Soma mashairi ya Wimbo wa Jumuiya Afrika Mashariki (Jumuiya Yetu)

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,106
10,178
Haya usipate tena aibu ukienda kwenye vikao vya maana kwa kushindwa kuimba wimbo wa Afrika mashariki. Kariri Mashairi haya ukienda sehemu kwenye hiyo kitu unaimba.

Ubeti ya kwanza
Ee Mungu twaomba uilinde
Jumuiya Afrika Mashariki
Tuwezeshe kuishi kwa amani
Tutimize na malengo yetu.

Kiitikio
Jumuiya Yetu sote tuilinde
Tuwajibike tuimarike
Umoja wetu ni nguzo yetu
Idumu Jumuiya yetu.

Ubeti wa Pili
Uzalendo pia mshikamano
Viwe msingi wa Umoja wetu
Natulinde Uhuru na Amani
Mila zetu na desturi zetu.

Rudia kiitikio

Ubeti wa tatu

Viwandani na hata mashambani
Tufanye kazi sote kwa makini
Tujitoe kwa hali na mali
Tuijenge Jumuiya bora.

Rudia kiitikio

Kama kawaida tunamaliza kwa kupiga makofi mengi

 
Waandamizi wote wanaohudhuria sehemu hizo wapewe nakala za huo wimbo wakariri kuepusha aibu ndogo ndogo
 
Imetungwa na mbongo tu uyo, kwa maana naona mashairi km ya bongofleva.
 
Heeh ngoja tuongeze...

Tanzania Tanzania

Mungu ibariki Africa

Na sasa Mungu ibariki Afrika mashariki
 
Back
Top Bottom