Soma biblia kama mwanafunzi anayejiandaa kufanya mtihani

Gulio Tanzania

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
2,223
4,725
Habari zenu wadau nimewaletea somo hili muhimu kwa wale wote wakristo kwa lengo la kufundishana na kukukumbasha ili sote tuweze kutenda sawa sawa na maandiko yanavyotutaka

Biblia inafundisha kila kitu katika maisha yetu haya tunayoyaishi

Biblia inatufundisha kufakari neno la Mungu usiku na mchana

Yoshua 1:8-9
Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.

Wakati Musa kufa Yoshua ndie aliyepewa nafasi na Mungu ili aweze kuwaongoza Wana wa Israel kufika mji wa caanan

Mungu anamuambia Yoshua kitabu hichi Cha torati kisiondoke kinywani mwako....hii inatufundisha Nini wakristo ? jibu ni kwamba neno la Mungu linatakiwa likae kichwani na sio kubakia kwenye kitabu Cha biblia

Watu wengi Wanasoma biblia kama gazeti ipo mistari ya biblia wakristo wengi wameikalili lakini hawajui imeandikwa kwenye kitabu gani au mstari gani jambo hili nazani tulikuwa tunakosea sana na wengi hawafahamu

Biblia inatufundisha kuwa neno la Mungu lisitoke kinywani mwetu Yani ni kama unaingia chumba Cha mtihani unakutana na swali linakuuliza mithali 4:23 imeandikwa Nini utaweza kujibu?

Inatukumbusha pale mafarisayo walipomfuata Yesu nakumuambia kwanini wanafunzi wako wanavuna ngano siku hii ya sabato Yesu aliweza kuwajibu hapo hapo

Mt 12:1-8
Mt 12:1-8 SUV
Wakati ule Yesu alipita katika mashamba siku ya sabato; wanafunzi wake wakaona njaa, wakaanza kuvunja masuke, wakala. Na Mafarisayo walipoona, walimwambia, Tazama! Wanafunzi wako wanafanya neno ambalo si halali kulifanya siku ya sabato. Akawaambia, Hamkusoma alivyotenda Daudi, alipokuwa na njaa, yeye na wenziwe? jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu, akaila mikate ile ya wonyesho, ambayo si halali kwake kuila wala kwa wale wenziwe,

Hapa utaona ni namna gani inatufundisha Yesu hakuacha ata nukta katika torati katika kutafakari usiku na mchana ata Yale yaliyotabiriwa kuhusu kifo chake huku mafarisayo wao walishasahau kama kwenye ufalme wa daudi njaa ilipotokea alikula Ile mikate wenzie

Kushuka kwa roho mtakatifu Ile siku ya pentekoste watu walinena kwa lugha siku Ile watu wengi walianza kushangaza labda wale watu wale kuzani wamelewa Petro akawajibu

Matendo 2:16
kweli ni kwamba jambo hili ni lile alilosema nabii Yoeli:
1Katika siku zile za mwisho, asema Bwana,
nitawamiminia binadamu wote Roho wangu.
Watoto wenu wa kiume na wa kike watatoa unabii,
vijana wenu wataona maono,
na wazee wenu wataota ndoto.
18Naam, hata watumishi wangu wa kiume na kike,
nitawamiminia Roho wangu siku zile,
nao watatoa unabii.

Hapa biblia inatufundisha kuwa ata Petro mtume wa Yesu neno kitabu kile hakikumtoka kinywani mwake na ndio mana wakati watu wengine wanashangaa yeye aliwakumbusha kwa utabiri ule alioutoa nabii Yoeli 2:28 aliwakumbusha wale watu walikuwa wakishangaa mana wao Kuna uwezekano walikuwa wameshaliacha kuishika torati

Tuangalie Nini sasa faida ya kulishika neno la Mungu lisitoke kinywani mwako

Moja kwa moja Kuna nguvu ya roho mtakatifu Ile nguvu ya utendaji wa kazi ya Mungu kujazwa ndani yako hapa kila jambo utaloweza kumuomba Mungu ataweza kulijibu kwa wakati kila jambo utalolifanya litaleta matokeo iwe kazi,biashara ,kutoka katika magojwa

Kulishika neno la Mungu lisitoke kinywani mwako ni Siri kubwa sana yakutatua matatizo yako kiurahisi

Angalia muongozo:
Kusanya vifungu vya biblia vinavyozungumzia roho mtakatifu soma biblia andika kila siku kitabu na mstari wa biblia hakikisha unaishika na kuitafari kama mtu unayejiandaa na maandalizi ya kufanya mtihani

Kusanya vifungu vya biblia vinavyozungumzia hekima,busara na maarifa soma biblia andika kila siku kitabu na mstari wa biblia hakikisha unaishika na kuitafari kama mtu unayejiandaa na maandalizi ya kufanya mtihani

Ikiwa unasumbuliwa na magojwa unataka kutoka katika magojwa kusanya vifungu vyote vyakukombolewa kutoka katika magojwa soma biblia andika kila siku kitabu na mstari wa biblia hakikisha unaishika na kuitafari kama mtu unayejiandaa na maandalizi ya kufanya mtihani

Mtu kama unataka upate kazi fanya hivyo hivyo

Mtu unataka kupata mafanikio ya kazi yako fanya hivyo hivyo nk

Fanya haya ndani ya miezi mitatu

Naamini kwanzia sasa unaenda kubarikiwa na utastawi kama biblia inavyotufundisha kwa jina la Yesu
 
Back
Top Bottom