawa, lakini siyo kazi ya hela ya kahawa kuhonga," amesema.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Wasira, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Maadili ya CCM amesema ana taarifa za kina kuhusu wagombea wanaotumia fedha kununua uungwaji mkono na kuonya kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

"Unajua mimi ni Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Maadili ya CCM, kazi yangu ni hiyo kucheki cheki. Sasa Kyela mnagawa hela sana! Ninataka niwaambie kuwa tunachunguza na tunajua, na wale magwiji wa kugawa hela tutawaondoa katika orodha ya wagombea."

 
Huyu Babu na mjukuu wake Makalla hawatufai kabisa ndani ya CCM yetu.

Team Mpina.
 
Back
Top Bottom