Starlink yawasilisha maombi ya leseni kwa TCRA. Je, safari hii watatoboa? Ushindani wa gharama na ubora wa internet utakuwaje?

Eli Cohen

JF-Expert Member
Jun 19, 2023
3,024
9,142
Bei zitapungua? Au wataambiwa waendane na bei za washindani zilizopo?

Najua kwenye ubora jamaa atawapiga chenga,

20241115_082129.jpg

Meanwhile hivi ndivyo voda na wenzake walivyo sasa hivi​


=====

Baada ya muda mrefu wa Watanzania kuhoji kwanini Tanzania hatujaruhusu uwepo wa Internet ya Starlink kutoka kwa tajiri Elon Musk, hatimaye leo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa tangazo kuonesha Kampuni hiyo imeomba kupatiwa leseni ya Kitaifa ya Miundombinu na Leseni ya Kitaifa ya Huduma ya Mifumo Tumizi.

IMG_2036.jpeg

Kwa muda mrefu Wananchi wamekuwa wakihoji kwanini Tanzania hatuna huduma hii na hasa ukizingatia kwa wenzetu majirani wanayo; Je, kwanini Tanzania hatupati huduma ya starlink nini shida?

Wakati hapa kwetu kumekuwa na kususua kupokea huduma hii wananchi wakihoji kwanini: Waziri Nape kwanini husemi ni vigezo gani ambavyo Starlink hawajatimiza? Au wamegoma sharti la kuzima mtandao muda wowote mkiamua?

Katika moja ya fafanuzi zake, aliyekuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye alisema kuwa Elon Musk hakuwa na mpango wa kuweka ofisi ya Starlink nchini katika hatua yake ya kuwekeza katika utoaji wa huduma ya intaneti, hivyo ingeweza kuleta usumbufu pale ambapo wateja wangehitaji msaada zaidi.

Na haya yalikuwa majibu ya Nape, kuwa serikali haikuwa imeweka vikwazo vyovyote ila bwana Elon hakuwa na mpango wa kuanzicha huduma hiyo nchini: Waziri Nape: Elon Musk hakuwa na mpango wa kuweka ofisi Tanzania

Hata hivyo, Februari mwaka huu, akiwa bado Waziri, Nape Nnauye alisema Kampuni hiyo inakamilisha hatua za mwisho ili kupata vibali vya kutoa huduma nchini. Aliongeza kuwa ikishatimiza taratibu zote itaanza kutoa huduma na kwamba Serikali inasubiri wakamilishe tu taratibu hizo.

Sasa hivi Kampuni hiyo imeomba leseni tena na TCRA kwa sasa imeweka wazi kabisa uombaji huo tofauti na awali ambapo haikuwa wazi. Sasa maswali ya kujiuliza ni

  1. Bei zitapungua? Au wataambiwa waendane na bei za washindani zilizopo? Najua kwenye ubora jamaa atawapiga chenga
  2. Je, sasa hivi amekubali kujenga ofisi au ile ilikuwa janja janja ya kipindi kile?
 
Back
Top Bottom