SSRA: Ufafanuzi kuhusu uraia wa Dr. Carina Wangwe

Wewe na utanzania wako wa kuzaliwa umeisadia nini nchi yako?? Sana sana wewe ni mzigo kwa nchi hii. Acha watu wafanye kazi kuleta maendeleo ya nchi.
Mbona unaushushia hadhi uraia wako to that extent kwa maneno yako kama hayo nadhani unaweza ata chagua raisi raia wa kigeni.
Rejea elimu yako ya uraia ndugu umenikwaza na sishangai watz wengi wako na metality kama yako.
Tuondokane na mawazo kama hayo pls pls.
Msimamo wangu so far hawa wageni wako na post nyingi kwa private companies na ata public but sensitive post stricly no kwao kushika izo post.Tuko na watz wengi.
Kumbuka 'Zimwi likujualo halikuli likakwisha"
 
Hatuna watanzania halisi wenye sifa? Kama huko nyuma ilishafanyika haina maana na wakati huu ambao tuna wasomi kila sekta tuendelee kuwatumia wakuja.

..ni bora basi ikapitishwa sheria kwamba uraia wa Tz upatikane kwa kuzaliwa tu.

..labda nikuulize: je hawa raia wa kuandikishwa wanazuiwa kwenda vitani kuilinda Tz?

..kama wanaweza kwenda vitani, kwanini wanyimwe kutumikia shirika kama nssf?
 
Kuna level za uongozi ambapo huwezi kutenga nasfi na kazi.

Huyo ni Mkuu wa Idara SSRA sio DG na hata DG hawezi kutetewa na ofisi. DG wa IMF alisingiziwa kubaka Mwanamke mweusi kule Washington mchezo uliochezwa Rais wa Ufaransa ili asiwanie Urais, uliwahi kusikia IMF imetoa statement?
Bill Clinton alipokutwa na kashfa ya Uzinzi wa Monica Lewinsky uliwahi kusikia Press release ya White house?
Kama hayo ya Zamani umesahau jikumbushe Kashfa ya Blatter FIFA hivi karibuni uliona press release ya FIFA? AU hiyo kanuni ni kwa Tanzania tu?
 
Hatuna watanzania halisi wenye sifa? Kama huko nyuma ilishafanyika haina maana na wakati huu ambao tuna wasomi kila sekta tuendelee kuwatumia wakuja.

..inawezekana mpaka kuandikishwa kuwa Mtanzania na kuachana na huko alikozaliwa basi ana maslahi na nchi hii.

..unaweza ukakuta ameolewa hapa, ana watoto amewazaa na kuwalea Tanzania, ana mali zisizohamishika etc etc.

..kuwa Mtanzania "halisi" siyo guarantee ya utumishi uliotukuka kwa nchi hii. tuna mafisadi wengi tu ambao ni wa-Tz "halisi."

..Salama yetu ipo ktk kuhakikisha kwamba vyombo vya dola vinakamata wote ambao wanavunja sheria. Vinginevyo tutaendelea kuishi kwa kuhisiana na kutoaminiana kuwa huyu Mtanzania "halisi" na huyu wa "kuandikishwa."
 
..tumeshapata kuwa na Jaji Mkuu ambaye siyo Mtanzania.

..tumewahi kuwa na mkurugenzi wa mashtaka[dpp] siyo Mtanzani, alikuwa mkimbizi toka South Rhodesia[zimbabwe].

..tumewahi kuwa makamu mkuu wa chuo kikuu siyo Mtanzania.

..tumewahi kuwa na mhariri wa magazeti ya serikali siyo Mtanzania.

..tumewahi kuwa na mkurugenzi mkuu wa Tanroads siyo Mtanzania.

..kabla ya kumshambulia huyo mama tuletee kipengele cha sheria kinachokataza raia wa tanzania wa kuandikishwa kuongoza shirika la umma kama nssf.

cc Pohamba
Asante sana
 
KWA HOJA ZENU HAPO JUU INAMAANA WAZIRI,IKULU USALAMA WA TAIFA,UHAMIAJI WOTE HAWAKUWA NA PROFILE YA URAIA WAKE HAPO KABLA .MABADIRIKO YANAHITAJIKA TANZANI.NA MPAKA DAKIKA HII TUNAPOST POST HAKUNA ALIYENUKUU SHERIA YA URAIA JAPO TUNAJUA RAIA TUNA HAKI SAWA.
 
..tumeshapata kuwa na Jaji Mkuu ambaye siyo Mtanzania.

..tumewahi kuwa na mkurugenzi wa mashtaka[dpp] siyo Mtanzani, alikuwa mkimbizi toka South Rhodesia[zimbabwe].

..tumewahi kuwa makamu mkuu wa chuo kikuu siyo Mtanzania.

..tumewahi kuwa na mhariri wa magazeti ya serikali siyo Mtanzania.

..tumewahi kuwa na mkurugenzi mkuu wa Tanroads siyo Mtanzania.

..kabla ya kumshambulia huyo mama tuletee kipengele cha sheria kinachokataza raia wa tanzania wa kuandikishwa kuongoza shirika la umma kama nssf.

cc Pohamba
Siyo tukuletee soma mwenyewe katiba pia kama walikuwepo basi sheria zirivunjwa tusigawe nafasi nyeti kwa waveni nirahisi nchi kuuzwa ? Mtanzania take care
 
acheni kelele wenzenu wanapopandishwa vyeo..mnatumbuliwa majipu ili nafasi zenu wapewe walioandaliwa
 
Getstart, Pohamba, Rangi za nyumba , Njowepo,

..Dr.Wangwe ana PhD ktk mambo ya IT.

..sasa tuache kumtumia kwasababu ni Mtanzania wa "kuandikishwa"?

..Wamarekani walitumia mpaka wanasayansi wa Nazi German ktk program zao za nuclear na space.

..Namibia walimtumia Mtanzania Prof.Keto Mshigheni na amewasaidia sana ktk uanzilishi wa univ of namibia na program ya marine biology.

..Rwanda wametumia maprofesa wa engineering toka udsm ktk chuo chao kikuu.

..Watanzani tujifunze kuiba wataalamu toka nchi nyingine na kuwatumia kwa manufaa yetu.
 
Nilikuwa na wazo kama ilo maana apo ndo wameharibu .
Raia wa kuandikishwa kweli mnampa taasisi kubwa kama ilo jamani si dharau hii kwa watanzania by birth.
Lets be serious jamani na inchi yetu pls this is the only country we have maslai binafsi wekeni kando.

Mkuu SSRA Hawahawa ambao wanashuhudia manyanyaso tunayopata kwenye mifuko ya jamii ! hawahawa tuliogombana juu ya fao la kujitoa wakiangalia? Sjawahi kuwa na imani nao na nadhani kujenga imani nao it is a process not overnight show!
 
I knew it before, serikali isingenyamaza kimya. wamejua kwamba wametoa "boko''. Kufunika sasa wanatumia nguvu zote to make the issue clear.....
;):cool:
 
..tumeshapata kuwa na Jaji Mkuu ambaye siyo Mtanzania.

..tumewahi kuwa na mkurugenzi wa mashtaka[dpp] siyo Mtanzani, alikuwa mkimbizi toka South Rhodesia[zimbabwe].

..tumewahi kuwa makamu mkuu wa chuo kikuu siyo Mtanzania.

..tumewahi kuwa na mhariri wa magazeti ya serikali siyo Mtanzania.

..tumewahi kuwa na mkurugenzi mkuu wa Tanroads siyo Mtanzania.

..kabla ya kumshambulia huyo mama tuletee kipengele cha sheria kinachokataza raia wa tanzania wa kuandikishwa kuongoza shirika la umma kama nssf.

cc Pohamba
Duh!!! haya mambo mageni kabisa kwangu. hadi jaji mkuu wa kuja? aisee kumbe napaswa kuijua zaidi my Tz, japokuwa ni mzaliwa tena hapa dar
 
Getstart, Pohamba, Rangi za nyumba , Njowepo,

..Dr.Wangwe ana PhD ktk mambo ya IT.

..sasa tuache kumtumia kwasababu ni Mtanzania wa "kuandikishwa"?

..Wamarekani walitumia mpaka wanasayansi wa Nazi German ktk program zao za nuclear na space.

..Namibia walimtumia Mtanzania Prof.Keto Mshigheni na amewasaidia sana ktk uanzilishi wa univ of namibia na program ya marine biology.

..Rwanda wametumia maprofesa wa engineering toka udsm ktk chuo chao kikuu.

..Watanzani tujifunze kuiba wataalamu toka nchi nyingine na kuwatumia kwa manufaa yetu.
Wanaodai hayo ni wapiga blaablaa tu. Hakuna sheria au katiba inayozuia mtanzania aliyeandikishwa au hata expatriate kufanya kazi yoyote ambayo ana ujuzi nayo.
 
Back
Top Bottom