Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 1,191
- 2,899
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Dk. Tulia Ackson, amewajulia hali baadhi ya Wabunge majeruhi, waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam, waliopata ajali ya gari mkoani Dodoma wakati wakielekea kwenye Mashindano ya Michezo ya Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Mombasa nchini Kenya Disemba 6, 2024.
Dkt. Tulia alifika katika Hospitali hiyo akiwa ameambatana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene.
Dkt. Tulia amewapa pole Wabunge waliojeruhiwa na kuwatakia uponaji wa haraka ili waweze kurejea katika majukumu yao ya kila siku.