South Sudan vows to shut down oil fields, pipeline over high transportation fees

Yapo makubaliano ya South Sudan kupitisha mafuta Sudan inapaswa kulipwa US$ 15 kwa barrel inaitwa rehabilitation fee pia wanalipa transit fee ya US$ 9.5, hivyo kabla ya kufikia mwafaka na GOSS vizuri kuwekana sawa na Al Bashir. Africa fursa ni nyingi mno hamna haja ya kusumbuka na MCC fund.
Kweli mkuu
mambo ya Mcc yanakera kiukweli
 
Mkuu according to BBC sources, hii agreement ya kupitisha mafuta Sudan ilisainiwa baada ya South Sudan kuwapigia magoti Khartoom na ilikua ni business deal tu haikua part ya agreement.

Sudan baada ya South kujitenga ilipiga marufuku South kutumia miundombinu yake kusafiishia mafuta kama sehemu ya kuwakomoa , ikabidi South awe mpole tu na mwaka 2012 ndipo akakubaliwa kusafirisha mafuta baada ya kwalilia na kukubali kuachia $24.5 per pipa moja.

Means kwamba makubaliano haya hayakuwa ya wao kupewa uhuru wao(kujitenga) isipokuwa ilikua ni business deal tu na aliye enda kui-nitiate ni South Sudan, na kwa kuwa ni business deal inaweza kuvunjwa wakati wowote, kama utatokea mbadala wa kusafirisha haya mafuta
Hili Dili mbona linaanza kuwa laini, tumtume sasa Dr.Mataragio akasake hii fursa wakati mchuzi haujapoa, napendekeza JPM ampeleke Dr Dau awe balozi South Sudan tufungue na ubalozi kabisa najua huyu mzee kwa fursa nayeye mzima.
 
lile bomba ni mali ya sudan kusini.Ndio maana muda wowote waweza lifunga hata kuling`oa wakitaka.Ni mkataba wa kawaida wa kibiashara.

Njia ya Sudan kusini kupitisha mafuta yake Tanga ni kuingiza mafuta yake soko la afrika mashariki na kati badala ya kusubiri kuyasafirisha nchi za mbali.Gharama zake zitashuka chini na atauza kwa faida sababu yakitua tu Tanga malori ya kutoka Africa Mashariki na kati yatafurika pale kubeba mafuta hana haja ya kupeleka ma ulaya au wapi.Soko hapa hapa
Linaweza kuwa sahihi
hilo
 
Sudan kusini imeingizwa kwenye jumuiya ya Afrika mashariki kama mwanachama.Igeukie upande huu wa Afrika mashariki haina haja kujikomba kwa wasudan kaskazini ambao ni wanachama wa jumiya ya nchi za kiarabu.Sudan kusini aje kwa waswahili wenzie aunge bomba na kampala hadi Tanga
Ni kweli kabisa, tatizo nchi zetu za Afrika ziko hoi sana kiuchumi, hata uwezo wa kulijenga hilo Bomba ni shughuli.
Mganda tu kashindwa kujenga mwenyewe inabidi Total ndie ajenge, Kenya walitaka kujikoki kwa kuchangamkia hii deal kwa kukopa lakini naona iashu imewageuka kidogo.
Kama tunaweza kupata mtu wa kutukospesha hela tunaweza ku-share deni na Uganda na Sudani Kusini yenyewe halafu tukajenga bomba au kupanua hili lililopo toka Juba mpaka Tanga, itakua bonge la deal
 
Hawawezi kujenga kirahisi hivyo, kumbuka wana mkataba na sudani, wakivunja mkataba inaweza kutokea vita
Al Bashir akilianzisha ajue anapambana na Uganda Tanzania Ufaransa China Ireland, yaani ndio tunamkamata na kumpeleka ICC.
 
Hofu ni Uganda atakubari
Maana waliopewa wote kukaa zizi moja huwa taabu

Ifikie mahali nchi zetu zipigane hata vita kwa maslahi ya kiuchumi na sio siasa tu.Majeshi ya Uganda yamekuwa yakipigana kuisaidia sudan kusini kwa muda mrefu ni wakati sasa wa Uganda kuona ni wakati muafaka wa kufanya biashara kubwa na sudan.Hilo bomba likipita Uganda atakuwa akilipwa!
 
lile bomba ni mali ya sudan kusini.Ndio maana muda wowote waweza lifunga hata kuling`oa wakitaka.Ni mkataba wa kawaida wa kibiashara.

Njia ya Sudan kusini kupitisha mafuta yake Tanga ni kuingiza mafuta yake soko la afrika mashariki na kati badala ya kusubiri kuyasafirisha nchi za mbali.Gharama zake zitashuka chini na atauza kwa faida sababu yakitua tu Tanga malori ya kutoka Africa Mashariki na kati yatafurika pale kubeba mafuta hana haja ya kupeleka ma ulaya au wapi.Soko hapa hapa
Soko hapa hapa???? Unajua mafuta yakishachimbwa yanapita sehem ngapi hadi yafae kutumika?
 
Ni kweli kabisa, tatizo nchi zetu za Afrika ziko hoi sana kiuchumi, hata uwezo wa kulijenga hilo Bomba ni shughuli.
Mganda tu kashindwa kujenga mwenyewe inabidi Total ndie ajenge, Kenya walitaka kujikoki kwa kuchangamkia hii deal kwa kukopa lakini naona iashu imewageuka kidogo.
Kama tunaweza kupata mtu wa kutukospesha hela tunaweza ku-share deni na Uganda na Sudani Kusini yenyewe halafu tukajenga bomba au kupanua hili lililopo toka Juba mpaka Tanga, itakua bonge la deal
tumejenga Mtwara Dar km 660, hizo 112 tunaweza jenga bila shida, isitoshe Total wanasema pesa sio tatizo.
 
Ifikie mahali nchi zetu zipigane hata vita kwa maslahi ya kiuchumi na sio siasa tu.Majeshi ya Uganda yamekuwa yakipigana kuisaidia sudan kusini kwa muda mrefu ni wakati sasa wa Uganda kuona ni wakati muafaka wa kufanya biashara kubwa na sudan.Hilo bomba likipita Uganda atakuwa akilipwa!
Na itasaidia kwa kiwango kikubwa k unafuu wa bei ya mafuta kwa nchi zisizo na mafuta
 
Kama tunaweza kupata mtu wa kutukospesha hela tunaweza ku-share deni na Uganda na Sudani Kusini yenyewe halafu tukajenga bomba au kupanua hili lililopo toka Juba mpaka Tanga, itakua bonge la deal

Mkuu nchi zikikubali ishu ya kupata wawekezaji kama Total sio shida.Wawekezaji wanajua wakijenga bomba kama hilo ni lifetime investment ukishamaliza kujenga wewe unabaki kula pesa tu ya kuchaji gharama za usafirishaji(Transport fee) kwa kila pipa.Kinachotakiwa ni viongozi wakubaliane wauze huo mradi yatajitokeza makampuni kama hiyo ya TOTAL ilivyofanya.

Lakini njia nyingine ya kupata pesa za huo mradi si kukopa ni kuuza hisa.Serikali zaweza unadi huo mradi kwenye masoko ya hisa uone kivumbi kitakavyotimuka pesa itakuja mbio.Wafanyabiashara wakubwa na makampuni makubwa ya kimataifa yaweza mwaga pesa za kuua mtu sababu wanajua una faida.Pesa si tatizo tatizo makubaliano.
 
Kwani Bashir ni wa south sudan??? Au una maana gani???
Tumtume JK aende UN akawashawishi waondoe hati ya kukamatwa kwa Al Bashir kwa kubadilishana na hili dili la mafuta, nusu yapite Port Sudan na Nusu yapite Tanga kupitia kampala.
 
Ifikie mahali nchi zetu zipigane hata vita kwa maslahi ya kiuchumi na sio siasa tu.Majeshi ya Uganda yamekuwa yakipigana kuisaidia sudan kusini kwa muda mrefu ni wakati sasa wa Uganda kuona ni wakati muafaka wa kufanya biashara kubwa na sudan.Hilo bomba likipita Uganda atakuwa akilipwa!
Uganda inabidi aamke sasa, kwa miaka mingi amekuwa hana ally wa kiuchumi kutokana na geographia yake, lakini naona sasa angalau kapata ally mzuri wa upande wa north.

Tatizo amezubaa mpaka mkenya anataka kumpokonya. Ngepambana kufa kupona South Sudan apitishe mafuta yaku Uganda mpaka Kampala, hii ingekua nafuu sana kwake
 
Napendekeza Raisi Magufuli na Museveni waishawishi Sudani kusini ijenge bomba la mafuta kutoka Sudan kusini hadi uganda ili waunganishe na lile linalokuja Tanzania mafuta yao yaje yaondokee bandari ya Tanga .Bomba hilo likitumiwa na nchi hizo mbili litawasaidia Uganda pia kupunguza gharama za uendeshaji kwani watakuwa wana-share na sudan kusini,

Faida ya Sudan kusini kujenga hilo bomba kupitia Uganda ni kama ifuatavyo

1.Usalama wa hilo bomba kwani linapita maeneo ambayo raia wa sudan kusini na wale wa kaskazini mwa uganda ni ndugu.Wametenganishwa tu na mpaka.Bomba halitapita maeneo ya waasi au yenye tishio la Alshababu

2.Uhusiano wa Uganda,Tanzania na sudan kusini ni mkubwa na wa kuaminika
3.Kwa kupitisha mafuta eneo hilo Sudan kusini itaweza uza mafuta yake kwenye masoko makubwa ya Tanzania,Kongo,rwanda,burundi,Zambia,Malawi na kenya kirahisi pamoja na kusafirisha nje ya nchi kirahisi
4.Umbali wa Kujenga bomba kutoka sudan kusini hadi uganda ni karibu kuliko kulijenga kwenda bandari ya Lamu.Angalia Ramani

east_africa.jpg
Item number 4, mafuta wanayozungumziwa ni ghafi, crude oil, kama sisi tunaweza kutangulia kimawazo, tutengeneze oil refinery hapa (JPM ameshauri hili tayari), ili kusafisaha hapa na kuwezesha kutumika katika nchi tajwa, pamoja na sisi.

Nahisi ndo Sudan Kusini wamekubaliwa kuingia EA commutnity
 
Hawawezi kujenga kirahisi hivyo, kumbuka wana mkataba na sudani, wakivunja mkataba inaweza kutokea vita

Kama vifungu vya mkataba vinafafanua hivyo, kwamba wakishindwana wapambane kivita ( kitu ambacho hakipo kisheria na kimaadili), lakini hili la kuwachimbia wenzao kweli linawaumiza sana, Khatoum wao wanakamata USD 24 wao tano tu, duh, huu ni kama mikaba yetu ya madini!
 
lile bomba ni mali ya sudan kusini.Ndio maana muda wowote waweza lifunga hata kuling`oa wakitaka.Ni mkataba wa kawaida wa kibiashara.

Njia ya Sudan kusini kupitisha mafuta yake Tanga ni kuingiza mafuta yake soko la afrika mashariki na kati badala ya kusubiri kuyasafirisha nchi za mbali.Gharama zake zitashuka chini na atauza kwa faida sababu yakitua tu Tanga malori ya kutoka Africa Mashariki na kati yatafurika pale kubeba mafuta hana haja ya kupeleka ma ulaya au wapi.Soko hapa hapa
Maroli yatapakia ikiwa yamesafishwa, crude/ghafi bado yanahitaji gharama ya kusafishwa ndipo yatumike, mawazo yangu ilikuwa sisi TZ tujenge refinery hapa ili kuongeza faida.
 
mafuta wanayozungumziwa ni ghafi, crude oil, kama sisi tunaweza kutangulia kimawazo, tutengeneze oil refinery hapa (JPM ameshauri hili tayari), ili kusafisaha hapa na kuwezesha kutumika katika nchi tajwa, pamoja na sisi.

Sudan kusini wanazo oil refinery zao,Uganda pia wanayo ya kwao moja hivyo mafuta ya Sudan kusini kuja kwetu yatafika yakiwa tayari kuingia sokoni.
 
kuna mkataba wa kusafirisha mafuta kati ya sudan na sudan ya kusini, ili kuepusha kuingia vitani ni vizuri kuweka mambo sawa.

Ukifikiria worst case, iwapo watafunga uzalishaji, watalazimishwa kupigana? kwa sababau ina kuwa hamna faida sasa, mpaka gharama za uzalishaji zitazidi na kuwa mzigo!
 
Sudan kusini wanazo oil refinery zao,Uganda pia wanayo ya kwao moja hivyo mafuta ya Sudan kusini kuja kwetu yatafika yakiwa tayari kuingia sokoni.

Sidhani mkuu, hii wanayozungumzia ni crude, kama yangekuwa ni tayari kwa matumizi basi wangesema kama ni mazao yake (products). refer hii Quote; The price of crude oil is currently at $29 dollars per barrel in the international markets.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom